dunia ndivyo ilivyo
Member
- Jul 16, 2012
- 72
- 8
kukamatwa nakushitakiwa ponda bado haiwezi saidia kitu.waislam wana madai yao ya msingi kwa serikali.tafakari.
Ukisikia akili ukwaju ndio hizi, wewe kama nani uwapangie maaskofu namna ya kutimiza majukumu yao? ningekuona wa maana kama ungewaambia Waislamu wamsikilize Mufti wao ndio kiongozi rasmi wa Waislamu kuliko huyo muhuni Ponda anayeendesha taasisi ambayo hata haijasajiliwa kwa ajili ya kupata misaada ya waarabu.Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:
Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.
- Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.
- Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya din
- Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.
Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo:
- Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa "mfumo Kristo", na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.
Malasusa na Kundi lake na Maaskofu wa KKKT kulikuwa hakuna haja ya kutaja mambo ya Baba wa Taifa au mabinti wa Nyerere kwani Nchi hii imeshapitia maRais wa3 zaidi na mambo km haya yametokea tukianzia na purukushani za KKKT meru zilizomalizwa na Augustino L. Mrema au ile ya KKKT Same na Mwanga ya Cleopa Msuya hawakumtaja Baba wa Taifa.
- Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania.
Mbona Kilaini alikuwa akibadilika kutokana na hali ya hewa na utawala.
Bado naamini hamjatuliza hizo vuguvugu za Mbagala hasa huyo kijana wa Anglican na vurugu za waislam sanasana mtachochea wakati hapohapo Temeke vurugu za Askofu Mwangwamba tulizisikia
Hivyo kulikuwa hakuna haja ya kutoa tamko lenu tofauti na lile la Askofu wa Anglican kuomba msamaha juu ya kadhia yote ktk Al Jazeera kwani kipengele km hichi Daima tukumbuke kuwa, "KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO" (Waefeso 6: 12).
Mm ni Mtanzania kipindi km hiki muwe na msemaji mmoja la sivyo Maaskofu ni wengi *nimemuona Askofu Shao wa dayosisi ya KKKT Kskz naye katoa yake ktk EATV 5 bado wengi watatoa na yao km wale Viongozi wa Dini waliouunga mkono mgomo wa MaDr na baadaye kuukana Namaanisha kesho sala ya Ijumaa wataingia mitaani sioni umuhimu wa kila mtu kutoa hotuba yake
huyu akifika gerezani wamuwahishe msitu wa MABWEPANDE