Tatizo hakuna mtu wa mbadala mwakani kwa hiyo atapeta na kupata kura za wadanganyika tena!
Kwani yule Shibuda kapotelea wapi!? Au Mtandao wa mafisadi umeshamnunua ili kumsafishia njia mtu wao!? Maana amekuwa kimya kwa kipindi sasa na huu ndiyo wakati wa yeye kuanza kusikika zaidi kwa Watanzania.
Good job Kikwete, usiwaogope hao Makafir. Tupo nyuma yako kwa nguvu zote.
Kwa rais aliye makini na ambaye anapata taarifa zote kutoka kwenye vyombo vyake vya usalama hata anapokuwa nje ya nchi, hakutakiwa kuomba muda wa kujiandaa ili kujibu hoja za akina Qure's. Alitakiwa awe na majibu hapo hapo maana tatizo ni la muda mrefu na analijua.
Sasa anataka kutwambia kwamba anaenda kushauriana na akina Kingunge na Makamba ndiyo atoe majibu, au anaenda kushauriana na Sophia Simba? Hapa ipo kazi, na kwavyovyote vile atatoa majibu yake kwenye salamu za mwaka mpya.
Namshauri Kikwete asigombee tena ili apate muda wa kuendelea na utalii, (maana huyu ni mtalii namba moja wa kitanzania) haiwezekani rais anatumia muda mwingi nje ya nchi kuliko anavyokaa ndani ya nchi yake.
Good job Kikwete, usiwaogope hao Makafir. Tupo nyuma yako kwa nguvu zote.
Bravo JK for good implementation of 2005 CCM MANIFESTO
NaaaamMtanzania yoyote anayesubiri majibu ya Kikwete kwa kudhani kwamba yatatoa mwanga kuhusiana na uongozi wake dhaifu katika kila nyanja ikiwemo kushindwa kupambana na mafisadi, kushindwa kuipitia mikataba ya uchimbaji wa madini na pia kushindwa kutimiza ahadi zake za "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" na "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" anapoteza muda wake bure.
Kikwete amepata nafasi chungu nzima za kufanya maamuzi ambayo yangerudisha imani ya Watanzania kwa uongozi wake kama Rais, lakini nafasi zote hizi amekuwa akijikanyagakanyaga na kujichanganya na kuzidi kutukatisha tamaa Watanzania.
Kwa hiyo siku atakapoamua kuongea rasmi ili kujibu tuhuma za uongozi wake dhaifu hakutakuwa na jipya lolote la kutupa matumaini Watanzania bali ni kujikanyagakanyaga kama ambavyo ilivyo kawaida yake na kwa mara nyingine tena kutukatisha tamaa mamilioni ya Watanzania. Tunahitaji Rais mpya 2010, Kikwete kazi imemshinda na hili siyo siri kabisa.