Majaji nao

Foundation

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
1,421
596
Majaji 12 wapata kikombe kwa Babu Saturday, 02 April 2011 08:56 0diggsdigg

Na Waandishi Wetu
MAJAJI 12 ambao ni wakuu wa Kanda za Mahakama Kuu ya Tanzania, jana waliingia katika orodha ya vigogo kufika Samunge, Loliondo kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila.Habari zilizopatikana jana zimeeleza kwamba majaji hao walifika Samunge wakitokea Arusha ambako walikuwa na semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Idara ya Mahakama katika kushughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu.

Majaji hao, walifika kijiji hapo majira ya saa saba mchana wakiwa wanaongozwa na maofisa wa Serikali wilayani Ngorongoro. Walifika kwa magari ya kukodi aina ya Land Cruiser ambayo ni maalumu kwa ajili ya kubeba watalii.

Tofauti na viongozi wengine, majaji hao, walikwenda kwa njia ya barabara wakitokea Arusha mjini na mara baada ya kufika nyumbani kwa mchungaji Mwasapila, waliandaliwa eneo maalumu na kila mmoja kupata kikombe cha dawa.

SOURCE: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom