Mahojiano ya Dr. Mwakyembe juu ya Madai ya Lowassa...


Hili linchi bana yaani Mtu anatumia ubaya wa Mtu mwingine kudanganya,mhojiwa anampigia simu mhoji kwamba nihoji na MIDANGANYIKA INAKUBALIANA NA UDANGANYIFU HUU.

shame on you......

mix with yours
 
Hakuna kitu hapo,Mahojiano ya kupanga...hiyo ni danganya toto

MSAUZI hivi unamfahamu Mwakyembe vilivyo. Umesikiliza mahojiano yake? Umesikiliza majibu aliyotoa? Nina uhakika hukumsikiliza kwa makini na hivyo hukuelewa. Kama ungeelewa alichosema wala usingeandika hiki ulichoandika hapa.

Kwa taarifa yako Mwakyembe ni mwalimu wa Chuo Kikuu Mlimani. Amesema amefundisha na marehemu aliyeuawa kwa miaka 30. Unatarajia kwa uzoefu wake wa kufundisha miaka 30 ashindwe kujibu maswali madogo hayo?. Kwanza nampa pole kwa kumpoteza mwenzake waliyesoma naye Mirambo na kufanya naye kazi Dar na pia ni wa nyumbani kwao.

MSAUZI unatakiwa uelewe pia kuwa Mwakyembe alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge iliyochunguza Richmond. Yeye na wanakamati wenzake wameshiriki katika kuchunguza na kutoa ripoti ya Richmond. Na kwa kukukumbusha, yeye ndiye aliyewasilisha ripoti ile kwa lugha tamu sana na kwa kujiamini. Dr. Mwakyembe anajua kila kitu kuhusu uchunguzi wa Richmond. Hahitaji kuambiwa majibu. Ukisikiliza mahojiano unaelewa kuwa hawakumhoji Lowasa kwa sababu kadhaa. Hizi sababu walikuwa wanazijua tangu awali.

Ni ajabu kusema kuwa eti ameandaliwa majibu.

Halafu kumbuka kuwa Mwakyembe ni Daktati wa shule. Mwakeymbe siyo Dr. Majimarefu au Dr. Kikwete cheo cha kupachikwa, kuvishwa kilemba cha ukoka. Dr. Mwekyembe siyo Dr. Kikwete wa kutaka sifa asizositahili, aliyeulizwa swali ughaibuni kwa nini nchi yako ni maskini japo ina maliasili nyingi, yeye kaseme sijui. Dr. Mwekyembe anajiamini, ni kati ya watu wachache wa CCM anayejali uhuru wake katika kuishi. Hafungwi na minyoro ya CCM, ameweza kupinga ufisadi bila kutetereka. Dr. Mwakyembe anaamua kuhojiwa na Mwanakijiji, ni wangapi wa CCM wanaoweza kudiriki kuhojiwa JF?.

MSAUZI unatakiwa ufanye tafakuri ya kina kabla ya kuandika. Mwakyembe anauwezo wa hali ya juu wa kupambanua mambo, ni msomi wa kweli, shule imetulia pale. Hongera Mwakyembe kwa kumrudishia Lowasa maji taka yake aendelee kujichafua.
 

Mwakyembe kaombwa afanye mdahalo na mpinzani mmoja kijana.

Akafurahi sana akidai mtu mwenyewe anaijua Kyela kutokea London.

Wengine wanaoweza kuleta upinzani kutokea Tanzania, wakina Mwamunyange, hata hawakuguswa.

Eti mwandishi kasahau.

ndiyo tatizo lako kuassume! mara kwa mara unassume vitu halafu unavifanya viwe kama ndiyo ukweli. Jifunze kuuliza maswali kwanza kabla ya kuassume na kukubaliana na assumptions zako kuwa ni kweli. Kuna mahali nimesema "nimesahau" au unadhania "nimesahau"? Unafikiri kwenye midahalo yote basi wagombea wote wanahusishwa.. ?
 
Swali kako Mwanakijiji,

Mwakyembe kakubali kufanya mdahalo na wapinzani wake, je kina Mwakalinga na wenzake wako tayari?
 
Nimesikiliza mahojiano ya Mwakyembe na M.M nimepata moyo sana kwamba kumbe hakuna haja ya watanzania kukata tamaa, Dr ametupa moyo kwamba sio watanzania wote watumwa na sio wote walionunuliwa.

