Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
TAMKO KUHUSU HUKUMU ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA RUFAA KUHUSU MGOMBEA BINAFSI TANZANIA .
Tumepokea kwa mshituko mkubwa Hukumu iliyotolewa na Mahakama Ya Rufani Tanzania iliyosomwa leo na Jopo la Majaji saba na kuamua kutupilia mbali Hukumu iliyokuwa imetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu uwepo wa Mgombea Binafsi .
Mambo makuu matatu ya msingi hayakuzingatiwa na jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani katika kutoa uamuzi wao ambayo ni;
Kwanza, Mahakama ya Rufani kwenye Hukumu hii imeamua ama kujisahau au kwa makusudi kabisa kuacha jukumu lake la kulinda Haki za Binadamu (Has aveded its duty as a custodian of Human Rights ).
Pili , haya ni maamuzi yenye msukumo wa Kisiasa zaidi na hayakuzingatia misingi ya Katiba , Sheria na Kanuni .
Tatu ,Mahakama ya Rufani imetoa Hukumu bila kufuata misingi Haki.
Kwa maoni yetu , ni Hukumu ambayo itaendelea kuuwa Demokrasia nchini Tanzania na ni jukumu la kila mpenda Demokrasia kuhakikisha kwamba anaipinga hukumu hii kwani imetolewa kwa misingi ya kisiasa zaidi na kulinda kikundi cha watawala .
Mahakama ya Rufani imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kutafsiri Katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,na kuliachia jukumu hilo kwa chombo kingine ambacho kimsingi sio kazi yake kutafsiri sheria bali kazi ya Bunge ni kutunga sheria.
Taarifa zaidi ya kina itatolewa pindi tutakapo pata nakala ya hukumu husika.
Imetolewa na Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri.
John Mrema .
17/06/2010.