Poleni sana wakuu, bahati mbaya sana nchi hii hatuna police wanaojua wajibu wao zaidi ya kushabikia siasa. Wao wanajua kuwapiga raia kwa risasi za moto pale wanapodai haki zao za msingi.
hi jf.
Nimepokea habari za kusikitisha kutoka sengerema inayoeleza kama ifuatavyo:-
huko kambi ya bugombe kata maisome tarafa kahunda (w) sengerema (m) mwanza.majambazi wapatao zaidi ya wawili wakiwa na silaha smg/sar na mapanga walivamia nyumba ya kulala wageni ya mandela na madini na kupora vitu mbalimbali vikiwa na thamani ya tsh.24,314,500/=
wageni katika nyumba hizo walikuwa wenyeji wa kutoka mikoa ya shinyanga, kigoma, bukoba na nchi ya jirani ya rwanda. Asilimia kubwa ya wageni hao ni wafanya biashara.
Hakuna aliyetiwa nguvuni na jeshi la polisi, na kila mwenye taarifa sahihi juu ya majambazi hawa asisite kuwasiliana na uongozi wa polisi wilaya ya sengerema au polisi mkoa wa mwanza.