Hongereni sana sana sana. Naomba tuwe strategic, namuomba Dr Mwakyembe kutumia uanasheria wangu kufanya linalowezekana kwa kutumia mahakama Tido atoke pale kabla ya uchaguzi, tunajua kikwete hana uwezo nalo kwa kuwa huyu bwana aliletwa na Lowassa huyo huyo. Hili ni la muhimu sana katika kupigania demokrasia ya nchi yetu sio tu katika swala la lowassa lakini pia kwa wagombea wote wanaokuja maana ni kituko ndio maana tunaambiwa huko BBC hakujiuzulu alilazimika kwa kuwa mfumo mpya wa organization ulimtoa sababu ya elimu ndogo n.k sasa tunaamini kabisa sasa kama mwenzetu kikwete hawezi kuangalia performance maana Uttoh ameshasema huyu bwana uwezo hana, basi itumike sheria manake sioni MCT, editors forum, TAMWA wala TLHR wakikemea ushenzi huu..

Jamani tuache kubebana kuna watanzania wengi sana wenye uwezo wa kuendesha hivi vyombo kisayansi
 
Swali kako Mwanakijiji,

Mwakyembe kakubali kufanya mdahalo na wapinzani wake, je kina Mwakalinga na wenzake wako tayari?

Mwakalinga alishakubali vile vile.. sasa nipange kuwapata wote wawili tukubaliane utaratibu wa mdahalo wenyewe halafu mambo yatakuwa set.. Halafu nafikiria Ubungo, Bumbuli n.k n.k
 
Kama Tido alimhoji Lowasa kama Waziri mkuu mstaafu, kwa sababu awamu ya kwanza ilikuwa inaishilia, Mwanakijiji amemhoji Mwakyembe kwa lipi? Mi nadhani kuna haja kuchunguza haya mahojianao ya pili kuliko ya kwanza.......Nina wasiwasi na makusudi ya mahojiano ya pili kuliko hata yale ya kwanza!!!!!!!!!!!!!!!! nikiangalia watu wenyewe na uwezo wao naogopa tunkopelekwa sie wadanganyika.....
 
Mi nashangaa sana watu wanaojisafisha kipindi cha kampeni kinapoanza,tu kinapoanza.
 
Nimesikiliza mahojiano ya Mwakyembe na M.M nimepata moyo sana kwamba kumbe hakuna haja ya watanzania kukata tamaa, Dr ametupa moyo kwamba sio watanzania wote watumwa na sio wote walionunuliwa.Hongereni sana sana sana. Naomba tuwe strategic, namuomba Dr Mwakyembe kutumia uanasheria wangu kufanya linalowezekana kwa kutumia mahakama Tido atoke pale kabla ya uchaguzi, tunajua kikwete hana uwezo nalo kwa kuwa huyu bwana aliletwa na Lowassa huyo huyo.

Dr. Mwakyembe anasisitiza watu wasikate tamaa wakati yeye alikata tamaa akaruhusu uozo wa Richmond kuzimwa Bungeni? Nionavyo mimi Mwakyembe sio mpambanaji kwa sababu mpambanaji sikuzote hawezi kuruhusu uozo ndani ya serikali. Angetoka CCM ningempa vote of confidence. Kwa sasa anaendeleza malumbano yasiyo na tija ndani ya jamii
 
Ripoti ya uchunguzi ya bunge haindikwi kama karatasi ya mashitaka ya mahakama. Karatasi ya mashitaka haibebi vidhibiti vyote vya yanayodaiwa kutokea, hayo yatakuja baadae maana hii ni kufungulia shauri tu. Ripoti ya Tume haifuatwi na kesi baadae, yenyewe ndio mwanzo wa yote na mwisho wa yote. Lazima ikamilike.

Mwakyembe anadai hakusema yote dhidi ya Lowassa kwa vile ripoti yao ilikuwa ni kama amemshutumu Mwanakijiji kwa kubaka, halafu Mwanakijiji kakiri kabaka, vidhibiti na ushahidi vya nini tena? Lowassa aliwajika.

