Majeshi ya Ukraine yameukomboa Mji wa Kharkiv baada ya Mashambulizi Makali dhidi ya Majeshi ya Urusi

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Wanajeshi wa Ukraine wameukomboa mji mzima ambao Ni wa pili kwa ukubwa Nchini Humo wa Kharkiv baada ya Wanajeshi wa urusi kuukimbia mji huo. Vijiji vingi hasa mashamba yamejaa miili ya Raia na Wanajeshi wa Urusi.

Wakionekana wenye furaha kubwa kupita maelezo,Wanajeshi wa Ukraine wameishukuru Marekani kwa kuwapatia mafunzo na Silaha za kushambulia mbali Jambo lililowafanya kushambulia maeneo yaliyokwisha tekwa na majeshi ya Urusi na kuyafanya yaanze kukimbia miji iliyotekwa.

Wanajeshi hao wamekili kwamba,endapo wangelipata Silaha hizo tangu mwanzo,Basi Majeshi ya Urusi yangeliweza kuteka hata eneo moja la Ukraine.

Haya yanakuja huku Bunge la Senate la Marekani Kuuangusha mswada wa bajeti Mpya ya Kijeshi wa Marekali kwa ajili ya Ukraine. Msaada wa awali wa $ 3.6B umekwisha na hivyo Rais Biden aliliomba Bunge kupitisha kiasi Cha $ 33B kwa ajili ya msaada wa Kijeshi kwa Ukraine. Bunge la Congress lilipitisha kiasi Cha $ 40B kwa ajili ya Ukraine,lakini Bunge la Senate limeutupilia mbali mswaada huo wakitaka Tume uchunguze kwamba matumizi ya msaada wa awali baada ya Wabunge wa REPUBLICAN kupinga Sera ya Biden kwenye Vita vya Ukraine.

Wataalamu wanasema kwamba,Biden na chama Cha Democrat wamepitisha kiasi hicho Cha Pesa cha $ 40B ili Kama Chama Chao kikishidwa kwenye Uchaguzi wa Mwezi November wa Bunge Basi Msaada kwa Ukraine uwepo pale pale bila kutatizwa na WaRepublican ambao maoni yanaonesha yatayadhibiti mabunge yote ya Congress na Senate Jambo litakalo hatarisha uwepo wa msaada wa kijeshi kwa Ukraine. WaRepublican wengi wanapinga Matumizi makubwa ya Kijeshi ya Serikali ya Biden katika kupeleka Silaha Nchini Ukraine.

Institute for the Study of War says evidence suggests Russia moving to withdraw amid strong Ukrainian counteroffensive. Ukraine wins ‘Battle of Kharkiv’; More war crimes charges planned



===========================

Wanajeshi wa Urusi waanza kujiondoa katika Mji wa Kharkiv Nchini Ukraine

Imeelezwa kuwa wanajeshi wa Urusi wameanza kujiondoa katika Mji wa Kharkiv Nchini Ukraine, hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanya mashambulizi katika Mji huo kwa wiki kadhaa mfululizo.

Jeshi la Ukraine ndilo lililotoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa Urusi wameelekeza nguvu zao katika kufanya mashambulizi katika eneo la Mashariki kunakotumika kusambaza bidhaa kwa Wanajeshi wa Ukraine waliosalia huko.

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Oleksii Reznikov amesema Ukraine inaingia katika kipindi kigumu cha vita vya muda mrefu, huku Rais Volodymyr Zelenskyy akisema Ukraine inafanya jitihada kubwa kuwaonda wavamizi, lakini matokeo ya vita yatategemea uungwaji mkono wa Ulaya na washirika wengine.

Baada ya kushindwa kuikamata Kyiv tangu walipoanza uvamizi Februari 24, 2022, Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameelekeza nguvu katika mashambulizi ya Donbas, eneo la viwanda ambalo limekuwa likitaja kujitenga kutoka katika utawala wa Ukraine tangu 2014.

Source: Apnews
 
... hawa jamaa nimewavulia kofia kwa hakika! Jeshi la Ukraine linatisha.

Cc: YEHODAYA, Glenn, Aleyn, Frank Wanjiru, et. al. njooni huku kuna habari mpya. Yale yasiyodhaniwa yamewezekana!
Jeshi la Ukraine hatari

Tulionya humu toka vita ilivyoanza kuwa Mrusi atakiona cha mtema kuni kwa kuvamia Ukraine

Hongera majeshi dume.ya Ukraine
 
... hawa jamaa nimewavulia kofia kwa hakika! Jeshi la Ukraine linatisha.

Cc: YEHODAYA, Glenn, Aleyn, Frank Wanjiru, et. al. njooni huku kuna habari mpya. Yale yasiyodhaniwa yamewezekana!
Jana Bwana Lukashenko amewaambia wanajeshi wake kwamba Kuweni na commitment kama wanajeshi wa Ukraine, pamoja na udogo wake wameweza kuonesha commitment kubwa sana kwenye jambo la Russia
 
Institute for the Study of War says evidence suggests Russia moving to withdraw amid strong Ukrainian counteroffensive. Ukraine wins ‘Battle of Kharkiv’; More war crimes charges planned
Nimefuatilia link uliyoiweka ya Al Jazeera. Hakuna mahali Aljazeer wameweka ushahidi wa maelezo uliyotoa kwenye bandiko la kwanza la uzi huu. Hakuna mahali wanaoonyesha askari wa Ukraine wanafurahia msaada wa Marekani!

Kibaya Zaidi Hata Aljazeer wameanza'kukwepa' kutoa taarifa za kina juu ya chanzo cha habari hiyo kwa kutumia vitu visivyona anwani mfano " The Institute for the Study of War"

wanatoa maelezo ya kusadikika

Maana wanajua watumbuliwa. Jisomee mwenyewe

Ukraine appears to have ‘won the Battle of Kharkiv’: IOW​

The Institute for the Study of War (IOW) says it appears that Ukraine has “won the Battle of Kharkiv”, with evidence suggesting Russia has “likely decided” to withdraw fully from its positions around the city because of the strength of Ukrainian counterattacks and a lack of reinforcements.
 
Mbuzi anazidi kutafuta mbwa.

Wiki ijayo kuna mzigo mpya na wakutisha wa silaha utatua Ukraine. Nakuambia kama mpaka wiki ijayo kutakuwa na Askari yeyeyote wa kirusi ndani ya mipaka ya Ukraine basi huyo atakuwa ni sehemu ya mbolea kwenye mashamba ya alizeti na ngano.

Ipo ivi wiki ijayo Ukreni itarusha ndege vita za kutosha juu ya anga lake lote na vikosi vyake vitafanya Usafi katika Aridhi yote ya Ukrein na baada ya apo Zelesk atatangaza kumalizika kwa awamu ya pili ya mapambano na kutangaza awamu ya tatu ya mapambano kwenda kuikomboa Crimea
 
Jana Bwana Lukashenko amewaambia wanajeshi wake kwamba Kuweni na commitment kama wanajeshi wa Ukraine, pamoja na udogo wake wameweza kuonesha commitment kubwa sana kwenye jambo la Russia
... wakati Ukraine wanapigana kuilinda nchi ya mababu zao urithi kwa vizazi vyao, wanajeshi wa Russia wanapigana kumfurahisha fashisti mmoja mpumbavu. Commitment itatoka wapi?
 
Mkuu mbona link uliyoweka na maelezo yako vinatofautiana juu ya kuukomboa huo mji?. Maana inaonekana kama taarifa haiko confirmed lakini wewe umeconferm kabisa , au uelewa wa maneno na usomaje wa maneno yenye funga semi na fungua semi maana yake haieleweki?. Mkuu wetu tueleze kwa uelewa wako haya maelezo wapi wameconferm wamekomboa?.

Ukraine appears to have ‘won the Battle of Kharkiv’: IOW​

The Institute for the Study of War (IOW) says it appears that Ukraine has “won the Battle of Kharkiv”, with evidence suggesting Russia has “likely decided” to withdraw fully from its positions around the city because of the strength of Ukrainian counterattacks and a lack of reinforcements.
 
Mkuu mbona link uliyoweka na maelezo yako vinatofautiana juu ya kuukomboa huo mji?. Maana inaonekana kama taarifa haiko confirmed lakini wewe umeconferm kabisa , au uelewa wa maneno na usomaje wa maneno yenye funga semi na fungua semi maana yake haieleweki?.
somapo hata humo basi
 
Back
Top Bottom