Mahakama yatupa hoja za serikali; Bunge laachiwa

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

TAMKO KUHUSU HUKUMU ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA RUFAA KUHUSU MGOMBEA BINAFSI TANZANIA .

Tumepokea kwa mshituko mkubwa Hukumu iliyotolewa na Mahakama Ya Rufani Tanzania iliyosomwa leo na Jopo la Majaji saba na kuamua kutupilia mbali Hukumu iliyokuwa imetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu uwepo wa Mgombea Binafsi .

Mambo makuu matatu ya msingi hayakuzingatiwa na jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani katika kutoa uamuzi wao ambayo ni;

Kwanza, Mahakama ya Rufani kwenye Hukumu hii imeamua ama kujisahau au kwa makusudi kabisa kuacha jukumu lake la kulinda Haki za Binadamu (Has aveded its duty as a custodian of Human Rights ).

Pili , haya ni maamuzi yenye msukumo wa Kisiasa zaidi na hayakuzingatia misingi ya Katiba , Sheria na Kanuni .

Tatu ,Mahakama ya Rufani imetoa Hukumu bila kufuata misingi Haki.

Kwa maoni yetu , ni Hukumu ambayo itaendelea kuuwa Demokrasia nchini Tanzania na ni jukumu la kila mpenda Demokrasia kuhakikisha kwamba anaipinga hukumu hii kwani imetolewa kwa misingi ya kisiasa zaidi na kulinda kikundi cha watawala .

Mahakama ya Rufani imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kutafsiri Katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,na kuliachia jukumu hilo kwa chombo kingine ambacho kimsingi sio kazi yake kutafsiri sheria bali kazi ya Bunge ni kutunga sheria.

Taarifa zaidi ya kina itatolewa pindi tutakapo pata nakala ya hukumu husika.

Imetolewa na Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri.
John Mrema .
17/06/2010.
 
Jaribu kufikiria scenario hii: Mahakama inaruhusu mgombea binafsi, Mtikila anatafuta mchungaji mwenzake ama mfuai mwenzake wa siasa za chuki dhidi ya wazanzibari, waasia, waislamu, wageni wengine na hata watanzania waishio mipakani ambao kwa mujibu wake sio watanzania wa kweli halafu wanakuwa wagombea binafsi katika uchaguzi ujao wa urais dhidi ya yule ambaye Mtikila tayari ameshasema kuwa ni gaidi na ana ajenda ya kuumaliza ukristo hapa nchini. Fikiria aina ya Tanzania tutakayokuwa nayo wakati na baada ya uchaguzi huo........

.... You have a Big Point there, Brother. Much as I may hate the Court of Apeal's Judgment, I am being honest to myself by asking myself...Ni lipi jipya na la maana tunalotegemea kupata kutokana na kuwa na Mgombea binafsi ambalo hatukulipata kutokana na Kuwa na mfumo wa Vyama Vingi kwa zaidi ya Miaka Kumi na Tano Sasa...? ? ? ? ?
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

TAMKO KUHUSU HUKUMU ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA RUFAA KUHUSU MGOMBEA BINAFSI TANZANIA .

Tumepokea kwa mshituko mkubwa Hukumu iliyotolewa na Mahakama Ya Rufani Tanzania iliyosomwa leo na Jopo la Majaji saba na kuamua kutupilia mbali Hukumu iliyokuwa imetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu uwepo wa Mgombea Binafsi .

Mambo makuu matatu ya msingi hayakuzingatiwa na jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani katika kutoa uamuzi wao ambayo ni;

Kwanza, Mahakama ya Rufani kwenye Hukumu hii imeamua ama kujisahau au kwa makusudi kabisa kuacha jukumu lake la kulinda Haki za Binadamu (Has aveded its duty as a custodian of Human Rights ).

Pili , haya ni maamuzi yenye msukumo wa Kisiasa zaidi na hayakuzingatia misingi ya Katiba , Sheria na Kanuni .

Tatu ,Mahakama ya Rufani imetoa Hukumu bila kufuata misingi Haki.

Kwa maoni yetu , ni Hukumu ambayo itaendelea kuuwa Demokrasia nchini Tanzania na ni jukumu la kila mpenda Demokrasia kuhakikisha kwamba anaipinga hukumu hii kwani imetolewa kwa misingi ya kisiasa zaidi na kulinda kikundi cha watawala .

Mahakama ya Rufani imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kutafsiri Katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,na kuliachia jukumu hilo kwa chombo kingine ambacho kimsingi sio kazi yake kutafsiri sheria bali kazi ya Bunge ni kutunga sheria.

Taarifa zaidi ya kina itatolewa pindi tutakapo pata nakala ya hukumu husika.

Imetolewa na Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri.
John Mrema .
17/06/2010.
Sasa mwanakijiji, huyu naye mbona hoja zake zinaelea hewani? Sasa hoja tatu zote hazina supporting evidence. Kwanini anasema mahakama haikufuata misingi ya haki, kwanini anasema haki za binadamu hazikuzingatiwa. Mtoa tamko naye amekurupuka bwana. Nilitegemea angekuja na hoja makini za kubeza baadhi ya vifungu vilivyokiukwa. Sasa story za aina hii si yeyote tu anaandika?
 
Ebu niwaulizeni mnaotaka hii sheria ya mgombea binafsi...
Tuseme mathlan sheria hii ingepitishwa... Na wananchi elfu, laki au millioni uwezo wa kupiga kura wakiamua wao kujiandikisha kama wagombea Binafsi - itakuwaje?..
Maanake sheria mnayoitaka inaruhusu mgombea binafsi na sidhani kama kuna kiwango cha haki kwa idadi ya wagombea wala kukataza wengine wasifanye hivyo..Ni wapi kikomo wa hiyo haki ya mgombea binafsi kwa wananchi wake kwa sababu huwezi sema baadhi ya watu tu ndio wanaruhusiwa wengine wakae pembeni..Je, gharama zake pia zitachukuliwa na nani?..

Kwani Malawi, Zambia n.k inakuwaje?? Sijasika wagombe 2000 kenye kiti kimmoja. Sasa kama wenzetu wanaweza kwa nini TZ tusiweze??? I am fail to understand how people can support such judgment!!!
 
Mkandara,

Jibu lako ni dogo sana. Kwa nchi zinavyofanya hivyo, basi huwa wana utaratibu kama uliopo leo kuandikisha vyama Tanzania. Ili uwe na chama, kuna idadi minimum ya wanachama ambao inabidi uwe nao (CJJ wanahaha na hilo sasa). Na hawa ndiyo inakuwa kama dhamana ya wabunge na wagombea urais kupitia chama hicho. Sasa kama ni mgombea wa Rais, inaweza kuwekwa idadi hiyohiyo ya wanachama ambao mgombea anatakiwa kuwa nayo au tuseme minimum Watanzania laki moja wamdhamini.

Ila inapokuja kwenye ubunge, wanaweza kusema kwa mfano elfu 20 tu na mtu unagombea kama mwanachama wa kujitegemea. Faida kubwa ya ubunge wa KUJITEGEMEA huwa ni ule uhuru wa KUTOKA mara pale ukiona chama chako hakina adabu. Hii ya kuwafunga WABUNGE ndani ya chama kwa kuogopa kuwa akifukuzwa basi na ubunge anakosa, inatufanya kuwa wabunge KUNGURU kama wabunge wengi wa CCM leo Tanzania ambao wamefanywa kama mhuli wa kupitishia mamboa ya hao wachache washika nchi.

Mnafanya makosa sana kuliangalia hili katika ngazi ya RAIS tu. Sidhani kama leo kuna mtu atashinda URAIS bila ya kuwa na chama ila kwenye UBUNGE hilo linawezekana kabisa na pia WABUNGE wanaweza kujitoa ndani ya CCM na kwenda chama cha upinzani pale wakiona mambo yanakwenda mrama. Ila nyie mnaona ni RAIS tu ndiyo anaongelewa hapa.

Hii hukumu ni sawa na UPUUZI wa KAITA wa Nigeria leo. Watanzania inabidi tuikumbuke hii siku. Ngoja tuone na kuisoma hukumu yenyewe.

