ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Askari Polisi saba wakiwemo watano wa kituo cha Polisi Usa Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha wamefukuzwa kazi kwa fedheha kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 100.

Wiki iliyopita Kamanda wa TAASISI ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini {TAKUKURU}Mkoani Arusha,James Ruge alikiri kuwakamata askari hao kushawishi na kupokea kiasi hicho Cha fedha ili wasimfungulie Kesi ya uhujumu uchumi ambapo angefia gerezani.

Hata hivyo Ruge alisema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na ukikamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya makasa mzima.

Vyanzo vya Habari vilisema kuwa mienendo ya mashtaka ya kijeshi ya kipolisi ilifanyika katika tarehe Aprill 22,23,24 na tarehe 25 mwaka huu , ambapo Askari hao walifukuzwa kazi rasmi ndani ya jeshi la polisi na sasa wanasubiri kushitakiwa katika Mahakama za kiraia wakati wowote.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa juu ya jeshi hilo kuchukua hatua hizo alisema kuwa hayo ni mambo ya ndani ya Polisi na sio rahisi kutolewa hadharani kwani ni kinyume na maadili ya kazi.

Naye mhanga wa tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara wa mji wa Usariver,Profesa Justin Maeda{77}akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Nshuku kata ya Nkoaranga wilayani Arumeru alisema pamoja na mkasa wote alioupata na kuishukuru Polisi kwa hatua walizochukua ila amesikitishwa na kitendo cha polisi hao kukiuka maadili ya kazi na kuomba rushwa katika kituo cha Polisi Usa hatua ambayo ilimshangaa na kushindwa kujua OCD na OC CID washindwe kujua tukio hilo.

Profesa Maeda ambaye alianza kufundisha UDSM Mwaka 1970 na kuwafundisha viongozi wengi wa serikali kabla ya kuwa Mshauri Mkuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1981-1985 Ikulu sasa ameanza kuamini maneno ya watu wa Usa kuwa ndani ya kituo cha polisi Usa kinanuka rushwa na kuna askari wa kituo hicho kitendo cha upelelezo ni miungu mtu kwani wako hapo kwa miaka mingi sasa wamejivika ufalme wa kuomba kiasi chochote cha rushwa ndani ya kituo mhicho bila kuogopa chochote.

Alisema kama yeye amebambikiwa kesi ya nyaraka za serikali na kuchomekewa shambani kwake na kutakiwa kutoa rushwa ya shilingi milioni 200 kabla ya kufikia makubaliano ya shilingi milioni 100 kuna raia gani Arumeru wameshafanyiwa unyama wa aina hiyo kwani hiyo ni hatari na viongozi wakuu wa polisi Mkoani Arusha na Makao makuu wanapaswa kutupia macho zaidi kituo hicho maana dhuruma na uhuni umekithiri kupita kiasi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa.

Profesa Maenda ambaye ana Mke na Watoto watatu ambao wote wako nje ya nchi alisema polisi hao ambao walikuja nyumbani kwake na gari mbili za polisi marchi 19 mwaka huu majira ya kati ya saa 7 mchana na saa 8 wakiwa wamejaa kwenye gari na wakiwa na silaha na gari ndogo aina ya Rv4 ambayo hakufanikiwa kushika namba walijitambulisha kuwa ni polisi ya Us ana makao makuu na alimtambua mmoja{jina tunahifadhi} wameagizwa kwenda kwake kupekua kwa kuwa wanataarifa za kiitelejesia kuwa anafanya biashara ya nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo na Ngozi za chui.

Alisema kwa kuwa hajawai na hajui kitu kinaitwa Nyara za serikali na hajawahi kufanya biashara hiyo aliwaruhusu kufanya upekuzi lakini cha kushangza hawakufanya ndani ya nyumba bali walikuwa wakipita nje ya kwenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki.

Profesa ambaye ameshafanya kazi UN hususani UNICEF nchi mbali za kiafrika na kumalizia nchi ya Zimbabwe mwaka 2002 alion aaskari mmoja akichukua mzinga na kutoa ndani ya mzinga kitu alichodai ni meno ya tembo na kusema hicho ndio kitu walichokuwa wakikitafuta.

Alisema kuwa yeye alisema shambani kwake hukaa zaidi ya miezi miwili au mitatu kuingia hivyo aliwauliza askari hao hii imeletwa na nani kwani hajawahi kufanya biashara hiyo ila alijibiwa na askari hao kuwa hiyo imekula kwake kwani hii ni kesi ya uhujumu uchumi na angefungwa Maisha hivyo anatakiwa kuweka mambo sawa.

Mzee huyo ambaye isema alistaafu miaka ishirini iliyopita alilipwa kiinua mgongo chake{PENSHENI} cha kiasi cha shilingi milioni 74 na kuweka benki ya CRDB na NMB alichukuliwa hadi kituo cha polisi Us ana kuanza kuchukuliwa maelezo na kuombwa rushwa ya shilingi milioni 200 wakati akitoa maelezo.

Profesa alisema yeye aliwaambia kuwa jana yake yaani marchi 18 mwaka huu alikwenda benki na kuchukua kiasi kidogo cha pesa hivyo kiasi hicho hana na kuwataka wapokee milioni 100 na ndipo alipokwenda benki akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na kuchukua shilingi milioni 74 na baadae alikwenda dukani kwa mdogo wake hapo Usariver na kuchukua kiasi cha shilingi milioni 30 na zote aliwapa polisi katika kituo cha Usa kwani rushwa ilifanyika hapo.

Alisema na kuiomba serikali iweze kumrudishia kiasi cha pesa yake kwani ni kiunua mgongo cha utumishi wake wa kazi wa miaka mingi kazi.

Mwisho


Ar1.jpg
Ar2.jpg
 
Back
Top Bottom