Magufuli hana tofauti na wanaCCM wengine

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
nimefuatilia sokomoko na Mh.Magufuli na kauli zake dhidi ya wakazi wa Kigamboni, likanikumbusha kauli zingine tata kuwahi kutolewa huko nyuma, nikadharau kuwa hayo ni malipo kwetu dhidi ya ujinga wa kuchagua wasio chagulika , wasioaminika na wasiojali usalama wa maisha yetu na ndio maana hata hakuwahi kuona aibu kugawa nyumba kwa kijana wake na kwa yule mwanamke ambae uusiano wake haujawahi kuwekwa wazi na familia yake.

Wiki iliyopita Magufuli akaibukia na Wajapani na kututangazia kuwa watarudia ujenzi wa Barabara ya Kilwa, na akajitapa kuwa watarudia bila malipo mapya na gharama yote italipwa na serikali ya Japan maana wao ndio waliomleta Mkandarasi yule alieshindwa.
Nakubaliana nae katika hilo.
lakini tujiulize, Je hawakua mainjinia wa serikali ya Jamhuri ya Muungano waliopokea hiyo barabara ya awali ikiwa na mapungufu makubwa ? Je wamechukuliwa hatua gani kwa kupokea barabara duni, dhaifu na mbovu ajabu ? Je muda wetu unaopotea wakati wa ukarabati mpya unalipwaje ? je Mkandarasi yule aliejenga barabara mbovu amechukuliwa hatua gani ? maana ni Magufuli huyuhuyu huwa anajitapa ni bingwa wa kufuta makamouni ya kitapeli , Mbona hawa Kajima ni maji mazito kwake ?
Kwatabia zake za kuwalinda watendaji waliopokea barabara hiyo namuona magufuli akielea katika bahari ileile ya wanachama wenzie dhaifu wa ccm
 
oyaa kamanda hizo chuki zako binafsi tu magufuli ni mchapakazi hodari tukiondoa chuki za kisiasa magufuli namfagilia kinoma kwanza kila wizara akipelekwa ana fiti tofauti na mawaziri wengine tusimtie dosari jamani ni mtu makini sana na mchapakazi mzuri sana myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
oyaa kamanda hizo chuki zako binafsi tu magufuli ni mchapakazi hodari tukiondoa chuki za kisiasa magufuli namfagilia kinoma kwanza kila wizara akipelekwa ana fiti tofauti na mawaziri wengine tusimtie dosari jamani ni mtu makini sana na mchapakazi mzuri sana myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

Jina tu linaontesha udhaifu wa kujenga hoja! Karibu usome pole pole halafu changia ! Usikariri majibu
 
DAIMA NIMEKUA NIKIAMINI kuna shida ya kuwajibishana ndani ya chama cha mapinduzi na viongozi wake wote, huu ni ugonjwa, Kama walipokea Barabara mbovu kwanini hawakuwajibishwa, kama waliojenga walijenga chini ya kiwango kwanini hawawajibishwi....kabla hawajaanza ujenzi ni vyema tukaelezwa wamechukuliwa hatua gani kati ya wajenzi na wapokeaji wa barabara fake kama ile.?
 
Magufuli ni walewale tuu,alichowazidi wenzake ni uwezo wa kucheza na media.Tokea Igunga ndio alieleweka kuwa ni mtu wa aina gani
 
barabara ya kilwa road ilianza enzi za kawambwa, angalia usiwe jinamizi jipya wa kumpaka matope, mafuguri goggggoooo gooo
 
wewe inaonekana una matatizo ya kiakili sio kosa lako hilo ni kosa la daktari alokupa ruhusa kutoka kule marembe
 
arudishe nyumba alizoiba na atuambie kwa nini alibomoa jengo la tanroads pale ubungo akaliogopa la tanesco
 
barabara ya kilwa road ilianza enzi za kawambwa, angalia usiwe jinamizi jipya wa kumpaka matope, mafuguri goggggoooo gooo

hata kama ilianza na Nalaila Kiula, nisemacho kile Magufuli anachotaka kutuaminisha kwamba yeye ni Imara angeanza kusimamia kuhakikisha maofisa wa serikali waliopokea barabara chovu kama ile wanawajibishwa, uimara wake, mbwembwe zake ni porojo tu kama waliotufikisha hapa hawataadhibiwa
 
Back
Top Bottom