MAISHA PLUS: Yanayojiri...!

Hatimae mshindi amepatikaana wa MAISHA PLUS nae ni alex MABIZA WA MBEYA
hakuna mwanzo pasipo na mwisho hakuna wengi pasipo
na mshindi hatimae mama shamsi mwangunga amemtangaza mshindi wetu
nae ni ALEX MABIZA WA MBEYA
alex alikuwa mshiriki wa mashindano mwaka jana akatupwa akaenda nje
akarudi ndani ya mwaaka huuu baada ya kujipanga leo hii ametwaa million
15,000,000
 
Sasa uyu Afande sele kumbusubusu mwanaume mwenzie mbele ya camera whats up with that???
 
Kumpa ushindi kijana kama huyu ni kumuwezesha kiukweli,, though iam not sure with that 2lak distribution at least lak1 ingekuwa fair! Iyo pesa si nyingi kihivo jamani! Hao waandaaji ndo wangewafikiria hao washiriki wengine! Na je anagawa kwa hao kumi au wote!!!????
 
BAADA ya viongozi wa asasi za kiraia (NGOs) kutajwa katika nafasi ya chini miongoni mwa makundi za wananchi wanaoaminiwa katika jamii, asasi wanazoziongoza zimeshutumiwa kwa kuwanufaisha watu binafsi zaidi ya jamii ambayo ndiyo chimbuko lake.

Utafiti uliofanywa na asasi ya kiraia ya Foundation For Civil Society kuhusu maoni ya umma juu ya asasi za kiraia Tanzania kwa mwaka 2009, umebaini kuwa sehemu kubwa ya wananchi wanazilaumu asasi hizo kwa kuwatajirisha watu binafsi zaidi ya jamii.

Shutuma hizo zimetolewa na jamii ya watu wanaozunguka miradi ya maendeleo ya asasi hizo walipotakiwa kuelezea mambo wanayoyachukia kuhusu asasi hizo.

Katika utafiti huo, watu 800 kwa kuzingatia jinsia kutoka mikoa minane iliyowakilisha kanda nane za Tanzania na Zanzibar, walihojiwa kwa njia ya ana kwa ana kwa dakika 20 kwa kila mwanajamii.

Kabla ya utafiti huo, utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2007 kwa kuhoji jumla ya Watanzania 7,879 kuhusu makundi ya watu wanaoaminika sana na jamii, kati ya makundi 18 ya jamii yaliyotajwa kuaminiwa, viongozi wa asasi hizo walitajwa katika nafasi ya 13.

Walioongoza kwa kuaminiwa zaidi na Watanzania ni ndugu zao wa familia wakifuatiwa na viongozi wa dini, ndugu wa ukoo, walimu, watu wa kabila moja, wazee wa kike, wazee wa kiume, wenyeviti wa vijiji na kata, madaktari na wauguzi na viongozi wa mitaa huku vijana wa kiume na wageni wasio Watanzania wakishika nafasi za 17 na 18 ambazo ni za mwisho.

Utafiti huo wa mwaka 2007 uliofanywa na Asasi ya Utafuti wa Kuondoa Umasikini (Repoa), ambao ulikuwa moja ya tathimini za utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (Mkukuta), ulionesha pia kuwa wanasiasa walishika nafasi ya 11, wafanyabiashara 12 na polisi nafasi ya kumi na tatu.

Licha ya asasi hizo kushutumiwa kwa kuwatajirisha watu binafsi zaidi ya jamii, wananchi hao waliohojiwa katika utafiti wa Foundation For Civil Society pia walisema wanachukizwa na kukosekana kwa muundo sahihi wa menejimenti katika asasi hizo.

Baadhi ya mambo mengine yaliyolalamikiwa ni kukosa uwajibikaji katika fedha za miradi, hazishirikishi jamii katika mipango yao, kutawaliwa na tabaka la wasomi na kujali viongozi zaidi ya jamii.

Licha ya wanajamii wanaozunguka miradi ya asasi hizo, pia wadau wa asasi hizo wakiwemo maofisa wa serikali kutoka kiongozi wa kata, mabaraza na shehia mpaka mawaziri, vyombo vya habari, taasisi za elimu ya juu, jumuiya ya wafanyabiashara na wabia wa maendeleo walipohojiwa walitoa maelezo yanayofanana na ya jamii hizo.

