Mbimbinho
JF-Expert Member
- Aug 1, 2009
- 8,317
- 7,738
Kwanza kabisa nianze kwa kusema Shikamooni nikiamini wengi wa member ni watu wazima na wenye heshima na familia zao. Mimi bado ni kijana wa miaka 21 na nipo chuo kikuu mwaka wa pili. Nisirefushe sana maelezo, kisa changu ni hiki,
Miaka kadhaa iliyopita nilipokuwa sekondari nilikuwa na msichana ambaye tulipishana kidato kimoja, na ndiye alikuwa msichana wangu wa kwanza, nami nilikuwa wake wa kwanza, kwa maana kwamba alikuwa bado bikira.
Nafikiri wengi kama haijawatokea basi mmesikia jinsi mpenzi wa kwanza anavyokuingia moyoni, labda kwa sababu ya ugeni wa fani. Nilitokea kumpenda sana yule binti na nikawa sisikii wala sioni kwake. Tatizo likaja pale alipogundua kuwa nampenda sana, basi akaanza kuniletea pozi nyingi zisizo na mpango. Mara ataibuka tu na kusema, nafikiri tuachane, kwa sababu kama, anataka asome sana, mara hatuwezi changanya mapenzi na elimu, mara mimi ni kiongozi wa dini hapa shuleni hivyo natakiwa kuwa mfano au kuna mtu anampenda, na sababu zisizoeleweka, mimi nikawa naona kuwa kuna kaukweli ndani yake, lakini ilikuwa ngumu kukubali kwa kuwa tayari alikuwa ndani ya moyo wangu, na ingawa nilikuwa mwanafunzi niliweka nadhiri kuwa sitakuja mwacha.(Tuliishi vile bila kukutana kimwili hadi siku moja akaniuliza kama nilikuwa kamili, nikamjibu kuwa wakati wake ukifika atajua.) Basi nikawa nasononeka sana hadi wakati mwingine nikawa napoteza uzito kwa kumuwaza, na uwezo wangu darasani ukawa unashuka, kila nikimfuata anakataa hadi inapotokea marafiki zangu wanapomfuata na kumbembeleza ndipo anakubali. Hii imetokea zaidi ya mara moja . Siku moja mmoja kati ya rafiki yake alinionea huruma na kuniambia kuwa huyo msichana wangu alikuwa anafanya vile pale tu anapojisikia, yaani akiamua kunikondesha ananikondesha, alikuwa anawaambia wenzake ngoja nimchemshe flani, ilikuwa kama aina ya mchezo wake kwangu, hivyo akanishauri niachane nae, lakini bado nilishindwa hadi nilipomaliza kidato cha nne na kuondoka shuleni ndipo nilipomsahau.
Sasa nipo nje ya nchi ninasoma na imetokea mimi na yule binti tumeanzisha upya mawasiliano tu, siku moja wakati tunaongea nikamuuliza kiutani kwamba alikuwa anaonaje kama turudishe uhusiano wetu??, binti wa watu akakubali bila matatizo, na kwa sasa anaonesha mahaba haswa, haipiti saa kani sms au kupiga kabisa, isitoshe amemwambia mama yake kuwa tumerudiana. Sasa hapo ndipo linapokuja tatizo kwani nilikuwa namtania tu na isitoshe nina mpenzi kwa sasa ambaye tunapendana kiukwelia kwelia.Kumwambia nilikuwa namtania naogopa maana sijui itakuwaje, mbaya zaidi katika maisha yangu huwa najisikia fedheha sana pale nimuonapo mwanamke akillia achilia mbali nikiwa chanzo.
Ndugu zangu najua nilikosea pale nilipotania kwani nilijua atakataa kwa kuwa alishawahi niambia hanipendi, Naombeni msaada wenu, akili imestaki.((
Kumwambia siwezi na kuendelea kukaanalo siwezi maana nahisi namsaliti mpenzi wangu.
Msaada wana JF.