Magufuli ataka CHADEMA "washindwe na walegee"

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Magufuli nae ameingia kwenye orodha ya walalamikaji wa CCM wanaoijia juu Chadema kuhusu maandamano wanayofanya akisema waache kutoa matusi kwenye mikutano na wanachochea chuki hivyo washindwe na walegee.

Gazeti la Mwananchi la Leo.

Magufuli nae ajibu hoja asilalamike,
Inaonekana na yeye ndio ameshindwa na ameshalegezwa na Pinda.
 
Mbu ni mbu tu, awe Anopheles au Culex anabaki ni mbu tu. Hematobium na mansoni vyote ni vichocho. Huwezi kumtenga Magufuli kati ya CCM isipokuwa kwa sub-species yake.
 
Mh hapa kazi. Kuna wengi ni pro-Chadema na wakati huo huo ni pro-Magufuli. Sasa sijui hapa wata chagua upande gani? Au watakaa kimya?
 
Mh hapa kazi. Kuna wengi ni pro-Chadema na wakati huo huo ni pro-Magufuli. Sasa sijui hapa wata chagua upande gani? Au watakaa kimya?

Ukiwa pro-CHADEMA at the same time ni pro-Magufuli maana yake wewe ni mnafiki a.k.a bendera ufuata upepo!

Huwezi kutenganisha Magufuli na CCM! Uchafu wa CCM Magufuli is part of it

Ukiwa pro-CHADEMA at the same time ni pro-Magufuli maana yake wewe ni mnafiki a.k.a bendera ufuata upepo!

Huwezi kutenganisha Magufuli na CCM! Uchafu wa CCM Magufuli is part of it

Lakini ni kweli kwamba CCM hakuna mwadilifu hata mmoja? nadhani wapo wanaogopa tu kutoka huko wasijekolimbwa, CCM ni zaidi ya tuijuavyo. Magufuli naomba kudeclare kwamba nilikuwa shabiki wake, lakini kwa hili naanza kuamini CCM ina wenyewe.
 
Magufuli,Sitta,Mwakyembe wote ndio wale wale tu,kama wangekuwa ni watu makini wasingetetereka kuikemea serikali yao na chama chao ila ni watu wa kuwahadaa wananchi na kujitafutia cheap popularity tu,kwani ni chuki zao za kichama ndio muda mwingine hupelekea kuropoka ropoka nakuonekana ni wakemea ufisadi.
"Mtu yeyote anayejifanya hapendi ufisadi lakini yumo ndani ya mfumo wa kifisadi basi mtu huyo pia ni fisadi tu"
 
Huyu Magufuli naona kama anataka kuiharibu CV yake kwa kujishuhulisha na kuwaingilia wanaChadema katika mikutano yao, yeye aendelee na bomoa bomoa yake tena naona hii spead yake Mizengo Pinda kashampiga stop!
 
Masikini magufuli, hata wewe umeshakuwa mtu wakuambiwa useme nini?
 
Masikini magufuli, hata wewe umeshakuwa mtu wakuambiwa useme nini?

Sio kaambiwa mzee, huyo kachanganyikiwa baada ya kuona CHADEMA wameshamwaga sumu kwake CHATO na watu hawamfagilii no more ndio maana kakurupuka na kuonyesha the TRUE Magufuli
 
Wananchi kazi tunayo! Naona viongozi wanachanganyikiwa sasa kama wameanza kukemea kama wachungaji hii tena siyo siasa ni vurugu kubwa
 
Kweli huu ndio familia ya bata watoto mbele mama nyuma yaani alichosema mkuu wote wanaelekea humo humo. Hawana jipya kwani mtoto akisaidia kama hawatamtoa, watamtoa kwa harufu.
 
CCM bana hawaishiwi viroja. Yani yule mnukuu biblia wao MAKAMBA KAPUMZIKA ANAIBUKA MWINGINE.....Tusubiri kama ameanza na hiyo salam ya wapendwa soon ataanza kunukuu vipengele vya Biblia kama katibu wake Makamba.
 
Ukiwa pro-CHADEMA at the same time ni pro-Magufuli maana yake wewe ni mnafiki a.k.a bendera ufuata upepo!

Huwezi kutenganisha Magufuli na CCM! Uchafu wa CCM Magufuli is part of it

word,..siku zote nimekuwa nikisema magufuli ni walewale tu
 
Kila atakaye kosoa cdm ni mkosaji hana akili tena ni fisadi. Hiki ni chama kutoka mbinguni,ambacho hakikosei?Au kwa sababu kinasapoti ya wale jamaa wasiomtambua meya wa arusha,kiasi wafuasi wake waamini kila kitu
 
Huyu Magufuli naona kama anataka kuiharibu CV yake kwa kujishuhulisha na kuwaingilia wanaChadema katika mikutano yao, yeye aendelee na bomoa bomoa yake tena naona hii spead yake Mizengo Pinda kashampiga stop!

Wote wameishalogwa, kwisha kazi. hawaeleweki kabisa.:hand: ccm bye
 
mungu mkubwa kama ameokoka maana kuna hadhithi wanayohusishwa na sababu za kuhamia chato na uchawi mie simo
 
Sikuwahi kumuweka Magufuli katika watu waadilifu toka ampe mimba mtoto wa rafiki yake, agawe nyumba za serikali kwa upendeleo na kumpa huyo hawara yake na kaka yake wakati wakiwa pasipo kuwa na sifa za kupewa nyumba hizo.

Magufuli ambaye hakuwawezesha wavuvi, hakuwatafutia soko wavuvi zaidi ya kukamata vyavu za korokoro na kukamata samaki tusizokuwa nauwezo wa kuvua kwasababu ya vitendea kazi duni.

Kizuri afanyacho mwache afanye maana ni wajibu wake lakini sio muadilifu kama wengi wanavyo mnadi
 
Back
Top Bottom