Ebu niwaulizeni mnaotaka hii sheria ya mgombea binafsi...
Tuseme mathlan sheria hii ingepitishwa... Na wananchi elfu, laki au millioni uwezo wa kupiga kura wakiamua wao kujiandikisha kama wagombea Binafsi - itakuwaje?..
Maanake sheria mnayoitaka inaruhusu mgombea binafsi na sidhani kama kuna kiwango cha haki kwa idadi ya wagombea wala kukataza wengine wasifanye hivyo..Ni wapi kikomo wa hiyo haki ya mgombea binafsi kwa wananchi wake kwa sababu huwezi sema baadhi ya watu tu ndio wanaruhusiwa wengine wakae pembeni..Je, gharama zake pia zitachukuliwa na nani?..
 
Jaribu kufikiria scenario hii: Mahakama inaruhusu mgombea binafsi, Mtikila anatafuta mchungaji mwenzake ama mfuai mwenzake wa siasa za chuki dhidi ya wazanzibari, waasia, waislamu, wageni wengine na hata watanzania waishio mipakani ambao kwa mujibu wake sio watanzania wa kweli halafu wanakuwa wagombea binafsi katika uchaguzi ujao wa urais dhidi ya yule ambaye Mtikila tayari ameshasema kuwa ni gaidi na ana ajenda ya kuumaliza ukristo hapa nchini. Fikiria aina ya Tanzania tutakayokuwa nayo wakati na baada ya uchaguzi huo........

Siamini kama kweli siasa za Mtikila zinaweza kufanya suala zima la mgombea huru kuwa baya. Suala la mgombea binafsi ni mwiba kwa wanaoimiliki CCM na wanaoila Tanzania, once CCM ikisambaratika hakutakuwa na wizi wa pamoja na kulindana, wanaojua dhuluma tunayofanyiwa watanzania wako ndani ya CCM, wakitoka hao ndio tutakuwa na ahueni.

Hukumu hii wenye akili wanajua si nzuri kwa Tanzania, lakini ni muhimu sana kwa kundi la wanaoimiliki CCM, wanajua kama sheria ingefuatwa na haki kutendeka hatma ingekuwa nini kwa wao. Lakini safari haijafika mwisho, wakifunga mlango mmoja mwingine utakuwa wazi. Mnakumbuka wazi jinsi mahakama hii ilivyoendesha kesi ya mauaji ya Dito, did you expect anything different? you were dreaming.
 
Kama nilivyokuwa ninafikiri hukumu yenyewe inaonesha hoja zote za msingi zilizotolewa na serikali dhidi ya Mtikila zimetupwa na Mahakama ya Rufani kwa mtiririko ule ule wa hoja niliokuwa nautetea. Waliotupa taarifa kuwa Mtikila kashindwa rufaa nadhani hawakusikiliza mtiririko wa hukuu. Mtikila kashinda kwa kiasi kikubwa saaaaana!!
 
siyo siambiliki nimeisoma hukumu nzima na iko wazi sana.. serikali imepoteza karibu hoja zake zote isipokuwa moja tu ambayo nayo imepewa kama ushindi wa mezani..
 
Sasa mwanakijiji, huyu naye mbona hoja zake zinaelea hewani? Sasa hoja tatu zote hazina supporting evidence. Kwanini anasema mahakama haikufuata misingi ya haki, kwanini anasema haki za binadamu hazikuzingatiwa. Mtoa tamko naye amekurupuka bwana. Nilitegemea angekuja na hoja makini za kubeza baadhi ya vifungu vilivyokiukwa. Sasa story za aina hii si yeyote tu anaandika?

Umeambiwa taarifaya kina itatolewa baada ya kupata na kusoma hukumu yenyewe??? Vipi? umetumwa??
 
Umeambiwa taarifaya kina itatolewa baada ya kupata na kusoma hukumu yenyewe??? Vipi? umetumwa??
Sasa kwanini ametoa tamko wakati hukumu yenyewe hajaisoma? Umeona hoja zilizojengwa na Mwanakijiji? Hilo ndo tulitaka tulisikie kutoka kwake aliyetoa tamko, kwamba hoja zote za serikali zimetupwa, sasa iweje serikali ishinde? Mimi ni mmojawapo ambaye nimeumizwa na hukumu hii, kwahiyo ningependa kuona anayetoa tamko anatoa kwa kujenga hoja ili tujue tumehujumiwa au ndo sheria ya nchi yetu ilivyo? Hizi kelele za laymen wa sheria hazitusaidii.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

TAMKO KUHUSU HUKUMU ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA RUFAA KUHUSU MGOMBEA BINAFSI TANZANIA .

Tumepokea kwa mshituko mkubwa Hukumu iliyotolewa na Mahakama Ya Rufani Tanzania iliyosomwa leo na Jopo la Majaji saba na kuamua kutupilia mbali Hukumu iliyokuwa imetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu uwepo wa Mgombea Binafsi .

Mambo makuu matatu ya msingi hayakuzingatiwa na jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani katika kutoa uamuzi wao ambayo ni;

Kwanza, Mahakama ya Rufani kwenye Hukumu hii imeamua ama kujisahau au kwa makusudi kabisa kuacha jukumu lake la kulinda Haki za Binadamu (Has aveded its duty as a custodian of Human Rights ).

Pili , haya ni maamuzi yenye msukumo wa Kisiasa zaidi na hayakuzingatia misingi ya Katiba , Sheria na Kanuni .

Tatu ,Mahakama ya Rufani imetoa Hukumu bila kufuata misingi Haki.

Kwa maoni yetu , ni Hukumu ambayo itaendelea kuuwa Demokrasia nchini Tanzania na ni jukumu la kila mpenda Demokrasia kuhakikisha kwamba anaipinga hukumu hii kwani imetolewa kwa misingi ya kisiasa zaidi na kulinda kikundi cha watawala .

Mahakama ya Rufani imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kutafsiri Katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,na kuliachia jukumu hilo kwa chombo kingine ambacho kimsingi sio kazi yake kutafsiri sheria bali kazi ya Bunge ni kutunga sheria.

Taarifa zaidi ya kina itatolewa pindi tutakapo pata nakala ya hukumu husika.

Imetolewa na Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri.

John Mrema .

17/06/2010.

Kweli tunavyama kweli!!! sasa haki ya watu wa Tanzania inatokana na katiba ya Tanzania... sio katiba ya Malawi au Zimbabwe... Chama Cha Mendeleo Makini.. .Du! Kazi ipo Tanzania.

Chama Makini kinasema hakijapata hukumu lakini kimeshatoa msimamo.. inaonyesha kinaongozwa na hisaia
 
mahakama ya rufani yaitolea nje hoja ya mtikila (Kutoka kwa Michuzi)

Na Ripota wa Mahakama
wa Globu ya Jamii
Hatima ya kuwapo au kutokuwapo kwa mgombe binafsi nchini, imebakia mikononi mwa bunge baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kubainisha kuwa suala hilo linapaswa kuamuliwa na Bunge na si Mahakama.

Maamuzi hayo ambayo ni ya Jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufani Tanzania, likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Augustino Ramadhani yametengua uamuzi wa kuwapo kwa mgombea binafsi nchini ambao ulitolewa hapo awali na mahakama kuu, baada ya kukubaliana na hoja za Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikil, zilizotaka kuwapo kwa mgombea binafsi nchini.

Jaji Ramadhani asubuhi ya leo alisoma hukumu dhidi ya kesi hiyo, hukumu ambayo imeufuta uamuzi wa kuwapo kwa mgombewa binafsi hivyo kurudisha suala hilo bungeni.

Katika maamuzi ya jopo hilo kuhusiana na rufani hiyo iliyofunguliwa na Serikali, mahakama hiyo imesema kuwa hoja ya mgombea binafsi ni ya kisiasa zaidi na si sheria.

Jaji Ramadhani alisema kuwa kutokana na ukweli huo, mahakama kama makahakama inasimamia sheria hivyo haiwezi kutolea maamuzi suala hilo ambalo kwa upande
mwingine linagusa katiba.

Aliongeza kuwa Bunge ndilo lenye mamlaka ya kufanya marekebisho ya kikatiba, hivyo iwapo katiba itakuwa inahitaji marekebisho inawajibika kufanya hivyo.

Kutokana na hilo, Jaji Mkuu amesema kuwa mahakama haina mamlaka ya kutengua kilichopo katika katikba, hivyo sula la mgombea binafsi linafaa kushughurikiwa na bunge.

