Mahakama ya Kisutu yawahukumu wezi wa EPA, Maranda na Farijala miaka 22 jela

Japo sijasoma habari hizi sehemu yeyote lakini kuwafunga miaka 22 samaki wachanga na kuwaacha mapapa haitoshi.
 
Mkuu maswali mengi ya kujiuliza hapo ina maana ni wenyewe tu ndio walichota hizo hela au vipi????

Kila mtu anayehusika na wizi wa epa ana kesi yake. Maranda na Farjala hawakushtakiwa kwa niaba ya akina Patel. Patel na wenzao wanakesi yao mahakamani. Inatia faraja japo kwa maoni ya mlalahoi wangepewa adhabu kubwa zaidi. Na hashimu maamuzi ya mahakama.
 
kwa nini walipe wakitoka?
wanatakiwa kufilisiwa sasa, watatoa wapi hiyo hela baada ya hiyo miaka ishirini au ndio itakuwa imeamishwa na sisi wananchi itakula kwetu?
mali zao zichukuliwe sasa ili liwe funzo
 
I take it as a start towards the right direction away from Impunity....let's wait and see...
 
I hope ni habari za kweli

CHADEMA watanasema hao jamaa wameonewa

What a shame kwa Chama kama Chadema , angehukumiwa Chenge na Lowasa pia wangesema wanaonewa na Kikwete

Damned if do damned if you dont!!
Toka lini chadema wakawatetea mafisadi kama nikuonewa ni kwanini wawe peke yao wengine inaishiaje! acha upumbavu wako wewe!
 
Sasa hapa kuna swali linafuata;
Kama pesa za EPA ndio zilizomwingiza Kikwete madarakani, kwanini hawa jamaa wamefungwa?
Kwanini aliruhusu wafikishwe mahakamani?
Je, hakuwa na uwezo wa kuwanusuru?
 
Habari kutoka Mahakama ya Kisutu inasema Rajabu Maranda ambaye ni katibu wa uchumi na fedha wa CCM mkoa wa kigoma na Mpwa wake Farijala wamefungwa jumla ya miaka kwa wizi wa EPA. Wakitoka wanalipa pesa walizokwapua
 
I hope ni habari za kweli

CHADEMA watanasema hao jamaa wameonewa

What a shame kwa Chama kama Chadema , angehukumiwa Chenge na Lowasa pia wangesema wanaonewa na Kikwete

Damned if do damned if you dont!!

Kaka hao ni small fish wapi big fish Kagoda? Inashangaza wizi umefanyika sehemu moja, kwa wakati mmoja yet wengine wanaenda jela just a week baada ya DPP kuomba ushahidi wa Kagoda. Where is equal justice for all? Hao watupwe Keko, but unless Kagoda wamepelekwa mahakamani EPA bado.
 
Naomba confirmation ya miaka waliohukumiwa maana nimepata source nyingine inasema wamehukumiwa miaka mitano (5) kila mmoja.
 
Nini maana ya Jumla? Je ina maana kila mmoja amefungwa miaka 11 jela?
Jumla maana yake ni kwa kila shitaka linalowakabili. Ina maana kama walikuwa na mashitaka 5 waliyotiwayo hatiani ina kuwa kosa 1 miaka 3 kosa la pili mwaka mmoja and so! Kuna kipengele kinasema (labda maana sikuwepo mahakamani) hukumu ya makosa hayo inakwenda kwa pamoja! Ukija kupiga hesabu labda hukumu kubwa ni miaka 3 theni watakaa miaka mitatu gerezani halafu msamaha wa rais au kamati ya parole ikawpunguzia! who knows!
 
Back
Top Bottom