Majibu ya Serikali (Wizara ya Nishati na Madini) kuhusu ripoti ya PAC juu ya Tegeta Escrow Account

'Tanesco' bhana, eti ndo wanarudisha umeme sasa. Sijui wamebana nini, simu zipo, radio zipo! Wanachekesha sana walivyo mataahira.
 
mbowe siku zote alikuwa haonekani lakini baada ya jana kujilidhisha kuwa jina lake halijatajwa ,leo kaja na mbwembwe zote....
 
Yaani huyu profesa sijamuelewa kabisa.

Habari za siku Mkuu? Baada ya ligi kusimama tumepotezana. Nashukuru tumekutana tena huku kwenye akaunti ya Tegeta ESCROW.

Maudhui ya hotuba ya jamaa ni mafupi tu kwamba fedha zilizokuwa ndani ya akunti ya ESCROW siyo za umma.
 
Kwa kweli kama anayoyasema Muhongo ni kweli ya kwamba hela ya ESCROW sio ya umma basi haya ni matusi kwa ofisi ya CAG na TAKUKURU kwa maana ya kuwa hizi ofisi zimetoa taarfia ya uongo. kwa maana hiyo zifumgwe. Na kama zimesema ukweli basi Muhogo afunguliwe mashitaka na afungwe.
 
Dah! ni hatari sana Watanzania mpaka leo bado tuanshindwa kutofautisha kati ya profesa na polopesa, mfano profesa Bere..gu na polopesa maji maref...u., Bongo hapa wengi ni mapolopesa sio maprofesa, ndo mana wanakuwa wezi na matapeli. Kisha bado kuna watu wanawatetea wezi hao hao, yaani hii nchi kama imerogwa. Ingekuwa amri yangu WEZI WOTE WA PESA ZA UMMA NA WALE WOTE WANAOWATETEA WEZI WANYONGWE HADHARANI.
 
Mm sina neno lakini ngoja tuone saa 11 hii ngoma nzito kumbe mkono alikuwa kaifanya tanesco "shamba la bibi"haki ya mungu nchi hii kila mtu mwizi hapa hakuna wa kumfunga paka kengele wooote wezi tu upepo upite tusonge mbele mm mwenyewe sasa niko ktk mchakato wa kusaka hizo fedha za escrow kumbe hazikuwa za serikali ngoja mtaona nitazinyaka tu.
 
Wakuu wasipojiuzuru ,ni kurudisha ile movement ya kukusanya sahihi ili kupiga kura ya vote of no confidence!!

Sioni dalili ya jamaa kusepa hapo.
Nilifikiri kuwa issue ni ufisadi!, kumbe issue na this time ni uwaziri mkuu?!, mkidhani itakuwa simple kama ile ya Richmond?!.

This time!, No way!.

Pasco.
 
Sijawahi kusikia mwizi akikubali kuwa yeye ni mwizi ni nadra sana kutoea, pia tujiulize ule muongozo wa yule mbunge wa CUF kuwa mbona serikali aikuombwa kutoa majibu wakati wa sakata la TOKOMEZA na RICHOMND ukilielewa hili ndio utajua kwa nini huyu mama alirudi nyumbani haraka baada ya NDUGAI kukubali mjadala wa wazi, MAKINDA ni miongoni mwa viongozi wachahe wanaoliumiza TAIFA


Escrow inatoa picha nzuri jinsi maadili kwenye uongozi nchi hii yalivyoshuka. Watu wamebeba hela kwenye mifuko ya rambo, mabox, lakini viongozi bila haya wanatetea, tena bungeni? Waziri anapata hela toka kwenye kampuni ambayo iko chini ya wizara anayoongoa lakini anasema hakuna tatizo!
 
Prof kawaambia kuwa kama yeye ni dalali basi udalali wake ni wa kupeleka umeme vijijini

Vijiji gani mbona hakutaja? Aache uongo wake hapa, vijana wametoa facts jana yeye kaishia kupiga kelele tu
 
Binafsi nilianza kuwa na wasiwasi na ripoti ya PAC hasa kitendo chao cha kutokutaja popote kodi ya Bilioni 38 iliyolipwa na VIP katika mauzo yake ya shares.
 
Huyu ni mwizi mkubwa alikuwa kaifanya tanesco shamba la bibi yaani ushauri tu bil 62 na bado anadai?mkono ww ni mse.........na utaona tu
 
Habari wakuu,
Kwa kua wote tunasubiri majibu ya Serikali kuhusu Escrow, Tutajuzana hapa kuhusu utetezi wa Serikali juu ya shutuma zilizotolewa na kamati ya bunge ya PAC jana iliyowasilishwa na Zitto Kabwe na Deo Fulikujombe ambaye yeye alisoma maazimio ya kamati.
=================

MUHONGO(UTETEZI WA SERIKALI)
Anaomba radhi kama jana kulikuwa na usumbufu wa umeme na anawaagiza mameneja wote wa TANESCO wasikate umeme.
Anatoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow, mengi yamesemwa na niwakati wa kuanza mjadala kujua ukweli, Shukraan kwa CAG, TAKUKURU kwa uchunguzi. Pia nawashukuru PAC, jana tulitulia kuwasikiliza PAC na leo tutulie tusikilize utetezi wangu

Miaka ya 90 tulikuwa tuna upungufu wa umeme kutokana na maji, 1994 serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa inamiliwa na VIP ya Tanzania iliyokuwa na 30% na Mechmar ya Malaysia 70%.

