Maigizo kila kukicha wacha tuizike elimu kwa ubaguzi huu

Ngolewasima

Member
Apr 4, 2017
51
112
Mwaka huu kweli masharti ni mengi mpaka napatwa na wasiwasi mkubwa.

Nimejaribu kupitia utaratibu wa utoaji wa mkopo kwa waombaji {Applicants} wa 2018/2019 kuna vigezo ambavyo ninaona hujuma juu ya watoto wa Maskini Kujiunga elimu ya juu {Chuo kikuu}.

Nimesoma kipengele cha sita kinaeleza kuwa mtoto wa mtumishi wa umma {Mtumishi ambae ametajwa kwenye kanuni za utumishi wa umma} mfano Mwalimu,mwanasheria,Muhasibu hatoruhusiwa kuomba mkopo! Yaani haruhusiwi kabisa kuomba maana yake hana vigezo!

Swali la kujiuliza Dogo tu,Asilimia kubwa ya vyuo vyetu Ada zake ni kuanzia 700,000 hapo bado Pesa za
.
~Gharama za chakula na malazi {meals & Accomodation}

~ Gharama za Vitabu na viandikwa {Stationary}

~Mahitaji maalumu ya kitivo..{special faculty}

~Ghrama za utafiti {Research}

Gharama za mafunzo ya vitendo {Field}

Je wazazi hawa amabo wana mshahara amabo haufiki walau Milioni moja. Wanao uwezo wa kuwasomesha hawa watoto wao?? Nafikiri watoto hawa wana hatihati ya kupoteza/Kukosa fursa ya kujiunga na Masomo ya elimu ya juu.

Pia nimeona kigezo cha utoaji kuwa : waombaji/Applicants wamegawanywa katika makundi matatu yaani Ualimu wa sayansi,uhandisi,sayansi ya wanyama.{kundi la kwanza}
Programu za msingi za sayansi,Programu ya sayansi ya Ardhi {kundi la Pili}
.
Kundi la tatu ni sanaa {Maana yake ni non priority} swali langu ni moja tu,,,,Je wanafunzi wanaochukua michepuo ya sanaa kama hawana maana {Serikali haina uhitaji nao} kwa nini wasifute hiyo michepuo? Tunawaruhusu watoto hawa wanasoma harafu mwishoni tunatumia kigezo cha #Uhitaji_na_Programu. This is totally unfair.
.
Ninaamini hapa kwa watoto waliosoma michepuo ya sanaa na ni watoto wa masikini serikali ya awamu ya tano inawapokonya haki yao ya kujiunga na elimu ya juu.{University level}

Mwisho,Nimeona Bodi ya mkopo imetoa Agizo kwa Wakala wa usajili ufilisi na Udhamini {RITA} Kuandaa utaratibu wa uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa/Vifo kwa waombaji upya na kila Mwombaji/Applicants anatakiwa kulipia shilingi elfu tatu za kitanzania Tsh.3,000 .

Je inamaana RITA kipindi wanampatia mtahiniwa cheti cha kuzaliwa walikuwa hawako makini? Kuna jambo limebadilika? Oky fine tufanye wanahitaji kujiridhisha na uhalali wa taarifa za Mwombaji ,Tsh elfu tatu ya nini? .....Huu siyo ufisadi??

Poleni wadogo zangu kwa kusoma kipindi cha uhakiki na kipindi cha hapa Kazi tu!
 
daaa! hii inakera sn aisee, kila ukifikiri unashindwa kuelewa nn kimebadilika mpaka wanafunzi iwe kazi hv kupata hii mikopo ya serikali, enzi za mkwere mbona haya hayakuwepo pamoja na pesa za serikali kuonekana kutumiwa vibaya mbona watoto walipata mikopo tena kwa mashart ya kawaida kabisa. hapa ngosha hatendi haki kwakwel, yaan amesahau kabisa mishara ya hawa watumishi wake wengi wao haivuki ata kilo 6 kama takehome kitu ambacho huishia kwny kodi ya nyumba na msosi, daa, hatareee sana jaman
 
Mwaka huu kweli masharti ni mengi mpaka napatwa na wasiwasi mkubwa.

Nimejaribu kupitia utaratibu wa utoaji wa mkopo kwa waombaji {Applicants} wa 2018/2019 kuna vigezo ambavyo ninaona hujuma juu ya watoto wa Maskini Kujiunga elimu ya juu {Chuo kikuu}.

Nimesoma kipengele cha sita kinaeleza kuwa mtoto wa mtumishi wa umma {Mtumishi ambae ametajwa kwenye kanuni za utumishi wa umma} mfano Mwalimu,mwanasheria,Muhasibu hatoruhusiwa kuomba mkopo! Yaani haruhusiwi kabisa kuomba maana yake hana vigezo!

Swali la kujiuliza Dogo tu,Asilimia kubwa ya vyuo vyetu Ada zake ni kuanzia 700,000 hapo bado Pesa za
.
~Gharama za chakula na malazi {meals & Accomodation}

~ Gharama za Vitabu na viandikwa {Stationary}

~Mahitaji maalumu ya kitivo..{special faculty}

~Ghrama za utafiti {Research}

Gharama za mafunzo ya vitendo {Field}

Je wazazi hawa amabo wana mshahara amabo haufiki walau Milioni moja. Wanao uwezo wa kuwasomesha hawa watoto wao?? Nafikiri watoto hawa wana hatihati ya kupoteza/Kukosa fursa ya kujiunga na Masomo ya elimu ya juu.

Pia nimeona kigezo cha utoaji kuwa : waombaji/Applicants wamegawanywa katika makundi matatu yaani Ualimu wa sayansi,uhandisi,sayansi ya wanyama.{kundi la kwanza}
Programu za msingi za sayansi,Programu ya sayansi ya Ardhi {kundi la Pili}
.
Kundi la tatu ni sanaa {Maana yake ni non priority} swali langu ni moja tu,,,,Je wanafunzi wanaochukua michepuo ya sanaa kama hawana maana {Serikali haina uhitaji nao} kwa nini wasifute hiyo michepuo? Tunawaruhusu watoto hawa wanasoma harafu mwishoni tunatumia kigezo cha #Uhitaji_na_Programu. This is totally unfair.
.
Ninaamini hapa kwa watoto waliosoma michepuo ya sanaa na ni watoto wa masikini serikali ya awamu ya tano inawapokonya haki yao ya kujiunga na elimu ya juu.{University level}

Mwisho,Nimeona Bodi ya mkopo imetoa Agizo kwa Wakala wa usajili ufilisi na Udhamini {RITA} Kuandaa utaratibu wa uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa/Vifo kwa waombaji upya na kila Mwombaji/Applicants anatakiwa kulipia shilingi elfu tatu za kitanzania Tsh.3,000 .

Je inamaana RITA kipindi wanampatia mtahiniwa cheti cha kuzaliwa walikuwa hawako makini? Kuna jambo limebadilika? Oky fine tufanye wanahitaji kujiridhisha na uhalali wa taarifa za Mwombaji ,Tsh elfu tatu ya nini? .....Huu siyo ufisadi??

Poleni wadogo zangu kwa kusoma kipindi cha uhakiki na kipindi cha hapa Kazi tu!

Mungu wetu uliye juu, tumekukosea nini hadi tuadhibiwe kiasi hiki?
Kama ni mateso yametosha kwa mda wote huu toka 2015,
Kwakuwa wewe ni MUNGU wa wote wenye mwili, tunakuomba tuondolee kikombe hiki kabla ya 2020, naamini umeyaona mateso yetu na kwa uwezo wako utanda sasa na hata milele AMINA
 
Siasa ni njia ya watu wasiokuwa na kanuni kuongoza watu wasiokuwa na kumbukumbu.
 
Na sasa hivi asilimia 15% tunayolipa kila mwezi ni kubwa sana. Hizi pesa wanapeleka wapi..!
 
Nafasi ilikuwa ni tarehe 26 ishapita sasa ni Maumivu mpk Israel atakapotusaidia....na hiyi itakuwa miaka 30 kutoka sasa
 
Hatari Sana, nashukuru Mungu nilisoma kipindi cha JK , kwa hali hii yajayo yanasikitisha sana japo 15% ya makato nayo imeniua kabisa.
 
Mungu wetu uliye juu, tumekukosea nini hadi tuadhibiwe kiasi hiki?
Kama ni mateso yametosha kwa mda wote huu toka 2015,
Kwakuwa wewe ni MUNGU wa wote wenye mwili, tunakuomba tuondolee kikombe hiki kabla ya 2020, naamini umeyaona mateso yetu na kwa uwezo wako utanda sasa na hata milele AMINA
Ameeen,mungu tumuonbe atuondolee hili balaa la duniani na mungu akiamua anafanya.Lamsingi tumuombe.
 
Kinachoumiza ni kwamba watoa maamuzi hayo walisoma bure bila hata kukopeshwa wao ndio wanaleta mazingira magumu kwa wanaokopa...watu weusi wana roho mbaya sana hawataki wenzao wafanikiwe kwa kupitia njia alizopitia yeye...
 
enzi za jk hadi tulikumbushwa kushusha net, msimu huu kila maombi yatatolewa lkn jiwe anakwenda tu.
 
Back
Top Bottom