Maiti yazua taharuki Hospitali, mwili wazikwa mara mbili

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1684560053374.png

Ilikuwa Mei 18 mwaka huu siku ambayo ilizuka taharuki na sintofahamu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro baada ya mwili wa mzee Melkiori Ndambale (85) uliokuwa umehifadhiwa katika hospitali hiyo kutoonekana kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Siku hiyo ndugu wa marehemu huyo mzee walifika katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti kwa lengo la kuchukua mwili kwa ajili ya maziko na kuukosa mwili wa mpendwa wao, jambo lililosababisha uongozi wa hospitali kuusaka.

Maulid Ndambale ni mdogo wa marehemu amesema kuwa baada ya uongozi wa hospitali kufuatilia katika vitabu kumbukumbu, ilifahamika kuwa mwili wa kaka yake ulichukuliwa na familia moja ambayo nayo ilikuwa na imemuhifadhi baba yao katika chumba hicho na kisha kwenda nao wilayani Kilosa kwa ajili ya maziko.
"Tukiwa pale pale mochwari tukapata taarifa kuwa tayari baba yetu huko Kilosa na kwamba Tayari alikuwa keshazikwa tena kwa dini ya kiislamu, na ilionekana kuwa hao watu wa Kilosa waliuacha mwili wa baba yao hapa hapa mochwari," amesema Ndambale.

Amesema kuwa kufuatia hali hiyo jana jioni (Mei 18) uongozi wa hospitali hiyo ulifanya jitihada za kwenda Kilosa kufukua na kuurudisha mwili baba yao Morogoro mjini na kuukabidhi kwaajili ya maziko yaliyofanyika leo (Mei 19) katika makaburi ya kola Manispaa ya Morogoro.

"Taarifa tulizopata ni kwamba ule mwili mwingine uliokuwa umeachwa, Tayari ulishapelekwa Kilosa na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya maziko. Hata hivyo siwezi kuzungumzia sana taratibu za huko Kilosa kwa kuwa mimi sio mwanafamilia," amesema Ndambale.

Wakati taratibu hizo zilipokuwa zikiendelea Mwananchi alimtafuta mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka kueleza tukio hilo ambapo amekiri kutokea kwa sintofahamu hiyo kwenye wilaya yake hata hivyo alisema kuwa jambo hilo kwa kuwa lipo kwenye ngazi ya hospitali ya rufaa mkoa na kwamba yeye kama mkuu wa Wilaya asingeweza kulizungumzia.

"Na mimi nimesikia na nimetuma vyombo vyangu vya ulinzi na usalama wilaya kufuatilia kwa karibu," amesema Shaka.

Baada ya uongozi wa hospitali hiyo kurudisha mwili huo Morogoro mjini na kukabidhi kwa ndugu, mdogo wa marehemu Ndambale aliyejitambulisha kwa jina na Benedius Towela amesema kuwa wanashukuru kwa ushirikiano ulioupata kutoka kwa uongozi wa hospitali hiyo hadi kufanikiwa kuupata mwili wa ndugu yao na kuuzika kwa imani ya dini ya kikristo ambayo alikuwa akiamini marehemu.

"Haikuwa makusudi tunaamini ni bahati mbaya tu ilikuwa imetokea kwa yule muhudumu wa mochwari na hata wale watu waliochukua mwili wa kaka yangu na kuupeleka Kilosa, kama familia tumewasemehe, na pia tumeusamehe uongozi wa hospitali yetu, kwa sababu sisi sote ni binadamu na hakuna binadamu aliyekamilika, bahati mbaya kwenye kazi ni kitu cha kawaida kabisa," amesema Towela.

Baadhi ya majirani waliofika katika maziko ya Ndambale wameuomba uongozi wa hospitali kuimarisha umakini ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo mizuri ya utambuzi wa miili ya marehemu inayohifadhiwa hospitali hapo, ili isije ikajitokeza tena changamoto kama hiyo na hivyo kuzua itazua taharuki kama ilivyotokea.

Mmoja wa majirani hao Grace Joseph amesema kuwa baada ya kutokea kwa sintofahamu hiyo alisikitika kwa kuwa anamfahamu vizuri marehemu Ndambale.

"Leo pamoja na kuja kuzika lakini nilikuwa na shahuku ya kuhakikisha kama kweli mzee Ndambale karudishwa na leo tunamzika nashukuru nimemuona ni yeye na nimemuaga," amesema Grace.

Uongozi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro ulipotafutwa kueleza kilichotokea mpaka miili hiyo ikabadilishwa umedai kuwa tayari suala hilo limeshashughuliwa na miili yote imeshakabidhiwa kwa ndugu na kuzikwa.

Aidha, imeelezwa kuwa hali hiyo imetokea kutokana na ukweli kuwa watu toka Kilosa hawakuwa ndugu wa karibu na marehemu hivyo walishindwa kuutambua mwili huo vizuri na kingine inawezekana ni hali ya uoga wa ndugu pale wanapoitwa kuutambua na kuosha mwili wa ndugu yao na hivyo majukumu yote hayo kumuachia muhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti.

MWANANCHI
 
Inahitaji resilience ya Hali ya juu katika kufanya kazi sensitive kama hizo
 
Kwani ukienda kumchukua marehemu si unamuangalia? Kumkagua na kuthibisha kuwa ndio yeye? Hao wengine pia hawakufanya hivyo ?
 
Back
Top Bottom