Kulingana na mkataba, majukumu ya IPTL yalikuwa kujenga, kumiliki na kuendesha hivyo utaifashaji utaiingiza serikali katika matatizo makubwa ikiwemo kushtakiwa kimataifa pia itafukuza wawekezaji binafsi. TANESCO na IPTL walisainiana mkataba wa miaka 20, hata hivyo uzalishaji haukuanza mara moja kutokana na mgogoro ulioibuka baina ya TANESCO na IPTL

Ilianza kuzalisha umeme 2002 hivyo mkataba ukaanza kuhasabiwa hapo, kutokana na mgogoro ikafunguliwa Escrow Account na escrow ilizungumziwa toka mkataba wa 1995.

2004 TANESCO ilifungua shauri kupinga tozo la capacity charge
Taarifa hio sio kweli kwani TANESCO haijawahi kufungua kesi yoyote dhidi ya standard charted kamailivyosemwa na PAC. Kesi hiyo ilifunguliwa na Standard charted na ilikuwa haihusu capacity charge. Hamna kokote mkataba kati ya standard charted na TANESCO.

Makinda ameingilia na kusema ripoti itatolewa baada ya wabunge kudai ripoti.

Muhongo anaendelea
Uwiano wa mtaji ni 70 kwa 30, na uamuzi haujabadilishwa na mahakama yoyote. 2004 kampuni ya Mkono and CO advocates iliishauri TANESCO iendelee kupinga capacity charge London. Hata hivyo, tanesco haikuishauri TANESCO kufungua kesi za TANZANIA wala mahakama ya kimataifa. Hadi 2013 jaji Utamwa anatoa hukumu ya mgogoro wa wanahisa wa IPTL kulikuwa hamna kesi yoyote kuhusu tozo ya IPTL.

UUZAJI WA HISA ZA VIP

Kutokana na kutokubalina Mechmar iliishauri VIP ifungue shauri. VIP ilifungua shauri Tanzania ikiomba IPTL ifilisiwe. Uamuzi ulitolewa kwa shauri la VIP. Chini ya Kimario, alpewa mfilisi wa mda kulinda mali za IPTL, kufanya uchunguzi ili mahakama iweze kutoa uamuzi. Uamuzi ulitoka IPTL iweke kwenye ufilisi kamili chini ya RITA. Hukumu ilipingwa mahakama ya rufaa ikianisha dosari katika uamuzi wa mahakama kuu na Standard charted Hong Kong. Mahakama ya rufaa ilikubaliana na hoja hiyo na ilipelekwa tena kwa mfilisi wa muda kukusanya madeni, kusuluhisha mogogoro na kuendesha mitambo ya IPTL kwa niaba ya IPTL.

Serikali haiwajibiki kuingilia hisa za makampuni binafsi, mauzo ya hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu endapo yatatambuliwa na BRELA. Uhamishaji wa hisa 7 ulisajiliwa hapa nchi. Kamati katika uthibitisho huo inakubali hisa za Mechmarr unamilikiwa na PAP

Hiza saba za IPTL unatambuliwa pia na Standard Charted, Kama PAP haimiliki asilimia sabini kwanini wana makubaliano na standard charted ya Uingereza.

Ilifilisiwa Malasia na sio Tanzania, madai ya standard charted dhidi ya TANESCO ni kwa sababu IPTL waliweka dhamana mtambo wa kuzalishia umeme, Lakini benki ya Hong Kong ilikosa sifa ya kufungua shauri Tanzania hivyo ilifungulia Uingereza

VIP chini ya usuluhishi wa RITA iliuza hisa zake PAP kwa dola milioni 70 na ndivyo ilivyomaliza mgogoro wa IPTL. Mimi sio dalali wa hii biashara bali ni dalali wa(anasema mambo mazuri aliyoyafanya)
Makinda amekuwa mkali kidogo kwa Muhongo asome taarifa na asiseme ambayo hayamo.

ESCROW ACCOUNT
TANESCO kwa ushauri wa mkono walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme na makadirio ya mtaji walitoa notisi(invoice disputes notice) ya kupinga usahihi wa malipo. Alietoa ushauri ni kampuni ya Mkono, 2006 serikali ulisaini mkataba wa kufungua account ya Escrow.

