Majaliwa kuwabana Mawaziri na Wabunge kurejesha Mikopo ya Elimu ya juu

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, amepewa ‘rungu’ ili kuweka shinikizo kali dhidi ya baadhi ya mawaziri na wabunge warejeshe mikopo ya Elimu ya juu waliyopewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu HESLB.

Mawaziri, manaibu na wabunge wanaolengwa ni wale wanaodaiwa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), na kazi hiyo itafanywa kwa kushirikisha ofisi ya Bunge pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.

Gazeti hili tayari limethibitishiwa kuwapo kwa orodha ya viongozi kadhaa wenye majina makubwa (vigogo) bungeni, kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kambi ya Upinzani.
Orodha hiyo ya vigogo wanaodaiwa mikopo sasa imepewa jina jipya la “List of Shame 2” ikifananishwa na orodha ya mafisadi iliyotangazwa na vyama vya upinzani ikihusisha majina ya vigogo wa serikali.
Raia Mwema linafahamu majina ya baadhi ya vigogo walio katika orodha hiyo lakini itawatangaza mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote za uhakiki wa madeni yao.

HELSB imekuwa ikilalamikiwa kwa makusanyo madogo ya mikopo ya wanafunzi na hatua hii ya serikali kuwatambua vigogo wanaodaiwa inaweza kuifanya jamii nzima kufahamu umuhimu wa kulipa mikopo hiyo.

“Waziri Mkuu ameamua kulivalia njuga suala hili na kupitia kwa Waziri wa Elimu au yeye mwenyewe moja kwa moja, majina ya vigogo wanaodaiwa yanaweza kuwekwa hadharani.
“Magufuli anataka sheria zisimamiwe bila kusita na kwa hiyo, ukisoma sheria ya kuanzisha Bodi ya Mikopo, kifungu cha 20 (1) (c) pamoja na mabadiliko yake, kinawataka waajiri baada ya kuwatambua waajiriwa wao, waijulishe bodi kwa maandishi ndani siku 28 tangu wapate ajira.

“Lakini wengi hawafanyi hivi… kwenye ofisi nyingi tu, serikali hii sasa inataka kusimamia sheria bila aibu,” kilieleza chanzo chetu cha habari kutoka ofisi ya Bunge ambako taarifa rasmi kuhusu wabunge wadaiwa imefikishwa kwa uongozi wa chombo hicho cha kutunga sheria nchini.
Tayari Raia Mwema imetaarifiwa kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alikwishaanza kukagua taaasisi za umma kujiridhisha kama zinatii matakwa hayo ya kisheria.
 
Lowasa alisema angechaguliww elimu ingekua bure na wenye madeni heslb wangefutiwa. Wacha tuisome namba
 
maziwa yakiisha safari hii ng'ombe atakamuliwa hadi damu..... wazungu wamekohoa ati.
 
Back
Top Bottom