Mahakama yatupa hoja za serikali; Bunge laachiwa

Mhhhhh! bora tuiite tu Mahakama ya CCM maana iko pale kulinda maslahi ya chama twawala badala ya yale ya Watanzania.
 
Mhhhhh! bora tuiite tu Mahakama ya CCM maana iko pale kulinda maslahi ya chama twawala badala ya yale ya Watanzania.
kweli Tanzania hatuna mahakama, sijuii tuta tokea wapi, wasomi wetu nao ni washirikina, viongozi wetu ndio hao hao wanatuuza kama watumwa na kujiuza wenyewe kwa mafisadi, mwisho wa siku kuna siku watakula wenyewe kwa wenyewe ndio hapo uasikia mbona kijiji kwetu au watu wangu hawapati kazi wa mwingine wanapata zaidi etc etc , kumbe matatizo tunajitafutia wenyewe kwa kuendekeza ujinga kama huu.
 
Alaaah!
Sasa nimepata majibu ya maswali yangu,
Ndio maana hawataki CCJ isajiliwe.
Wanahakikisha kila upenyo umezibwa.
Ila wanasahau kitu kimoja
"sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU, maamuzi ya wengi ndio sheria"

Pakacha litavuja tuu,
veeery soon.
Inshallah!
 
DAH ebwanaee uje hii kitu ni lazima ingepindishwa sababu kama mtikila angeshinda ina maana mwaka huu kusingekua na uchaguzi mkuu na serikali tayari imeshatumia fedha nyingi.Kwa kweli inasikitisha lakini ndio Tanzania hiyo bwana hakuna haki kabisa.Haki ipo mbinguni tu.Ngoja tumsiklizie mtikila atakuja na mpya gani
 
kweli Tanzania hatuna mahakama, sijuii tuta tokea wapi, wasomi wetu nao ni washirikina, viongozi wetu ndio hao hao wanatuuza kama watumwa na kujiuza wenyewe kwa mafisadi, mwisho wa siku kuna siku watakula wenyewe kwa wenyewe ndio hapo uasikia mbona kijiji kwetu au watu wangu hawapati kazi wa mwingine wanapata zaidi etc etc , kumbe matatizo tunajitafutia wenyewe kwa kuendekeza ujinga kama huu.

Labda mahakama ya Kadhi itakuwa ya haki!Wenzetu mnaoaka hiyo mahakama tupeni dondoo ili nasi tuisimamie ipitishwe na ccm!
 
Sasa ndio maana ya kukosa uzalendo, hawa majaji hawajui hata kazi yaoooooo, jamani nini hakieleweki? baba wa taigfa alisema hakuna tabu kwa mgombea binafsi, sasa JK waogopa nini?, maana naona mwatumia nguvu mpaka kuwaghalilisha majaji wanatuoa jugment za ajabu ajabu, ebu watanzania tuamke hawa CCM ni wanacha 3,000,000 tu na maamuzi haya makubwa ya nchi wanafanya CC ambao wako 36 tu, sasa hawa ndio wanatupeleka? mwenye jukumu la kutetea natioal interst ni TISS au UWT, sasa nayo yapo kana ni mgambo tu wa CCM, maana huwezi sema ni walinzi wa viongozi amboa wanashindwa amgalia mali ya hiyo CCM yenyewe,
 
Naunga mkono uamuzi wa wa mahakama kuu na pia ya rufaa kwani wametekeleza wajibu wao kikatiba bila kuyumbishwa na siasa za njia za mkato. Nikiangalia hali ya kisiasa na kijamii hivi sasa nchini mwetu naanza kutambua umakini wa CCM kufanya ujanja wa kikatiba na kubinya haki hiyo ya kimsingi. Tanzania ya sasa inapaswa kuepuka kuruhusu wanasiasa wajanjawajanja walio tayari kuvunja misingi ili kufanikisha ajenda zao---populists. Naamini kuwa Mgombea binafsi hasa katika nafasi ya Urais itageuka kuwa platform of irresponsible and un-principled opputunists to light the flames of national devide and hatred. Napendekeza katiba ibadilishwe baada ya uchaguzi ujao na kuruhusu mgombea binafsi katika ngazi za serikali za mitaa halafu baadaye turuhusu udiwani na ubunge kabla ya kuruhusu urais. Watanzania tumethibitisha kuwa inapokuja katika mabadiliko tunakuwa malimbukeni mno kiasi ya kugeuza mabadiliko hayo kuwa mzigo na nafasi ya kufakamia siasa za ujanjujanja badala ya nafasi ya kuleta mabadiliko makini. Wengi wetu tunapenda kuona mgombea binafsi anaruhusiwa sio kwa kuwa tunamini hilo litasaidia kujenga taifa bora lakini kwa kuwa tumeshindwa kuondoa siasa hovyohovyo katika vyama tulivyomo ama tungelipenda tuwemo. Ukweli ni kuwa vyama vya siasa vina role ya kuwa SPEED GOVERNORS za irresponsible politics ambazo zimekuwa zikiota mizizi katika nchi yetu. Kuruhusu mgombea mwenza kwa SASA ni hatari kwa taifa letu. Haswa wakati kama huu ambako bado hatujafanikiwa kujenga mfumo bora/asasi za kuweza kudhibiti populist, irresponsible and oppurtunistic politicians walio tayari kutumia ajenda zozote zile ili wafanikiwe kuwaghilibu watanzania katika kufanikisha matakwa yao.
 