MMILIKI WA FEDHA YA ESCROW
Account ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa na TANESCO. PAC walitoa mapendekezo kuwa imethibitisha kuwa mchakato wa kutoa pesa Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kutakatishwa na benki mbili nchi

TAHADHARI ZILIZOCHUKULIWA
Serikali ilichukua kinga kutoka IPTL, kwa mujibu wa kinga IPTL itawajibika yakitokea madai yoyote na ilipitiwa na mwanasheria mkuu wa serikali. (Yoyote anaedai chochote aende IPTL)

PAC wameeleza serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha juu ya madai mapya kama yangejitokeza kitu ambacho sio kweli.

DHANA YA MADAI YA BILIONI 321
Madai kwamba IPTL inaidai IPTL 321 Bilioni, bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG hakionyeshi madai haya.

Madai yaliyowasilishwa na mufilisi, yalitakiwa kuhakikiwa lakini hayakuhakikiwa na hayakuwa na uhalali wowote.

Kamati ya PAC, wamesema yana uhalali japo uhalali wake unategemea maamuzi.

TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Deni la TANESCO kama capacity charge lilikuwa $370milioni ambazo ni pungufu ya $90 milioni ya madai ya IPTL. Yalifanyika hoteli ya Kunduchi na majina ya waliokuwepo anawataja.

Hizi takwimu zinaonyesha hakuna fedha yetu pale tunayodai bali tunadaiwa na IPTL. Hamna fedha ya umma popote bali tunadaiwa na makampuni ya uzalishaji umeme(anataja makampuni na madeni wanayodai).

Madai yoyote yaliyotokea nje ya nchi laima yasajiliwa nchini, shauri la London haliusiani na fedha za IPTL.

Madai dhidi ya IPTL ikiwemo VAT, serikali ilitaka kinga.

Gharama za mawakili za Mkono adv, hadi hukumu inatoka 2013. TANESCO na serikali zililipa mawakili bilioni 62.9 na bado mawakili hawa wanadai TANESCO $ milioni 4.5 na walipendekeza wapewe kazi nyingine ya kwenda kupinga huku lakini bodi ilikataa kuendelea na hio kazi. Tunajua fika tumepata hasara gani kupitia kampuni ya Mkono.

Kumalizika kwa mgororo na IPTL tumeokoa bilioni 95 za uwakili. TANESCO ilikua na nafasi finyu mno ya kushinda kesi ya London kulingana na ushauri wa mawakili ushauri unaogongana.


2013 kwa mujibu wa RITA, IPTL ilikuwa inaidai TANESCO $224.3 milioni, taarifa ya CAG inasema fedha za Escrow ni za umma.

FEDHA SIO ZA UMMA
TANESCO ilisimamisha malipo ya Escrow na ya IPTL kuanzia mwaka 2010 japo iliendelea kupata huduma kadri ilivyohitaji.
Hakuna fedha ya umma Escrow

Account ya Escrow iilikuwa na 182 na bado kuna upungufu wa 122 katika deni la IPTL.

Kamati haikupitia majukumu ya wazira, Mikutano ya bodi wakurugenzi TANESCO, PAC inasema ilifanya mikutano miwili mfuulizo hivyo kutia shaka. Si sahihi bodi ya TANESCO ilikuwa na njama.

Hoja ya mwanasheria wa TANESCO kazi, Taarifa ya PAC inasema mwanasheria iliagizwa kwenda Malashia na aliporudi kuwasilisha ripoti ya due deligence aliachishwa kazi.

Mwanasheria wa TANESCO aliomba kwenda Malasia kwa madai kuwa alipewa na mwanasheria mkuu wa serikali kitu ambacho ni uongo na aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa kutoa taarifa kwa mkurugenzi mtendaji.

Alisema anaacha kazi kwa hiari yake mwenyewe kufanya shughuli zake binafsi. Hivyo bodi haikuwahi kumfukuza huyo mfanyakazi.

Hii kesi mimi nilielezwa na bahati mbaya bodi haikufata ushauri wangu wa kumshitaki muhusika.

WABUNGE WANADAI NAKALA YA RIPOTI KWA NGUVU NA BAADHI KUMUITA MWIZI

Anamalizia hapa kwa nukuu(anazinukuu nukuu kwa kiingereza na tafsiri zake), Spika anamwambia amalizie.

Spika amesimama tena kupoza hali ya hewa, Anamlazimisha waziri amalizie.

Waziri anawasilisha hoja na kumaliza.

MATANGAZO YA KAZI


Shughuli za bunge zimesitishwa mpaka saa kumi na moja.

====================================

Soma hapa kujua Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Alhamisi, Tarehe 27 Novemba, 2014 (click)
=============================

Upuuuzi mtupu....ni kaburi jingine kwa ccm
 
Back
Top Bottom