Hii ni aibu kubwa, kwamba Mwakyembe msomi wa wasomi wa Tanzania hajui kuwa ripoti inayobeba mapendekezo ni lazima iwe kamili. Kuacha kuweka yote ni sawa na kuandika ripoti ya mauaji ya Kituo cha Biashara cha Dunia halafu usiseme Bin Laden alishiriki vipi kinaga ubaga, alijipenyeza vipi, n.k. eti unasubiri uone kama Bin Laden atabisha ndio uanike mengine.

Usiposema yote kuhusu kisanga kilichofanya utumwe kuandika ripoti, utawezaje kutushauri kwenye ripoti hiyo hiyo jinsi ya kufanya kuepuka majanga hayo mbeleni? Maana hatujui nini kilifanyika. Sijui anaelewa huyu Mwakyembe?
 
Haya ni mahojiano feki.Mshindwe kwa jina ya Yesu..Utupu mtupu

TAFADHALI YESU NI MWANA WA MUNGU MWENYE HAKI KAMWE USIMUUINGIZE KWENYE FIKRA ZAKO ZA KIKONSEVATIVU
Haiitaji degree kujua nani anasema kweli kati ya Mwakyembe na lowasa....mnaomtetea lowasa mnajua mnapata nini ...Yesu hawezi kuwa upande wa watu wanaotafuna nchi kwa gharama ya umaskini wa watz
Mwanakijiji umefanya vema kuleta mahojiano haya hapa hawa mafisadi wasikubabaishe.......UMETENDA JAMBO JEMA NA UNASTAHILI PONGEZI

mix with yours
 
Kwa jina la bwana mlegee na maudanganyifu yenu,watoto wenu wanasoma International school wetu uku Kyela shule za Kata..Mahojiano feki.
 
Wakati mjadala wa richmond unazikwa bungeni Mwakyembe alikuwa wapi? Mbona hakuinuka na kusema hiki hakiwezekani? Je mapendekezo ya kamati yalitekelezwa? Yeye mwenyewe Mwakyembe anajua wazi jinsi suala hilo lilivyo hatari kwake. Si lazima wampige risasi. Lakini wanaweza kumneglect na kumsahau. Cha msingi tuchange karata zetu vizuri, watu wote waelewe ni mabadiliko gani yanahitajika nchini, wampe kura Dr Slaa, basi. Ukiwa ndani ya system ya CCM usije ukadhani kuna uhuru kihivyo my friend.
...fuckken opinions, from a fuckken person!!!
 
Shukrani sana Mwanakijiji kwa kutupatia mahojiano hayo na Mhe. Mwakyembe. Kwa kweli nimepata kufahamu mengi zaidi kuhusiana na suala zima la Richmond.

Mahojiano ni mazuri, yanatosha na yanaonyesha upeo mkubwa wa mhoji na mhojiwa. Ni vyema kuwa yamefanyika kuliko kabla hayajafanyika. Sina uhakika kama unaweza kumhoji na Mhe. Lowassa ili nae aseme anachoweza kusema kuhusiana na suala hili. Na pia sina uhakika kama atavumilia maswali magumu (kama utaweza kuthubutu kuyauliza) ili tupate upande wa pili wa hadithi hii ya Richmond. Naiita hadithi maana pamoja na kila kitu, hakuna hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yake hata kama kuna makosa yaliyofanyika.

Nimejaribu kukumbuka maazimio ya mwisho ya Bunge kuhusu mjadala wa Richmond, nikakumbuka kuwa iliazimiwa kuwa mijadala hiyo iishe. Sasa nini kilichomfanya Mhe. Lowassa kuuanzisha tena?
 
Ripoti ya uchunguzi ya bunge haindikwi kama karatasi ya mashitaka ya mahakama. Karatasi ya mashitaka haibebi vidhibiti vyote vya yanayodaiwa kutokea, hayo yatakuja baadae maana hii ni kufungulia shauri tu. Ripoti ya Tume haifuatwi na kesi baadae, yenyewe ndio mwanzo wa yote na mwisho wa yote. Lazima ikamilike.

Mwakyembe anadai hakusema yote dhidi ya Lowassa kwa vile ripoti yao ilikuwa ni kama amemshutumu Mwanakijiji kwa kubaka, halafu Mwanakijiji kakiri kabaka, vidhibiti na ushahidi vya nini tena? Lowassa aliwajika.