Mimi naona siyo Mtikila aliyeshindwa bali ni watanzania wapenda demokrasia ya kweli wameshindwa. Kwa lugha nyingine ni kuwa demokrasia imeshindwa Tanzania. Kwa hiyo wabunge wa CCM wataendelea kuwa misukule ya watawala kwani wataendelea kufinywa kwa koleo liitwalo kulinda masilahi ya chama. Masikini wasomi wetu watakao kuwa wabunge kupitia CCM wataishia kufungwa midomo na akili zao na watu wasio na elimu kama akina Y M .

Jaribu kufikiria scenario hii: Mahakama inaruhusu mgombea binafsi, Mtikila anatafuta mchungaji mwenzake ama mfuai mwenzake wa siasa za chuki dhidi ya wazanzibari, waasia, waislamu, wageni wengine na hata watanzania waishio mipakani ambao kwa mujibu wake sio watanzania wa kweli halafu wanakuwa wagombea binafsi katika uchaguzi ujao wa urais dhidi ya yule ambaye Mtikila tayari ameshasema kuwa ni gaidi na ana ajenda ya kuumaliza ukristo hapa nchini. Fikiria aina ya Tanzania tutakayokuwa nayo wakati na baada ya uchaguzi huo........
 
Naona mahakama imejishusha hadhi kwa kusema " shauri hilo ni la kisiasa zaidi na lilipaswa kujadiliwa Bungeni na kwamba Mahakama haina mamlaka ya kuamua suala hili".

sijaona nchi yenye viongozi waoga wa mabadiriko kama nchi yetu,na hii inatokana na ubovu wao na maovu yao wanayofanya kiasi cha kwamba wanaona wananchi watafaidi sana tukipata wagombea binafsi ambao hawafanyi kazi kwa manufaa ya chama chao.
 
Sasa ni ndio tunaingizwa kwenye mzungumkuti!!! Nilidhani Mahakama ndiyo chombo pekee cha kutoa haki mbalimbali kwa raia hata kama haki hizo zilibanwa katika taasisi mbalimbali za kijamii. Kama mahakama kwa upande mwingine unajipa jukumu la kutatua migogoro ya kiimani mathalani kutoa talaka, inashangaza sasa inapotuambia suala la mgombea binafsi ni la kisiasa....ndo maana wakati mwingine hao wanaojipachika majina ya 'learned brothers' kama walivyo wale ndugu zetu pale mjengoni Dodoma, :lol:huwa wananichefua kwa uzandiki kama huu.
 
Hatimaye rufaa yatupwa uamuzi kufanywa na Bunge!.

Ili mswada wa sheria ya mgombea binafsi upitishwe na bunge lazima wabunge wapige kura sasa kwa bunge la CCM hakuna kitu mpaka malaika atakapo shuka kuiokoa Tanzania.
 
Jaribu kufikiria scenario hii: Mahakama inaruhusu mgombea binafsi, Mtikila anatafuta mchungaji mwenzake ama mfuai mwenzake wa siasa za chuki dhidi ya wazanzibari, waasia, waislamu, wageni wengine na hata watanzania waishio mipakani ambao kwa mujibu wake sio watanzania wa kweli halafu wanakuwa wagombea binafsi katika uchaguzi ujao wa urais dhidi ya yule ambaye Mtikila tayari ameshasema kuwa ni gaidi na ana ajenda ya kuumaliza ukristo hapa nchini. Fikiria aina ya Tanzania tutakayokuwa nayo wakati na baada ya uchaguzi huo........

Now am back to my senses; Omar thanks a lot I was in a deep sleep......
 
kwa mara nyingine wananchi wameshindwa na serikali yao....eeeeh mungu tuokoe

Kweli wanainchi tumeshindwa lakini tujihurumie wote lakini zaidi ndugu yetu Mkjj kwani hayazijui mahakama za bongo na ni jana tu alituaminisha kwa kusema ..."ngojeni muone safari hii"
 
Jaribu kufikiria scenario hii: Mahakama inaruhusu mgombea binafsi, Mtikila anatafuta mchungaji mwenzake ama mfuai mwenzake wa siasa za chuki dhidi ya wazanzibari, waasia, waislamu, wageni wengine na hata watanzania waishio mipakani ambao kwa mujibu wake sio watanzania wa kweli halafu wanakuwa wagombea binafsi katika uchaguzi ujao wa urais dhidi ya yule ambaye Mtikila tayari ameshasema kuwa ni gaidi na ana ajenda ya kuumaliza ukristo hapa nchini. Fikiria aina ya Tanzania tutakayokuwa nayo wakati na baada ya uchaguzi huo........

Usiwe biased mkuu mtikila ni mkweli siku zote japo kwa sababu ya njaa kidogo naye aliingia mkenge wa mafisadi. Lakini ktk kupigania haki mtikila is real.....hakuna anayewachukia wazanzibari......wahindi wanachukiwa kwa tabia zao za ubaguzi na unyonyaji.
 
Ndugu zangu ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa CCM sasa hivi wameamua kuendesha nchi kidikteta, si mmeona ya CCJ? Ni kuhakikisha kuwa hakuna ajenda ya kutishia maslahi yao inapita...sijajua tutatokea wapi ni udikteta tu!
 
Back
Top Bottom