Maisha tunayoishi Watanzania na Waafrika ni aibu tupu

Maisha ambayo raia wa Africa na Tanzania kwa ujumla tunaishi ni aibu, huzuni na mateso matupu. Maji shida, umeme shida, ajira hakuna, huduma za afya mbovu Yani Kila kitu tatizo.

Waafrika na Tanzania kwa ujumla tunaishi katika umaskini wa kunuka ndani ya utajiri wa kutupwa. Hakika hii ni laaana!

Waafrica wanajua chuki, roho mbaya, uchawi na husuda, hakika hii ni laaana.

Laaana! Laaana! Laaana ! Hakika Africa Ina laana ya kudumu.

SWALI LA MSINGI KIPI KIFANYIKE KUONDOA LAANA HII

Binafsi, laana ya Tanzania na bara la Afrika itaondolewa na walimu tu, walimu pekee na sio wachungaji Wala ma-sheik, ni wakati sasa serikali za Africa na Tanzania kwa ujumla kulitazama kundi Hili la walimu kwa jicho la tatu

NINI MSINGI WA KUSEMA HAYA

Laana ya Tanzania na Africa inasababishwa na philosophy problem, matatizo ya kimaaadili yaani ethics issues, na ukosefu wa uzalendo. Walimu pekee ndio Wana jukumu la kushape tabia za wanafunzi ambao badae ndio watawala na raia wa kesho.

Falsafa ya mwalimu ni falsafa ya wanafunzi, na falsafa ya wanafunzi ni falsafa ya taifa.

Serikali ya Tanzania, wizi huu, huduma mbovu za jamii kama maji, umeme na afya, tiba yake ni moja tu kutengeneza mazingira Bora ya walimu na motisha ili walimu wa impart falsafa chanya kwa wanafunzi na hatimae laaana hii itutoke.


Wenu mtiifu, Wana Duce mwaka wa tatu bachelor of science with education.
Bado tunajitafuta vumilieni sio lazima wewe huishi vizuri vitukuu vyako vitaishi tu..
 
Back
Top Bottom