Majibu kwa Mdau aliyeuliza tofauti ya Toyota Harrier na Rav 4 Old Models

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
May 17, 2018
358
670
Tofauti ya Harrier na Rav 4 Old Model

1. Uundwaji na Moboresho
Harrier iliundwa baadae miaka ya 1998 ikadumu mpaka 2002 wakati Rav 4 iliundwa miaka ya 1995 ikadumu mpaka 1999. Hivyo Harrier ilifanyiwa maboresho kwenye upande wa luxury haswa kwenye viti kua na mfumo wa umeme na uchaguzi wa injini. pia Harrier ilipata kua na screen ya kisasa unayoweza kuwekea kifaa flani ikaonesha video pamoja na sehem za kupumzishia mikono huku upana na urefu wa bodi vikiongezwa kuliko Rav 4.

2. Utulivu barabarani
Harrier ni nzito zaidi kuliko Rav 4 hivyo kuifanya itulie zaidi barabarani katika barabara zote yaani ya vumbi pamoja na lami.

3. Injini
Injini ya Rav 4 ni 3S ikiwa na Cc 2000 injini hii inapatikana pia kwenye Noah Old, wakati Harrier ilikuja na aina 3 tofauti. 1MZ ikiwa na Cc 3000, 2AZ ikiwa na Cc 2400, 5S ikiwa na Cc 2200. hivyo utapata kuchagua injini kulingana na matumizi.

4. Matumizi ya mafuta
Rav 4 inaweza kwenda mpaka kilomita 10 kwa lita, Wakati Harrier ina injini ya kwenda hadi kilomita 13 kwa lita hiyo ya 2AZ sbb ni wepesi wa body wakati injini ni kubwa, na teknolojia ya Vvti kwa injini hiyo.

5. Mafundi na Vifaa
Kwa ujumla gharama za uendeshaji kwenye ufundi na vifaa vinakaribiana sana kwa gari hizi. Mfano bei ya shock up ya Harrier ni 90,000 wakati ya Rav 4 ni 80,000.

6. Usalama
Rav 4 zilinyimwa funguo ya kubonyeza kulock au unlock milango, wakati harrier zilikuja na hii option. Pia Harrier zilikuja na Airbag 2 wakati Rav 4 ilikuja na Aibag moja isipokua baadhi za mwaka 1998-1999

7. 2WD na 4WD
Rav 4 haikupi option ya 2WD wakati Harrier unaweza kuchagua zenye 4WD au 2WD.

8. Gharama
Kuagiza Harrier yenye injini ndogo kwa sasa kunagharim kati ya 18m-19m wakati Rav 4 ni 17m- 18m

9. Maoni
Kwa kua gari hizi 2 zinakaaribiana bei na gharama za maendesho hazipishani sana, vizuri muhusika achague gari iliyofanyiwa maboresho yaani Toyota Harrier.

images (1).jpeg
images (2).jpeg
 
Ni wapi inauzwa Shock up ya Harrier 90k?
 
Back
Top Bottom