Wadau hao walisema asasi hizo haziwajibiki katika fedha za miradi, zimekosa muundo sahihi wa menejimenti, zinawatajirisha watu binafsi zaidi ya jamii na haziwahusishi wanajamii katika mipango yao.

Hata hivyo, jamii hiyo na wadau walipoulizwa kama bado asasi hizo zina umuhimu katika jamii, asilimia 94 ya wadau walisema zina umuhimu na asilimia 81 ya wanajamii pia walisema zina manufaa kwao.

Walipotakiwa kueleza sekta ambazo asasi hizo zimeshindwa, sekta ya kilimo ilitajwa kuwa inayoongoza kutoshughulikiwa na asasi hizo ikifuatiwa na mazingira, utawala bora, maji safi na afya ya akina mama.

Sekta ambazo asasi hizo zimefanikiwa sana ni mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Ukimwi, elimu, kutunza yatima na makundi ya pembezoni.

Kutokana na udhaifu huo baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa katika utafiti huo ni pamoja na asasi hizo kutakiwa kuweka msukumo katika miradi ya kilimo kwa kuwa Watanzania wengi wanajihusisha nacho na kwenye mazingira na maji safi.

Aidha zimeshauriwa kutengeneza mkakati wa mawasiliano ulio dhahiri ili kupunguza hisia kwamba zinakosa uwazi, uwajibikaji na zina wafujaji.

Pia zimeshauriwa kuwajibika kwa watu kwa kuwa wao ndio wanaowafanyia kazi, kwa wafadhili kuhalalisha walichokifanya na sababu zake na kwa serikali kwa kuwa ni mdau mwenye maslahi katika utoaji wa huduma kwa umma.
 
Duh! Uko fasta chalii yangu.
Mi nimeangaliakwa mara ya kwanza leo. Lakini imenitia hasara. Nimemaliza wine zangu zote humu ndani.

Hata mimi nimeangalia leo mara ya kwanza na sikujua kama leo ndio final , ilini bore nikachange channel bada ya kumaliza ile dance , dah ningecheki iliishaje
 
haya mmeridhika na matokeo? na nini maoni yako kwa maisha plus season 3. maana yake suala iwe kuboresho sio kuchonga tu kutwa kucha.
 
walikuwaa na utovu wa nidhamu,wenzao walipokuwa mazoezini wenyewe warirudi kjjn so babu akawapa adhabu ya gogo na hiyo adhabu wakaona ni ya kawaida so babu na masud wakaamua kuwaambia waondoke kurudi kwao coz walionyesha tabia mbaya ya kumdharau babu
 
Masoud amewanyanyasa bure. Adhabu kawapa mbili ,which is out of good governance.
Kwani watu hawakosei au mood kupotea kwa sababu fulani fulani? Huku Maisha Plus, huku ngono na hao hao , kwani nini tusitafsiri cheaply kuwa waliwagomea ngono zao ndio maana wakawatimua? Logic iko wapi ? Disqualification, then wanaweza kupigiwa kura wakiwa nyumbani kwao.

Nina mashaka na Kipanya. Huenda ana elimu ya ngumbaro .CV zake jamani.
 
Masoud amewanyanyasa bure. Adhabu kawapa mbili ,which is out of good governance.
Kwani watu hawakosei au mood kupotea kwa sababu fulani fulani? Huku Maisha Plus, huku ngono na hao hao , kwani nini tusitafsiri cheaply kuwa waliwagomea ngono zao ndio maana wakawatimua? Logic iko wapi ? Disqualification, then wanaweza kupigiwa kura wakiwa nyumbani kwao.

Nina mashaka na Kipanya. Huenda ana elimu ya ngumbaro .CV zake jamani.

Jamani hivi tuna uhakika na hizi shutuma za ngono? Hebu tuwe wakweli katika comments zetu! Upo ushahidi wa Ngono huku MP? Tusije tukawanyima wengine nafasi kwa wazazi kuamini haya ambayo si hakika. Kumtuhumu mtu bila ushahidi ni vibaya. Jacqueline alisema anakubali wamekosea na haoni kwa nini watu wanalikuza...kama tunaona Masoud hafanyi tunaloona sahihi hebu tuanzishe mashindano mengine. Ni Maoni tu.
 
Maisha Plus ni usanii usanii tu, hakuna mpangalio wa matukio, yaani bi blah blah tu! Sioni mantiki yoyote ya shindano lenyewe zaidi ya kuongeza nafasi ya kuambikizwa malaria huko kijijini!
 
Ahaa ameshinda mwanaume, mara ya mwisho ile likizo ya xmass nilona kuna dogo mmoja alikuwa anatokea Iringa kwa kwei mambo yake nilkuwa namuona kama vile siyo rizki, alifika wapi yule? Na yule dada wa Dar aliyekuwa anavaa na kuact kiume naye aliishia wapi? Hao ndo ninawakumbuka at least
 
walikuwaa na utovu wa nidhamu,wenzao walipokuwa mazoezini wenyewe warirudi kjjn so babu akawapa adhabu ya gogo na hiyo adhabu wakaona ni ya kawaida so babu na masud wakaamua kuwaambia waondoke kurudi kwao coz walionyesha tabia mbaya ya kumdharau babu

nadhani bado hajajua vizuri jinsi ya kuiendesha hiyo kipindi, nadhani muda umefika sasa wa kuwashirikisha watu wengine ambao watakuwa wabunifu ili hicho kipindi kipate maboresho mazuri
 
Yule Neema wake amebaki bado.Akishinda basi confirmed ule uvumi uliokuja hapa jamvini kuwa jamaa anamla na pia kuwa ndiye mshindi aliteandaliwa


Watanzania kwa kuzusha siwawezi kiukweli, dada alikuwa na sifa zote na kushinda amekosa ushindi kwa sababu ya maneno ya wabongo wasiopenda maendeleo ya watu, haya sasa semini na yule mwanaume aliyeshinda alikuwa analala na nani?? Wabongo ndio maana tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele kwa sababu ya majungu yasiokuwa na maana yoyote.
 
Maisha Plus ni usanii usanii tu, hakuna mpangalio wa matukio, yaani bi blah blah tu! Sioni mantiki yoyote ya shindano lenyewe zaidi ya kuongeza nafasi ya kuambikizwa malaria huko kijijini!

Andaa na wewe program yako ili tuchukue mfano.
 
Maisha Plus .or Maisha Pumba?

Hivi mnategemea mtu kama Masudi Kipanya aje na kitu gani? bangi tupu.....na fans wote hiyo maisha pumba ni wa vilevile...maoni yangu tu.
 
Maisha Plus .or Maisha Pumba?

Hivi mnategemea mtu kama Masudi Kipanya aje na kitu gani? bangi tupu.....na fans wote hiyo maisha pumba ni wa vilevile...maoni yangu tu.
Don't take it too personal mzee!!
 
Wabongo na kasumba zenu siwawezi! ubaya wa maisha plus uko wapi? hivi maisha plus na big brother Africa ipi bora? najua majuha watasema BBA kwa sababu ni zao la Wazungu wa SA! na kutoka wale mabinti, jamani kile game ina sheria zake, na utaratibu wa adhabu unapovunja sheria, na tukumbuke sheria za maisha plus haziwezi fanana na BBA, Miss Tanzania wala Project fame au game yoyote nyingine ni lazima tuheshimu uamuzi wa crew ya maisha plus!
kama KP anavuta bangi na hawezi kuja na kitu bora, hivi hicho chenu msiovuta bangi kiko wapi? majungu si mtaji!
 
Maisha Plus .or Maisha Pumba?

Hivi mnategemea mtu kama Masudi Kipanya aje na kitu gani? bangi tupu.....na fans wote hiyo maisha pumba ni wa vilevile...maoni yangu tu.
Yule ni msanii na Maisha Plus ni usanii ambayo ndiyo watu wanataka. Wanaongalia wanapenda sanaa na wanategemea kuridhika na hivyo ilivyo. May be interests zako si sanaa then don't watch or change the channel or do something else. But sanaa should be sanaa!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom