Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,494
Kwanza nianze kwa kuwatakia Mwaka mpya 2011 uwe wa fanaka na mafanikio. Kwangu Mwaka uliyopita ulikuwa na changamoto nyingi sana ila nashukuru Mungu kwa yote.
Leo nitapenda zungumzia silaha zitumikazo kwenye kuangamiza mahusiano katika ndoa. Urafiki wa kimapenzi hudumu zaidi na kuwa na faraja pale tendo zima takatifu la ndoa linapofanyika kwa maridhiano ya wote. Huleta matatizo iwapo mwanamke anatumia sex kama silaha, siku akichukia basi mnapeana migongo ama mzungu wa nne. Mara nyingi wadada wanaotumia njia hii husababisha wenzi wao kutafuta wagombea wenza. Tendo la ndoa ni muhimu katika kuboresha mahusiano tafiti nyingi zimeonyesha hilo, sitaki kurudia umuhimu wa sex kwenye maisha ya kila siku. Wanawake wanaotumia Ngono kama silaha mara nyingi hawadumu kwenye ndoa zao maana hujifananisha wao na kama chombo cha burudani ambayo anaweza mpatia mteja mwingine.
Ulevi kupindukia, pamoja na kuwa na madhara kiafya pombe husababisha kuyumba kwenye suala zima la ndoa. Wanaume walevi wengi wao wamekuwa hawana uwezo wa kukidhi haja za kingono kwa wenzi wao. Wanawake waliolewa na wanaume walevi wanaongoza kwenye suala zima la cheating, tafiti zinaonyesha hivyo.
Kudumisha ndoa cha muhimu ni kusikilizana na kupeana kile roho na matamanio ya mwili yanachohitaji. Sababu za kichwa kinauma, leo sijisikii ama baba anarudi amelewa kila siku na kuishia lala sebuleni ni hatari sana kwenye ndoa.
The Most Rev Masanilo ni mtafiti huru aliyebobea katika masuala ya Mahusiano, mapenzi na urafiki