Lakini kwa upande wa Mch. Mtikila ambaye alifika mahakamani hapo kusikiliza uamuzi huo, akiwa nje ya mahakama aliifanananisha hukumu hiyo na hukumu ya kisiasa na kusema kuwa haikuwa ya kisheria.

Akizungumza na wanahabari, Mtikila alisema kwamba mahakama hiyo hakikutenda haki na kwamba maamuzi ya mwanzo ya kuruhusu mgombea binafsi ndio yaliyokuwa ya haki.

Awali katika rufani hiyo Serikali ilidai kuwa Mahakama Kuu ilikosea kwa kujipa mamlaka ya kutoa uamuzi wa kuwapo kwa mgombea binafsi nchini.

Katika hilo Serikali ilidai kuwa mahakama kuu ilifanya makosa kwa kujipa mamlaka yakutengua vifungu vya katiba ya nchi.

Mbali na sababu hiyo Serikali ilidai kuwa mahakama hiyo ilijipachika mamlaka ya kibunge ya kutunga sheria.

Hiyo ni ilikuwa ni Rufani ya pili kufunguliwa na serikali kuhusiana na hoja hiyo ya mgombea bianafsi, kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2007 Serikali ilikata rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ikidai kuwa mahakama hiyo ilikosea kisheria kutafsiri ibara ya 21(1)(c), 39(1)(c) (b) na 69(1)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini rufani hiyo ya mwanzo ilitupwa na Mahakama ya Rufani, baada ya mahakama hiyo kukubaliana na hoja ya kuwapo kwa mgombea binafsi.

Mei 2006, mahakama Kuu ilitoa maamuzi ya kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi ambapo mahakama hiyo ilisema kuwa maamuzi hayo yanatokana na katiba ya nchi ambayo inatoa haki hiyo.

Maamuzi hayo yaliweka wazi kuwa kila mwananchi ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Pia maamuzi hayo yalibahinisha kuwa Katiba haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mtu kujiunga na chama fulani na kwamba hilo limewekwa wazi katika katiba.

Kwa mara ya kwanza Mtikila aliwahi kushinda kesi kama hiyo mnamo mwaka 1993, ushindi ambao ulitokana na maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Pamoja na maamuzi hayo yaliyomfanya Mtikila kuibuka kidedea, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi.
 
Si alishatamka waziri Marmo kwamba hakuna mgombea binafsi. CJ na jopo lake wamepiga mhuri tu amri ya waziri! LONG LIVE TANZANIA AND ITS POLITICS!!!!!!!

Mkuu ZM, uliandika vizuri sana siku chache zilizopita katika uchambuzi wako wa kutabiri hukumu kuhusu swala hili na utabiri wako umekuwa 100% accurate.
 
Sasa kwanini ametoa tamko wakati hukumu yenyewe hajaisoma? Umeona hoja zilizojengwa na Mwanakijiji? Hilo ndo tulitaka tulisikie kutoka kwake aliyetoa tamko, kwamba hoja zote za serikali zimetupwa, sasa iweje serikali ishinde? Mimi ni mmojawapo ambaye nimeumizwa na hukumu hii, kwahiyo ningependa kuona anayetoa tamko anatoa kwa kujenga hoja ili tujue tumehujumiwa au ndo sheria ya nchi yetu ilivyo? Hizi kelele za laymen wa sheria hazitusaidii.
Shida ni uvivu wakusoma tu posts. Ukipitia kila post vizuri hapa utaelewa nini MMKJJ anasema. Wengi mnaanzia kusoma posts katikati na mnaanza kutoa comments za aibu. Nenda jukwaa la sheria kuna hukumu ya leo pale. Download na ujisomee usimsumbue mmkujj kwa vihoja dhaifu vyako.
 
wabongo tuna matatizo; hukumu ipo kwenye thread nyingine hapo na inaonesha kuwa serikali kati ya hoja zake zote imepoteza zote na mahakama imeliachia suala hilo kwa Bunge kama Mahakama Kuu. Someni basi hukumu msiseme tu kuwa Mahakama imetumiwa na serikali.. wakati hoja zote za serikali zimetupwa mbali kabisa!!!

Au ndio huu uvivu wa kusoma unatusumbua maana haikuandikwa kwa maandishi ya madaktari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom