Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Reverend,
Let me be clear as I can , I still stand by everything I said and I am not going to apologize as you have requested. In fact , you are the one who should apologize for distorting my position. By the way, can you please explain to me what u' meant by :
Rufiji,
Nilitoa mfano kuwa katika BOT kufanya biashara yake kwa niaba ya Serikali, 75% ya mapato inarudi Serikalini na 25% inabakia kuwa ni yao kwa kujiendesha (let say my breakdown of percentage is accurate).
Nimeuliza kwa nini kama wao wanatumia hiyo 25% yao wanavyotaka kinatuumia nini katika maana kubwa na pana na sivyo ilivyopokelewa.
Tanzania tunadai kuwa kila kitu kilikuwa kinaingiliwa na Serikali au kudhibitiwa na Serikali (big brother) sasa kama tunataka kuwa na jamii na taasisi zinazojiendesha kwa uhuru, na hicho ndio kilio chetu kingine kwa nini Wanasiasa wanaingilia uendeshaji wa taasisi na mashirika, iweje nasi tung'ang'anie kuwa hilo fungu la BOT kujiamulia wajifanyie wanalotaka tutake nalo lidhibitiwe?
Kama unakumbuka, nilikuuliza, weye unanifahamu vizuri na ninachoandia katikati ya mstari, lakini mkanirukia kiringe na kunitusi eti najidai jiniasi!
NItaendela kukujibu hivi:
NIliuliza, je kuna mtu kafanya tathmini ya gharama za ujenzi Tanzania? NIkaendelea kuuliza kama BOT ndio wadhibiti na walinda uchumi, iweje kuwe na uholela wa gharama za ujenzi mpaka leo hii?
Sasa kama nilitamka kuwa BOT wajiamulie wanalotaka halafu nikahoji suala la uholela wa gharama za ujenzi, huoni ninachoainisha kuwa kuna Tatizo kubwa sana la kiutendaji Tanzania na hata ubovu BOT ambayo ndiyo inapaswa kuwalinda Watanzania? Tena nikaongeza kwa kuuliza, kama BOT waliafiki kununua kiwanja au kulipa gharama hizo za ujenzi, ina maana kuwa Tanzania katika sekta ya nyumba, ardhi na ujenzi, gharma hizo ni halali na hazihitaji kuangaliwa?
NItaendela kufafanua kauli zangu.
Nikaendelea na kuhoji, ikiwa BOT leo hii wanajukumu la kuratibu shughuli za ujenzi wa nyumba boa na nafuu, Tanzania, je walitumia kwa kiasi gani ujuzi wa wajibu wao katika kujijengea nyumba hizi? Zaidi nikauliza, je nyumba za Wafanyakazi wengine ziwe pale Dar, Arusha, Mwanza, Mbeya au Zanzibar, nazo zinakarabatiwa kama zilivyofanyiwa hizi nyumba?
Sasa kwa kuwa hukuelewa nilichokuwa na lenga, basi ilikuwa ni rahisi kwako kuainisha kuwa nilichosema kuwa nahalalisha matumizi ya kodi ya wananchi. JokaKuu akaamua kuangalia Act na Charter ya BOT akakutakuwa Mwenyekiti wa Bodi ni Gavana na hao manaibu Gavana nao wako kwenye bodi, hivyo wao wana sauti katika upigaji kura.
Je ilikuwa ni lazima niandike kuwa hili lian walakini? Ni kila kitu watu warahisishiwe? Ndio maana nikaghadhibika na kuuliza je kuna mwenye kuchukua muda kusoma na kuangalia facts nba si kutumia emotions?
Sasa kwa nyongeza ya maswali yangu matatu ya awali ambayo umeamua kuniita mnafiki, nina mengine ya ziada, kwa BOT na kwa faida ya wengine. Ni uamuzi wako na msomaji yeyote kama utaamua kuendelea kuamini kuwa ama nimeamua kubadilika au sikueleweka hapo awali na kupokelewa kwa utata kwa kuwa sikujibu hoja kwa hisia bali kwa kupima hali halisi ya Tanzania.
Maswali yangu yanayofuatia ni hayal
Je nyumba hizi zimejengwa kuwa kutumia malighafi na Rasilimali ambazo zinazalishwa Tanzania? Kama sivyo, ni kwa nini BOT ambayo inatakiwa kuchochea uzalishaji wa mali na kukuza uchumi wetu ilikubali mkandarasi alieagiza mbao kutoka Malaysia, huku tuna mbao nyingi kule Mufindi? Je udongo ulaya, misumari, fito, madirisha, samani, nyaya na hata udongo vilitoka nje ya nchi na hivyo kuongeza gharama za ujenzi?
Je Benki Kuu pamoja na kuwa hizi pesa zilitengwa awali, je kulikuwa na ulazima wa kuingia gharama na kuzijenga nyumba hizi wakati huu ambao Uchumi si wa Tanzania tuu bali wa Dunia ni mbaya na hivyo matumizi haya yalifanyiwa maamuzi na kuidhinishwa bila kutumia busara? Je Ndulu na wenzake walikuwa wanakaa wapi kabla ya kuwa Gavana wa Benki?
Je, Serikali na Mkaguzi Mkuu walikuwa wapi kuhoji matumizi haya? Nyumba hizi zimejengwa kwa Bajeti ya BOT ya 2007-2008/2009. je hakuna hata mtu mmoja ambaye alipitia mahesabu ya BOT hasa Wizara ya Fedha na kuwauliza BOT mantiki ya wao kutumia fedha nyingi kiasi hicho hata kama kiko ndani ya uwezo wa wa kutumia wakati huu ambapo BOT imeshakumbwa na kashfa nyingi za uhujumu na ufujaji mali?
La mwisho, ni mfumo wa BOT wa kujiendesha na maamuzi yake. Ikiwa Bodi na Menejimenti ya BOT viliamua kutokutumia busara katika matumizi haya, hata kutumia vigezo vya kiuchumi kama Taaluma na hasa kulinda mfumuko wa Bei na thamani ya sarafu yetu, je leo hii kama Wangetumia robo ya fedha hizi, kujijengea nyumab hizi, kungeleta mwamko ulioko leo hii wa kulalamika? Hapa nikiwa na maana ya kusema ikiwa Ndulu, Reli, na wenzao wawili wana kura nne ndani ya Bodi na wao ndio wakubwa wa Bodi, Serikali haioni kuwa kuna makosa makubwa kuwa maamuzi makubwa yaliyotuletea EPA na Minara ya BOT yalifanywa katika mazingira haya haya ambayo yanatokana na mfumo mbovu wa kiutawala?
Nilipouliza iweje CCM wajinunulie magari 200, kuna mtu akanijibu BOT ni mali ya umma, na CCM ni Chama cha Kisiasa. Lakini CCM nayo si inategemea Ruzuku ambayo ni kodi yetu na zaidi ni kuwa CCM imekuwa ikijiendesha na kutumia kodi zetu hata bila idhini yetu?
Sasa leo iweje tuone la BOT kuwa ni kubwa zaidi an tukasirike kuwa hizi ni kodi zetu, ilhali CCM wanadai kuwa Serikali ni yao na wanatumia mamlaka na dola ya Jamhuri ya Tanzania kwa Manufaa yao binafsi na si kwa manufaa ya Taifa?
I hope mlioko Tanzania ambao mtapata nafasi ya kuongea na Ndulu, Mkulo au kiongozi yyote hata kama ni Pinda na Kikwete, mtapata nafasi ya kuwauliza ninachouliza hapa na kuonyesha udhaifu na ubovu wa mfumo wetu wa uongozi na kukosekana kwa busara na hata soni kwa waliochaguliwa na kuteuliwa kulitumikia Taifa letu (kama Taifa na Serikali ni bado zetu!)!