Mahanga alikimbia na kura!!!

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
: Mahanga alikamatwa na masanduku ya kura Send to a friend

SHAHIDI wa tisa katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Segerea, Aziza Masoud (25) ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk Makongoro Mahanga alikamatwa na masanduku ya kura.

Masoud ambaye ni Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi, alidai hayo jana kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Profesa Ibrahim Juma, akiongozwa na wakili Peter Kibatala anayemtetea Mpendazoe.

Kesi namba 98 ya mwaka 2011, ilifunguliwa na Mpendazoe aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chadema, akipinga ushindi wa Dk Mahanga katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Katika ushahidi wake jana Masoud alidai kuwa Dk Mahanga alikamatwa wakati akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea na walipata taarifa za kukamatwa kwake kupitia kwa baadhi ya mawakala waliokuwa wakishiriki katika uchaguzi huo katika jimbo hilo.

Alidai kuwa Novemba Mosi mwaka 2010 Msimaizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo katika Manispaa ya Ialala, Gabriel Fuime alithibitisha kukamatwa kwa mgombea huyo na kwamba tayari alishapeleka taarifa hizo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

"Katika mkutano wa wandishi wa habari ulioitishwa na Fuime kuna mwandishi aliomuuliza kuhusu suala hili, Fuime alikiri kuwa na taarifa hizo na alisema kwamba yeye hawezi kulishughulikia suala hilo bali atalipeleka NEC na atatoa majibu kwa wagomea,"alidai Masoud.

Aliendelea kudai kuwa baada ya msimamizi huyo wa uchaguizi kukiri kupata taarifa hizo aliandika habari iliyotoka katika gazeti la Mwananchi Novemba 2, 2010.

Hata hivyo Maosud alidai kuwa katika habari hiyo, hakumtaja kwa jina mgombe huyo aliyekamatwa na masanduku wala cheo chake licha ya kutajiwa na vyanzo vya vyake vya habari.

Alidai kuwa kuandika taarifa hiyo hakukumletea matatizo ama vitisho ingawa aliwahi kusikia ofisini kwake kuwa kuna baadhi ya watu waliopiga simu kuhoji kuhusu habari hiyo.

Aliongeza kuwa yeye binafsi wala gazeti lake hawajawahi kushtakiwa mahali popote kutokana na kuandika au kuchapisha habari hiyo.

"Hatujawahi kushtakiwa au kufikishwa mahakamani kwa kum-quote (kumnukuu) Fuime katika stori hiyo, sisi tuna utaratibu wa kutoa taarifa kwa jamii , hatuogopi ikiwa habari husika ina maslahi kwa jamii,"alidai.
Katika kesi hiyo Mpendazoe analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi katika jimbo hilo akida taratibu na sheria za uchaguzi zilikiukwa katika ukusanyaji ujumulishaji na utaratibu wa kuhesabu na utangazaji wa matokeo.

Hivyo anaiomba Mahakama hiyo itengue matokeo ya ushindi wa mbunge aliyetangazwa na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo, au yeye atangazwea mshindi.Kesi hiyo itaendelea tena leo mahakamani hapo ambapo mashahidi wa upande wa madai wataendelea kutoa ushahidi.

 
Mungu msaidie mpendazoe ili 2ongeze nguvu bungeni ya kupinga udhalimu wa serikali ya ccm kwa wananchi.
 
Hata mimi nikiitwa nitatoa ushahidi kuwa nilisikia habarai za Mahanga alishikwa na masanduku ya kura..

Na kwa kuwa tusivyo na Raisi Makini akamteua mwizi wa kura mwenzake kuwa naibu waziri huu ni uchafu kuliko Yale yatokayo kwenye Masabur....

Nyerere alisema watu kama hawa waingiao Ikulu kwa njia za Panya au wanakopa pesa nyingi wapate madaraka je Watazilipaje hizo pesa ....

Za Mwizi 40 ila Mahanga akipona basi zake zitakuwa zaidi ya 40...

Kikwete naye Afunguliwe kesi
 
so what??

mwendelezo wa story, mdau mwenza wa Chenge,Malima pamoja na Nyarandu na ccmagamba wengineyo.Kabla ya kutokea 12 mwaka wazir kumilik ak47. eeh ccm wazee wa totos du hamjiamin nini hadi mtembee na silaha kubwa!Kweli kuwa ccm uwe na akil kama nyegere(mnyama mwenye wivu).wazir bunduki mbunge nae bastola yaelekea rais wenu ana mabomu, woga wa nn?uroda wa ukubwa taabu tupu
 
huyu baba ma CD wanamsifia kwamba ananyonya kule chini balaa. Yaani yeye Adam Malima #2

hahaha! hao nndo wanaitwa viongozi wetu tunaowaiba kwenye wimbo wa taifa mungu awabariki!!!! labda ndo maana hizo dua zetu hazisikiki manake matendo yao laaaana tupu!
 
so what??
So what? what?

Hana Maadili ya kushika nafasi yoyote ya Uongozi katika Jamii yetu. Unafikiri anatoa Picha Gani kwa Vijana wetu. Zaidi ni kwamba alitakiwa kuwa chachu ya kuhakikisha hao wadada wanaweza kufanya kazi za kistaarabu ni kuhifadhi utamu wao kwa ajili ya matumizi ya nyumbani (approved Family - Mke na Mme)

Unakuja kuuliza so what hapa. unafikiria wewe??
 
mwendelezo wa story, mdau mwenza wa Chenge,Malima pamoja na Nyarandu na ccmagamba wengineyo.Kabla ya kutokea 12 mwaka wazir kumilik ak47. eeh ccm wazee wa totos du hamjiamin nini hadi mtembee na silaha kubwa!Kweli kuwa ccm uwe na akil kama nyegere(mnyama mwenye wivu).wazir bunduki mbunge nae bastola yaelekea rais wenu ana mabomu, woga wa nn?uroda wa ukubwa taabu tupu

aisee umenichekesha sana yaani mkuu wao atakuwa na magrenade hahaha
 
Ikishafika Judgement nadhani Judge atawasiliana na JK kwanza then asbh mtashangaa Mpendazoe kashindwa kesi.Ninachofahamu ni JK alimwelekeza Fuime kumtangaza Makongoro licha ya kushindwa kura. Fuime alikuwa na wakati mgumu sana that time kabla ya kutangaza, nafsi ilimtuma amtangaze mshindi wa kweli Fred,maelekezo ya juu yakamtaka tofauti,nilikuwa pale Manispaa
 
Mzazi,Mpendazoe kaa mkao wa Kampeni hii ngoma ishalala,japokuwa huyo Jaji Juma ni mtu wa JK mwanzo mwisho alipokuwa Dean Facult of Law UDSM alimbeba sana Ridhiwani maana dogo alidisco........................do JK akampa mtu mzima zawadi ya Ujaji.
 
Hukumu ya kesi hii itakuwa kipimo kizuri cha utendaji haki wa mahakama zetu bila shinikizo kutoka muhimili mwingine.
 
huyu baba ma CD wanamsifia kwamba ananyonya kule chini balaa. Yaani yeye Adam Malima #2

Ingawa haya ni mambo binafsi yasiyohisiana na kazi ikingatiwa kuwa anayafanya usiku, lakini ukishakuwa Kiongozi unatakiwa kuwa makini na mwenendo wa maisha yako.
 
Back
Top Bottom