Majambazi saba yakamatwa dar wakiwa na sare za askari polisi

Verdy CB

Senior Member
Mar 19, 2013
149
66
Majambazi saba yamekamatwa maeneo ya kiluvya wakiwa na sare za akari polisi zenye vyeo, radio call za polisi, vitambulisho vya kipolisi na bunduki. Majina yao sijayasikia

Report hii imetolewa na Suleiman Kova

Source: Kurasa EATV

======
Hivi huwa wanatoa wapi vifaa hivi vyote?

Je wananchi tukiacha kuwaamini maaskari wetu, tutakuwa tumekosea?

Jeshi letu lijipangeee, heshima yake inashuka. Japo ninawapa hongera kwa kuwakamata hawa watu saba.
 
Mwakyembe anafanya kazi ya kuamsha kila idara....

Ila isiwe wanawasingizia tu
 
Eti kuna ukweli wowote kuhusu polizi badia waliokamatwa DSM

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Sasa mbona hatujaonyeshwa hao majambazi tumeonyeshwa nguo na silaha au ndo njama za kutufanya tuamini hata yule aliyesemekana karusha bomu nae alikua bandia .tafakari chukua hatua

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Usiwe na mchecheto. Nchi safi na jeshi la Polisi lipo imara. Haya matukio ni shamrashamra tu za kuiaga Tanzania Bara na kukaribisha Tanganyika ndani ya Serikali tatu. Si unajua tupo katika maandalizi ya Katiba Mpya. Tanganyika ikizinduliwa Jeshi la Polisi litakuwa makini.
 
Nina wasiwsi hata mkuu wao ni feki, hata yule aliempiga risasi Ponda hakuwa polisi wa kweli.
 
Unataka Kova aonyeshe wajomba na shemeji zake????
Ujambazi wa Kipolisi mara nyingi sana una connection na polisi wenyewe na watendaji wakuu serikalini.
Ndiyo maana akina Kinje na RiziOne huweza wapitisha mules wao wa UNGA pale Airport kirahisi kabisa.

Sasa mbona hatujaonyeshwa hao majambazi tumeonyeshwa nguo na silaha au ndo njama za kutufanya tuamini hata yule aliyesemekana karusha bomu nae alikua bandia .tafakari chukua hatua

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwa usahihi ungesema: Askari Polisi wanaswa wakiwa kwenye harakati za kufanya tukio la Ujambazi..
 
Back
Top Bottom