Maiti afufuka chumba cha maiti - Iringa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
DSCF2298.JPG
DSCF2306.JPG
DSCF2304.JPG

MAITI YAFUFUKA IKIWA MOCHWARI YARUDISHWA KWA MADAKTARI

Mauaza uza yaibuka mjini Iringa baada ya mgonjwa ambaye alifika kufanyiwa maombi kwa mmoja kati ya wahubiri maarufu mkoani Iringa kukata kauli yake akiwa nje ya ukumbi huo maarufu wa maombi mjini hapa na baada ya kufikishwa chumba cha kuhifadhiwa maiti (Mochwari) katika hospital ya mkoa wa Iringa maiti hiyo iliamuka na kupelekea ndugu kuupeleka mwili huo kwa madaktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mke wa mgonjwa huyo Amina Ramadhan alisema kuwa mme wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa kabla ya jana mgonjwa huyo kuomba kuletwa mjini Iringa kwa mhubiri huyo maarufu mkoani Iringa Boaz Sollo wa kituo cha maombezi cha overcomers .

Hata hivyo alisema kuwa akiwa katika foleni ya kuingia ndani ya ukumbi ghafla mgonjwa huyo aliomba kupelekwa chooni na kabla ya kuingia chooni alikata kauli na hivyo kulazimika kuupeleka mwili wake mochwari katika hospital ya mkoa ambako kabla ya kuingizwa Mochwari ghafla marehemu aliamuka na kuanza kurusha rusha mikono yake hali iliyopelekea kurudishwa tena mapokezi kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi na kumtaja mjane wa marehemu Bi Amina Ramadhan alimtaja marehemu kuwa ni Gerald Tadei Ngusi

Tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa IDYDC mjini Iringa na hadi mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima unatoka hospital hapo majira ya saa 11 .20 jioni madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.

... Na kabla ya kuingia chooni alikata kauli na hivyo kulazimika kuupeleka mwili wake mochwari katika hospital ya mkoa ambako kabla ya kuingizwa Mochwari ghafla ..

Hivi kumbe Kukata kauli ni ishara tosha kuwa kesha fariki... strange!!!!
 
Huyo hakufa bwana, alikata kauli. Mtu akizimia wewe kama sio mtaalamu unaweza kujua kesha kufa tayari.
 
Maiti haipokelewi mortuary mpaka dr a_certify! Stori haijatulia hii

Soma habari yote kabla ya kutoa comment. Madaktari walithibitisha kuwa ameshakufana na kuruhusu kwamba maiti apelekwe mortuary kama ifuatavyo hapa chini:
Tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa IDYDC mjini Iringa na hadi mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima unatoka hospital hapo majira ya saa 11 .20 jioni madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.
 
Maiti haipokelewi mortuary mpaka dr a_certify! Stori haijatulia hii

Soma kwanza story yote tangu mwanzo hadi mwisho kabla ya kutoa comment. Paragraph ya hapo chnini ambayo ni ya mwisho wa habari inahitimisha kwamba maiti ilikuwa certified by the doctor.

Tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa IDYDC mjini Iringa na hadi mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima unatoka hospital hapo majira ya saa 11 .20 jioni madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.
 
Tatizo ni madaktari wetu si werefu wa kutumia vema utaalamu wao. Huyu mgonjwa alikufa nusu kaputi, mapigo ya moyo yalikuwa chini sana, na hivyo kuna vyombo kadhaa vinavyotumika kupima kuhakiki uhai wa mgonjwa au umetoweka kabisa. Hii ni aibu sana kwa taaluma ya waganga.
 
Wakati ndugu yangu alipofariki recently how l wished muujiza kama huo ungetokea! Yaani hata siku ya pili tunavalisha Nguo ready kwa safari kuelekea kwetu bado nilikuwa nawish pamoja na kwamba mwili wake ulikuwa na baridi ya kutoka kwenye jokofu!

Mungu ampe miaka zaidi huyo mkaka; ni relief kubwa kwa familia! Haijalishi ni muujiza au alikuwa kwenye coma kikubwa ni mzima sasa!
 
dscf2298.jpg
dscf2306.jpg
dscf2304.jpg

maiti yafufuka ikiwa mochwari yarudishwa kwa madaktari

mauaza uza yaibuka mjini iringa baada ya mgonjwa ambaye alifika kufanyiwa maombi kwa mmoja kati ya wahubiri maarufu mkoani iringa kukata kauli yake akiwa nje ya ukumbi huo maarufu wa maombi mjini hapa na baada ya kufikishwa chumba cha kuhifadhiwa maiti (mochwari) katika hospital ya mkoa wa iringa maiti hiyo iliamuka na kupelekea ndugu kuupeleka mwili huo kwa madaktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

mke wa mgonjwa huyo amina ramadhan alisema kuwa mme wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa kabla ya jana mgonjwa huyo kuomba kuletwa mjini iringa kwa mhubiri huyo maarufu mkoani iringa boaz sollo wa kituo cha maombezi cha overcomers .

