Majibu ya IKULU dhidi ya Tanzania Daima kuhusu ndege ya Rais na safari ya Davos

Sijaona mahali walipokanusha hizo million 300, wamesema tu hawajui" Tanzania Daima" imepata wapi hizo habari.
Hawajsema ni kiasi gani kitatumika, au kimetengewa hii trip.
Je hizi Mil.300 ni kweli??
Ndege itakuja Lini??
 
Asanteni mmekosoa kinacho stahili kukosoa ila tukiwa wakweli na bila unafiki mchanganuo wenu huo una vipengele vingi vinavyostahili kukosolewa pia kuna vingi vinavyotia shaka mfano.

Bado sijaona faida ya moja kwa moja ya kukutana na watu mashuhuri kama kina Gates,shah,zoellick,ruud nk,

(2)mradi unaodaiwa kuibuliwa na wef bado haujaonyesha uwezo wala uhakika wa kuweza kufikia malengo yaliyoainishwa hivyo si ajabu kukuta mradi huo ukididimiza maendeleo badala ya kusukuma mbele maendeleo

(3)kuhusu Davos sweden na davos swiss sioni kama ni issue kwani yaweza kuwa makosa ya kiuandishi

(4)nilitaraji kupata ukweli wa gharama halisi ya safari hiyo ukiacha hiyo uliyodai kuwa ya kizushi iliyoonyeshwa na tanzania daima,kuhusu qatar au qatal pia nadhani ungeweza tu kusahihisha mwenyewe nakupata kile mwandishi alichotarajia kuandika.

Mwisho napenda kuwaomba wa tz hasa viongozi kuwa na tabia ya kupinga uongo kwa kuelezea ukweli ni upi ili mtu wa kawaida aweze kupambanua kati ya uongo na ukweli kwani siku zote uongo bila ukweli hubaki kuwa uongo. Pia safari hii nimuombe Mh Jk kuja na mipango kamili inayotekelezeka na itakayo tekelezwa badala ya picha na takwimu zilizokaa kiubabaishaji.
 
Ok, 1: kama hatatumia milioni 300 atatumia milioni mia ngapi?
2: kwa kuwa unarekebisha sentensi i.e QATAL kuwa Qatar, je nini maana ya kuonana na WAKUBWA ?
3: huoni kwamba miradi ya wafadhali haileti maendeleo ya kweli ? Mradi wa Mbarali uliendeshwa kwa tija sana na JICA , ukafa
baada ya wao kuondoka, sasa mnaleta SAGGOT, matokeo si yatakua yaleyale?
4: Safari ya JK haitakua ya siku nne Uswisi. itakua ya siku ngapi Uswisi?
5: Kwa nini ameondoka ameacha hali ya mgomo wa waganga ikiwa tete?

Swali la nyongeza: CT Scan Muhimbili inatengenezwa lini?

thank you for this very useful post.
 
Nadhani kupata na kuripoti taarifa sahihi inatusaidia sisi wananchi kuchambua mchele na chuya.sasa gazeti tunaloliamini likitupatia taarifa za kimagumashi litatuchanganya na hatimaye kulidharau na kuacha kusoma habari zake.
 
Ok, 1: kama hatatumia milioni 300 atatumia milioni mia ngapi?
2: kwa kuwa unarekebisha sentensi i.e QATAL kuwa Qatar, je nini maana ya kuonana na WAKUBWA ?
3: huoni kwamba miradi ya wafadhali haileti maendeleo ya kweli ? Mradi wa Mbarali uliendeshwa kwa tija sana na JICA , ukafa
baada ya wao kuondoka, sasa mnaleta SAGGOT, matokeo si yatakua yaleyale?
4: Safari ya JK haitakua ya siku nne Uswisi. itakua ya siku ngapi Uswisi?
5: Kwa nini ameondoka ameacha hali ya mgomo wa waganga ikiwa tete?

Swali la nyongeza: CT Scan Muhimbili inatengenezwa lini?

naona mkuu kaedit habari na si kukanusha.
 
Kuandika habari ya uongo nao ni ufisadi,kwani pesa nyingi zimetumika kutunga uongo badala yake zingepelekwa hata kwenye ujenzi wa ofisi zetu pale makao makuu kinondoni.
 
Waandishi kuanzia magazeti mpaka Ikulu wote mafafa matupu. Kama Salva kafanya makosa ya syntax, spelling na grammar katika taarifa ya sentensi moja kuwaandaa watu na kutangazwa kwa Katibu Mkuu kiongozi mpya, siwezi kushangaa "Tanzania Daima" wakikosea mji na nchi multiple times. Wanawapata wapi hawa waandishi? Hamna wahariri?

Kutoka Ikulu tumepata maneno mengi lakini kitu kimoja muhimu hawajakanusha kwa data. JK na msafara wake wanatumia kiasi gani?
 
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu bado ina matatizo. Hawaonekani kabisa kuelewa kazi yao. Hii taarifa waliyotoa inaonekana kujaa 'povu' na kukurupuka. Kama gazeti linatoa taarifa isiyo sahihi kinachotakiwa ni kwa kurugenzi hii kueleza ukweli ni upi na sio kuanzisha zogo au confrontation!

Pili, nadhani siko peke yangu kusema kuwa hili sio kanusho ya kile kilichoandikwa na Tanzania daima bali ni taarifa kamili juu ya safari ya Rais Kikwete huko Davos Uswisi na Addis Ababa! Na hapa najiuliza kama Tanzania Daima haikundika ilichoandika kurugenzi ingeeleza wananchi ni kitu gani kilichompeleka rais Davos?

Hapa kuna massive failure kutoka kwa hii kurugenzi, badala ya kuwa pro-active wamekuwa ni re-active. Kila siku wanaonekana kujibu mapigo badala ya kufanya kazi za mawasiliano kati ya Ikulu na wananchi. Mikakati mibovu.

Pia, sikubaliani na maelezo kuwa kwenda Davos kwa rais Kikwete kunampa yeye rais fursa kukutana na watu mashuhuri! Ili iwaje akishakutana na hao watu mashuhuri? Bill Gates na Melinda si hivi majuzi tu walikuwa magogoni? Na kama lengo ni kukutana na watu mashuhuri lipi bora; kuwaalika magogoni na kufanya nao mazungumzo au kwenda huko Davos? Kwa maoni yangu MKAPA angefaa kuhudhuria huu mkutano kuliko rais. Kwanza ukiangalia list ya viongozi wanaohudhuria wengi wao ama ni wastaafu au mawaziri wadogo. viongozi wakubwa ni wachache sana na sina hakika wameenda hapo kujadili kilimo huko Rufiji! sidhani!

Mwisho, naomba niwapongeze Tanzania Daima kwa 'kumtoa nyoka pangoni'. Kama sio uchokonozi wenu Ikulu isingetufahamisha kuwa rais Kikwete atashiriki mjadala mkubwa kuhusu Kilimo kusini mwa Tanzania!
 
Tanzania Daima si waandishi makanjanja hata mji au nchi walikuwa hawajui ni upi na ipi, na wahariri nao basi hata hawajui kama inaitwa Qatar na si "Qatal"? hata kompyuta yangu ya nyumbani nikiandika "Qatal" inaniwekea mstari mwekundu chini kuonesha kuwa nimekosea. Nna uhakika hata wamiliki wake ni makanjanja kwani wangekuwa na umakini kidogo wasingeruhusu uozo kama huo uandikwe gazetini.

na habari ya zile suti wangekanusha namna hii ndo wangekosea kweli kweli. Kumbe afadhali wanavyotoa taarifa ya sentensi nne.
 
Davous, nchini Sweden????!!!!. Sweden???!!!! Davous???!!!! I never heard about this City. I know Davos Switzerland.
 
me nlishangaa kuona imeandikwakwenye TOP PAGE eti Davos iko sweden wakati iko switzerland=uswis.pia eti shirika la Qatal badala ya Qatar,waziri NDUNDU badala ya Nundu,huu ni ubabaishaji,inabidi jamaa waombe radhi
 
hivi kuna marais wengine hasa kutoka africa watahudhuri?kwa nini asingehudhuria waziri ili huyo kikwete atatue matatizo ya madaktari???kweli kufikiri kutumia kalio moja ni noma!
 
Tanzania Daima si waandishi makanjanja hata mji au nchi walikuwa hawajui ni upi na ipi, na wahariri nao basi hata hawajui kama inaitwa Qatar na si "Qatal"? hata kompyuta yangu ya nyumbani nikiandika "Qatal" inaniwekea mstari mwekundu chini kuonesha kuwa nimekosea. Nna uhakika hata wamiliki wake ni makanjanja kwani wangekuwa na umakini kidogo wasingeruhusu uozo kama huo uandikwe gazetini.
Gazeti la Tanzania Daima huchapwa na Mwananchi Communications.
 
Davous, nchini Sweden????!!!!. Sweden???!!!! Davous???!!!! I never heard about this City. I know Davos Switzerland.

the guys are empty stomarch, and u know the impact of being hungry,unaweza kuropoka lolote ilimradi mdomo ni wako.
 
Waandishi kuanzia magazeti mpaka Ikulu wote mafafa matupu.

Maneno mengi lakini kitu kimoja muhimu hawajakanusha kwa data. JK na msafara wake wanatumia kiasi gani?

fanya hivi
if 3days = 300m
8days = ?
 
hivi kuna marais wengine hasa kutoka africa watahudhuri?kwa nini asingehudhuria waziri ili huyo kikwete atatue matatizo ya madaktari???kweli kufikiri kutumia kalio moja ni noma!

Na wewe unajiita great thinker hata aibu huna.
 
fanya hivi
if 3days = 300m
8days = ?

Nani kasema 3 days = 300m? Hao wanaosema rais kapanda ndege ya nchi ya Qatal kwenda Daveous Sweden?

Daang, utafikiri wanafanya makusudi eenh, maana hata kukosea mara moja au mbili, mara tatu? Hivi huyu muandishi kashawahi kuangalia ramani ya dunia?

Bottom line, Ikulu haiwezi kukataa figures bila kutoa figures.
 
hivi kuna marais wengine hasa kutoka africa watahudhuri?kwa nini asingehudhuria waziri ili huyo kikwete atatue matatizo ya madaktari???kweli kufikiri kutumia kalio moja ni noma!

anaenda kudiscuss na WAKUBWA kuhusu kilimo hapo Rufiji.
Kweli? Unaenda kuongea kilimo na wakubwa? Kilimo hiki cha powertiller?
 
Back
Top Bottom