Hii ni aibu kubwa, kwamba Mwakyembe msomi wa wasomi wa Tanzania hajui kuwa ripoti inayobeba mapendekezo ni lazima iwe kamili. Kuacha kuweka yote ni sawa na kuandika ripoti ya mauaji ya Kituo cha Biashara cha Dunia halafu usiseme Bin Laden alishiriki vipi kinaga ubaga, alijipenyeza vipi, n.k. eti unasubiri uone kama Bin Laden atabisha ndio uanike mengine.

Usiposema yote kuhusu kisanga kilichofanya utumwe kuandika ripoti, utawezaje kutushauri kwenye ripoti hiyo hiyo jinsi ya kufanya kuepuka majanga hayo mbeleni? Maana hatujui nini kilifanyika. Sijui anaelewa huyu Mwakyembe?

Mkuu, nadhani Kamati ile ilipewa scope ya kazi. Inategemea na ukubwa wa scope waliopewa katika kufanya uchunguzi huo na hiyo ndiyo dira ya nini wanachoweza ku-report.

Naamini kuwa, katika kutafuta ukweli wa kilichotokea, unakutana na mambo mengi ambayo ni zaidi ya uliyotakiwa kutolea report. Mambo hayo yanaweza kuwa ya msaada tu katika uandaaji na/au utoaji report, bila kuwa na ulazima wa kuwa sehemu ya report yenyewe.
 
Asante mzee Mwanakijiji kwa kujitahidi na kutoa muda wako ili kumtafuta Mh. Mwakyembe ili aongelee kuhusu comments alizotoa Mh. Lowasa...

Lakini Je hiyo uliyofanya ndio inatosha peke yake??? Hapana...nadhani tunahitaji kuenda mbele zaidi na ikiwezekana (naamini inawezekana) Umtafute pia Lowasa umuhoji na yeye kuhusu aliyoongea Mwakyembe kama kweli alionewa kutokana na statements alizotoa Mwakyembe au la...

Pia nadhani hata TBC hasa Tido..wameteleza katika hili kutumia chombo cha umma kumhoji mtu mmoja tena mara mbili kuhusu tuhuma zake...lazima kuna kitu kimefanyika hapa...aidha Lowasa amelazimisha kutumia TBC ili kujisafisha akijiandaa kwenda kugombea tena ubunge jimboni kwake au Tido amepewa kitu ili arushe hayo mahojiano...it is purely non-sense kuhoji upande mmoja.....na kama alichosema Mwakyembe ni sawa basi Lowasa anatapatapa sasahivi, na kama kweli anajiona alikuwa sahihi kufanya alichofanya na alionewa kama alivyodai, basi nadhani waitwe wote na M/kiti wa kamati, na mahojiano yarushwe live!! hapo ndipo tutajua ukweli ni upi...pia awepo Spika Sita.

Asitake kutufanya kuwa sisi ni watoto ambao hatujui anayoyafanya nyuma ya pazia. Kama anasema ameonewa mbona hajaenda mahakamani?? au kwa Tido ndio mahakama yake??
 
..Dr.Mwakyembe aliwahi kusema kwamba kuna mambo ambayo hawakuyaandika ktk ripoti yao ili kukwepa kuiabisha serikali.

..kwa msingi huo naamini kwamba kuna ufisadi mkubwa zaidi ambao Mwakyembe na timu yake waliamua kwa makusudi kabisa kuyaficha.

..sasa ni ufisadi upi ambao Mwakyembe aliamua kuuficha? je ni mafisadi gani ambao Mwakyembe aliamua kuwasitiri?
 
JokaKuu... ni lazima tukumbuke kuwa Lowassa alijiuzulu kuzuia huko unakotaka kwenda. Asingeweza kupinga Bungeni na kusema yote yaliyosema hayakuwa kweli kwani hapo ushahidi zaidi ungetakiwa kutolewa. Lakini kwa vile wahusika wakubwa walikubali kuwajibishwa utoana ile haja ya kwenda huko mbele zaidi ilipotea. Ndio maana bado anashauriwa kuwa kama hakutendewa haki aende mahakamani au kufungua kesi ya madai au wherever other discourse ambayo anafikiri anayo.
 
Back
Top Bottom