Majibu ya Kikwete ya Tuhuma za Uongozi Dhaifu Yasubiriwa kwa Hamu!

In politics when u say nitajibu it means I wont jibu or ndio nimeshajibu hivyo - its a political tactic of buying time!
 
In politics when u say nitajibu it means I wont jibu or ndio nimeshajibu hivyo - its a political tactic of buying time!

Tatizo hakuna mtu wa mbadala mwakani kwa hiyo atapeta na kupata kura za wadanganyika tena!
 
Tatizo hakuna mtu wa mbadala mwakani kwa hiyo atapeta na kupata kura za wadanganyika tena!

Kwani yule Shibuda kapotelea wapi!? Au Mtandao wa mafisadi umeshamnunua ili kumsafishia njia mtu wao!? Maana amekuwa kimya kwa kipindi sasa na huu ndiyo wakati wa yeye kuanza kusikika zaidi kwa Watanzania.
 
Shibuda yupo lakini itakuwa ngumu sana kupitishwa na CCM dhidi ya JK! Akihamia upinzani CCM watafanya kila njia kuanika mabaya yake tangu alipokuwa chekechea, kisha mtamwona hafai kuliko kiumbe chochote duniani! Tanzania ukitaka kuwa "msafi" bakia CCM, usiwaseme wakubwa wanapomega mapande makubwa ya keki ya taifa, wewe okota vipande vidogo vidogo vinavyodondoka na kuvitafuna!
 
Nadhani kama mheshmiwa anataka kujibu tuhuma, basi asiwajibu watoa hoja katika kongamano, bali ajibu hoja kwa kina, kama zilivyotolewa. Maana katika kongamano wananchi wamezungumza hoja zenye ushahidi. Ajaribu kupangua hoja zile kwa hoja na asiropoke kama katibu mkuu wake alivyoropoka na kuwaita watu wazima wehu! Vinginevyo, atakuwa amejipigilia msumari wa mwisho katika kutofikirika ndani ya chama na serikali yake!
 
Kwa rais aliye makini na ambaye anapata taarifa zote kutoka kwenye vyombo vyake vya usalama hata anapokuwa nje ya nchi, hakutakiwa kuomba muda wa kujiandaa ili kujibu hoja za akina Qure's. Alitakiwa awe na majibu hapo hapo maana tatizo ni la muda mrefu na analijua.

Sasa anataka kutwambia kwamba anaenda kushauriana na akina Kingunge na Makamba ndiyo atoe majibu, au anaenda kushauriana na Sophia Simba? Hapa ipo kazi, na kwavyovyote vile atatoa majibu yake kwenye salamu za mwaka mpya.

Namshauri Kikwete asigombee tena ili apate muda wa kuendelea na utalii, (maana huyu ni mtalii namba moja wa kitanzania) haiwezekani rais anatumia muda mwingi nje ya nchi kuliko anavyokaa ndani ya nchi yake.
 
Huyo ndo tulimwamini kwa zaidi ya asilimia 70% ya kura. Natumai hayo anayoyafanya ndo tulotegemea, la! Kelele zingelikuwa zimemng'oa kutoka pale Magogoni.
Ninaisubiria Tanzania wa watanzania ambao hawatakuwa radhi kuishi kwa porojo na propaganda. Hakika wakati waja ambao suala litakalokuwa ni la muhimu kati ya watanzania ni nini kuli wao amefanya na siyo porojo gani kaongea kwenye press confrence.
 
Good job Kikwete, usiwaogope hao Makafir. Tupo nyuma yako kwa nguvu zote.

Unahitaji moyo mzito sana kumtetea Rais Kikwete, kwani ni wazi ameshindwa kuonesha viwango na kasi katika utendaji wake.
 
Mr president tunakuomba ikamilishe ahadi yako hii ya kujibu tuhuma zilizotolewa ukiwa Cuba ,na isije ikawa kauli za mzee yousuf makamba kama alivyofanya miezi michache iliyopita ndani ya mwaka huu ,wakati ule Mama Anna Kilango kwa kukerwa kwake na baadhi ya Mafisadi ndani ya chama (CCM )na kumbidi aondowe uvivi na kuweka wazi hali hiyo,haikuchukuwa muda Mzee Yousuf Makamba akatowa kauli katika vyombo vya habari na magazeti kuwa watamjibu mama Kilango ,wananchi tukasubiri mpaka hivi sasa naleta maoni hayo inakaribia mwaka tena, Mzee yousufu hajamjibu mama Kilango na wanachi tumepigwa na butwaa huku tukijadiliana hivi huyu mzee Makamba ni mtu wa kuwekwa manani na kuaminika? au ni miongoni mwa maporojo yake ya kuchunga madaraka yeke ?pia tunajiuliza baadhi yetu ,au zile kauli za sofia simba zidi ya mama Kilango ndio alitumwa Indirect kumjibu mama Kilango mtetezi wa wananchi na nchi yake? Tunakusubiri Mheshimiwa Rais wetu .
 
Mtanzania yoyote anayesubiri majibu ya Kikwete kwa kudhani kwamba yatatoa mwanga kuhusiana na uongozi wake dhaifu katika kila nyanja ikiwemo kushindwa kupambana na mafisadi, kushindwa kuipitia mikataba ya uchimbaji wa madini na pia kushindwa kutimiza ahadi zake za "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" na "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" anapoteza muda wake bure.

Kikwete amepata nafasi chungu nzima za kufanya maamuzi ambayo yangerudisha imani ya Watanzania kwa uongozi wake kama Rais, lakini nafasi zote hizi amekuwa akijikanyagakanyaga na kujichanganya na kuzidi kutukatisha tamaa Watanzania.

Kwa hiyo siku atakapoamua kuongea rasmi ili kujibu tuhuma za uongozi wake dhaifu hakutakuwa na jipya lolote la kutupa matumaini Watanzania bali ni kujikanyagakanyaga kama ambavyo ilivyo kawaida yake na kwa mara nyingine tena kutukatisha tamaa mamilioni ya Watanzania. Tunahitaji Rais mpya 2010, Kikwete kazi imemshinda na hili siyo siri kabisa.
Naaaam
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom