Majibu ya Serikali (Wizara ya Nishati na Madini) kuhusu ripoti ya PAC juu ya Tegeta Escrow Account

Escrow inatoa picha nzuri jinsi maadili kwenye uongozi nchi hii yalivyoshuka. Watu wamebeba hela kwenye mifuko ya rambo, mabox, lakini viongozi bila haya wanatetea, tena bungeni? Waziri anapata hela toka kwenye kampuni ambayo iko chini ya wizara anayoongoa lakini anasema hakuna tatizo!

Hili suala la PAP Kugawa fedha kwa Viongozi amejitahidi kulikwepa.Nafkiri alikosa namna ya kulitolea ufafanuzi.

Pia Shutuma dhidi ya Mkono hata kama zina Ukweli kiasi gani,hazikupaswa kupewa uzito mkubwa kama alivyofanya.

Suala la kodi kutoka fedha za ESCROW Ndio kabisa sijamuelewa.Ni vipi haikulipwa TRA na ikatoka BOT? Ni vp TRA waanze kufuatilia upya kodi badala ya Wizara yake kurahisisha makusanyo hayo?
 
Hili suala si la watu tu kuachia madaraka. Hapa inatakiwa kieleweke ile pesa waliyopewa kila mmoja airudishe yote na hatua za ziada kuchukuliwa. Ila kwa system tunayopelekwa nayo tuombe Mungu atusaidie tufikie lengo kuu la sivyo tutapiga kelele tu humu alafu watu wataendelea tu kwenda na VIROBA katika benk kuchota. Inauma sana.

Mgavi Fulani naachia line.
 
Mbona sijaona majibu ya sababu ya malipo waliopewa fedha zilikuwa za kazi gani hasa watumishi was serikali.
 
We tulia kwanza prof amefanya nini la maana? Zaidi ya kudefence matatizo na watawala wenzake? Kama ulikuwa makini kumsikiliza wanachotaka kufanya ni kutumia dola kujilinda. Hotuba yake ni sawa na mwizi amepewa wakati kujitetea mahakamani huku akijua vema jela inamngojea wadhani atafanya makosa?
vox populi vox dei
 
Escrow inatoa picha nzuri jinsi maadili kwenye uongozi nchi hii yalivyoshuka. Watu wamebeba hela kwenye mifuko ya rambo, mabox, lakini viongozi bila haya wanatetea, tena bungeni? Waziri anapata hela toka kwenye kampuni ambayo iko chini ya wizara anayoongoa lakini anasema hakuna tatizo!


Mkuu, kuna mambo mi nadhani unaweza kuyapata hapa kwetu pekee yani serikali inajipanga kujibu hoja zilizoelekezwa kwake ili ijrekebishe na kuwapatia unafuu wananchi yenyewe inajipanga kutetea walioiba pesa ili kujineemesha alafu unakuta watu wakawaida tu kama mimi tunakuja kwenye mitandao kufurahia uporaji, kuna wakati najisikia aibu kuwa na ndugu wa aina hii eti ni waTZ wenzangu
 
Kufuatana na utetezi wa muhongo, pesa za escrow si za umma bali ni za iptl. Kama hii ni kweli, singasinga kapata wapi ukarimu wa kugawa au kutapanya hela kwa watanzania? Naomba jibu tafadhali
 
Mburula ni wewe na nani.......zako,wewe hujui cha moto au sio mtanzania,unataka kuning'oa kucha bila ganzi? utaniweza? jaribu unaweaz ukawa na bahati hiyo
Sasa ni shujaa gani huyo anayetaka kwenda peponi bila kufa? Yaani unasema unataka jamaa waone cha moto wakati huo huo unajificha nyuma ya keyboard? Ndio maana nikakuuliza, au hicho cha moto ndio hizi posts za hapa JF? Watu walio serious na wanachokimaanisha huwa hawaogopi kama mbwa jike kama wewe, hebu rejea Tunisia, Misri, Syria, Hong Kong, USA na kwingineko uone jinsi wanaume wanavyojua kuonyesha vya moto wazi wazi pasipo kuogopa watoa kucha na meno kama wewe! Shame on you for showing how coward you are! Just cover your ass mbwa wee! Kusema ni rahisi, ila vitendo sasa......Ingekuwa hivyo basi Tz ingekuwa kama USA.
 
hivi lizaboni na msalani mna akili kweli au mnafanya comedy?

Hajajibu maswali mengi ambayo mwananchi wa kawaida anajiuliza.Amekuwa mwanasiasa zaidi kuliko kutoa facts za kupinga report ya CAG na Takukuru.
 
Amazing! Nilidhani watakubali yaishe kama EL kumbe wamejipanga kupambana, naona vita imekuwa kubwa kuliko wengi tulivyodhani.
 
Nilifikiri kuwa issue ni ufisadi!, kumbe issue na this time ni uwaziri mkuu?!, mkidhani itakuwa simple kama ile ya Richmond?!.

This time!, No way!.

Pasco.

Mkuu Pasco Nakuheshimu sana sana ila kwa hili unaniangusha mno. Siyakatai mawazo na mitizamo yako kuhusu hili ila kweli unaniangusha sana.
 
Kweli Le profeseri Muhongo umezingua,huvi kodi sio pesa ya umma?Benki kuu ilihoji juu ya kodi mwanasheria wenu akasema hamna kodi,leo hii unasema TRA wanaweza kudai kodi yao,watadai wapi wakati hela imeshatakatishwa na nyie mkiwa kwenye mgao huo....hawa watu wanatuona Watanzania hatuna akili kabisa..
 
Simwamini yeyote katika hawa, hata kama anasema ukweli. Taa yangu ni wahisani. Wahisani wamezuia fedha zao kwa sababu ya skendo hii, mpaka waone hatua zinachukuliwa. Usidanganywe!
 
Back
Top Bottom