hata hivyo alisema kuwa akiwa katika foleni ya kuingia ndani ya ukumbi ghafla mgonjwa huyo aliomba kupelekwa chooni na kabla ya kuingia chooni alikata kauli na hivyo kulazimika kuupeleka mwili wake mochwari katika hospital ya mkoa ambako kabla ya kuingizwa mochwari ghafla marehemu aliamuka na
kuanza kurusha rusha mikono yake hali iliyopelekea kurudishwa tena mapokezi kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi na kumtaja mjane wa marehemu bi amina ramadhan alimtaja marehemu kuwa ni gerald tadei ngusi

tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa idydc mjini iringa na hadi mtandao huu wa francis godwin mzee wa matukio daima unatoka hospital hapo majira ya saa 11 .20 jioni madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.

tuchukue lipi, amefariki au amerudiwa na uhai? Kama amerudiwa na uhai, mke wake anaitwa mjane, na aliyerudiwa na uhai anaitwa marehemu? Unajichanganya mwenyewe, kifupi hueleweki. Jipange vizuri ndugu
 
Wakati ndugu yangu alipofariki recently how l wished muujiza kama huo ungetokea! Yaani hata siku ya pili tunavalisha Nguo ready kwa safari kuelekea kwetu bado nilikuwa nawish pamoja na kwamba mwili wake ulikuwa na baridi ya kutoka kwenye jokofu!

Mungu ampe miaka zaidi huyo mkaka; ni relief kubwa kwa familia! Haijalishi ni muujiza au alikuwa kwenye coma kikubwa ni mzima sasa!

DSCF2304.JPG

Mke wa mfufuka

Kwa vyo vyote Mungu anatoa funzo fulani kwetu, si jambo la kawaida maana hata mke wake ni kama haamini vile.
 
Soma kwanza story yote tangu mwanzo hadi mwisho kabla ya kutoa comment. Paragraph ya hapo chnini ambayo ni ya mwisho wa habari inahitimisha kwamba maiti ilikuwa certified by the doctor.

Hapana mkuu, jinsi ulivyoiripoti tafsiri yangu (nadhani na ya king'asti) ni kuwa huyo bwana hakuthibitishwa kama ameshafariki. Ila baada ya "kufufuka" ndipo alipotolewa mochware na kupelekea madaktari kuthibitisha sasa kuwa kweli ameshafariki (ambapo supposedly ndio muda source wa habari hii alipotoka hospitalini hapo)

Kwangu mimi hakuna kufufuka hapo katika habari hii. Ni kwamba ndugu huyo alikuwa amekata tu kauli (si kufa) hadi pale madaktari walipothibitisha kuwa amefariki. Labda kama kuna maelezo tofauti ya story hii.
 
Tatizo ni madaktari wetu si werefu wa kutumia vema utaalamu wao. Huyu mgonjwa alikufa nusu kaputi, mapigo ya moyo yalikuwa chini sana, na hivyo kuna vyombo kadhaa vinavyotumika kupima kuhakiki uhai wa mgonjwa au umetoweka kabisa. Hii ni aibu sana kwa taaluma ya waganga.

Alikufa nusu kaputi?
 
Hata ku certify kifo kunahitaji utaalamu gani? Je, una uhakika alionwa na daktari? Au hata hao auxiliary nurses unaowaona hapo juu wewe wawaita madaktari? Siamini kama huyo jamaa alionwa na daktari MD.
 
tuchukue lipi, amefariki au amerudiwa na uhai? Kama amerudiwa na uhai, mke wake anaitwa mjane, na aliyerudiwa na uhai anaitwa marehemu? Unajichanganya mwenyewe, kifupi hueleweki. Jipange vizuri ndugu

Hakuna la kuchukua hapa mkuu. Utata wa story huu unalazimishwa na masimulizi yenye controversy. So ni better kusema hii story iko na confusion zaidi kuliko maajabu ya "kufufuka" ambayo allegedly inasema yametokea
 
Hapana mkuu, jinsi ulivyoiripoti tafsiri yangu (nadhani na ya king'asti) ni kuwa huyo bwana hakuthibitishwa kama ameshafariki. Ila baada ya "kufufuka" ndipo alipotolewa mochware na kupelekea madaktari kuthibitisha sasa kuwa kweli ameshafariki (ambapo supposedly ndio muda source wa habari hii alipotoka hospitalini hapo)

Kwangu mimi hakuna kufufuka hapo katika habari hii. Ni kwamba ndugu huyo alikuwa amekata tu kauli (si kufa) hadi pale madaktari walipothibitisha kuwa amefariki. Labda kama kuna maelezo tofauti ya story hii.

na mimi nimeelewa kama wewe mkuu,labda wengine mtueleweshe vzr kwamba mwisho wa siku jamaa ni mzima au ni marehemu?naona mnajichanganya tu
 
Kama amefufuka inakuaje mumbatize jina la "Marehemu" na mkewe mumuite "Mjane"?.
 
Hahahaaaa, duuhizi si habari za kweli haiwezekani mtu kukatakauli halafu akaoneka bado ni mzima hayo ni maajabu ya dunia hivi dunia hiii inakwenda wapi mungu atunusuru na haya majanga
 
Tatizo ni madaktari wetu si wataalam wa kutumia vema utaalamu wao. Huyu mgonjwa alikufa nusu kaputi, mapigo ya moyo yalikuwa chini sana, na hivyo kuna vyombo kadhaa vinavyotumika kupima kuhakiki uhai wa mgonjwa au umetoweka kabisa. Hii ni aibu sana kwa taaluma ya waganga.
 
Back
Top Bottom