Magufuli apiga STOP Safari za nje ya Nchi; Elimu Bure kuanza Januari 2016...

Asisahau semina elekezi na jinsi ya kujenga viwanda na kuunda mahakama ya mafiosi hadi
 
Asisahau semina elekezi na jinsi ya kujenga viwanda na kuunda mahakama ya mafisadi
 
Yap. Anapenda sana publicity huyu Ngosha. Nchi haiendeshwi kama wizara kwa kukurupuka, kupigwa picha na kupigiwa makofi kwa kudhalilisha watendaji hadharani kama ilivyotokea jana wizara ya Fedha.Very soon ataisoma namba yeye mwenyewe. Tunataka mikakati siyo misifa ya kufoka mbele ya kamera.

Msifanye kazi kwa mazoea tulieni maofisini mpige kazi
Siyo kuruka ruka muda wa kazi, mtafukuzwa kazi muanze kulia lia oooho msicheze na magufuli ati
 
attachment.php

Ikiwa ni siku yake ya tatu kulitumikia taifa kama Rais wa awamu ya tano ya jamhuri wa Muungano wa Tanzania baada ya jana kufanya ziara ya kushtukiza Wizara ya fedha na kubaini uwepo wa changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na utoro wa watumishi alioushuhudia,leo Rais John Pombe Magufuli akutana na watendaji wakuu wa serikali na kufanya nao kikao kwa masaa kadhaa.

Katika kikao hicho,mbali na kuelezana changamoto zilizopo katika utumishi wa umma na namna ya kukabiliana/kuzitafutia ufumbuzi Rais John Pombe Magufuli asema bado msimamo wake uko palepale aliposema yeye ni rafiki wa wachapakazi nanukuu "Nasema kweli kabisa, msema kweli mpenzi wa Mungu. Wazembe ,majizi na mafisadi nitalala nao mbele" na kuongeza kuwa haikuwa kauli ya kutafutia kura tu bali ndivyo yeye alivyo.

Mwisho Rais John Pombe Magufuli aliwaasa watumishi wote kulitumikia taifa na kuzitendea haki nafasi na mishahara ya walipa kodi maskini na wavujajasho wa-Tanzania wanayolipwa na kuongeza kwake yeye ni kazi tu.
 
Attachments

  • Screenshot from 2015-11-07 13:58:29.png
    Screenshot from 2015-11-07 13:58:29.png
    122.7 KB · Views: 2,750
Magufuli amewapiga marufuku Makatibu Wakuu wa Serikali kusafriri nje ya nchi akiwataka wakae wafanye kazi na hasa kuokoa fedha kiasi kikubwa kinatumika ktk sfari za nje. Vile vile ameelekeza mabalozi walioko nje waiwakilishe serikali lakini kama kuna ulazima itabidi kibali kitolewe na Katibu Mkuu Kiongozi au yeye mwenyewe.

Amewaagiza Makatibu Wakuu kwa sasa waelekeze nguvu zao kutembelkea miradi na kutatua kero za wananchi vijijini.

Kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, amewataka kutoza kodi kwa wafanya biashara wakubwa wakubwa na wale watakaokwepa basi maafisa wa TRA wajiandae kuwajibika.

Ameitaka Mamlaka ya Bandari kuhakikisha inasimamia vilivyo upitishwaji wa mizigo na kulipa kodi inayotakiwa.

2bb9176be1c83227bd7f5bc5099a13d2.jpg
 
Hakika Magufuli ni chaguo la Mungu na ni fahari kwa watanzania.....
 
nn maana ya wafanya biashara wakubwa ndo wahusika wakod jmn!? je sisi wenye maduka itakuwaje?
 
Jamani naomba tumpe muda.Tusiwe watu waku-crisize tu hata pale ambapo hakuna sababu.Angekutana nao Ngurdoto mngesema ametumia hela vibaya,sasa kakutana nao Ikulu,nongwa.Personally so far so good.Keep it up Rais wangu.Naamini with detrmination utazivunja ngome.
Kama mikutano ndo kasi na viwango waliomtangulia mbona wangetisha?? Mikutano si tija, aelekeze anachokitaka kifanyike tu. Walikaa mahoteli makuubwa ya Ngurdoto lakini mwisho wa siku tuliona kilichotokea. Akumbuke maneno yake mujarab; HAPA KAZI TU sio vikao na kutembeleana ofisini. Hiyo ni kazi ya tarishi tuuuu
 
Magufuli amewapiga marufuku Makatibu Wakuu wa Serikali kusafriri nje ya nchi akiwataka wakae wafanye kazi na hasa kuokoa fedha kiasi kikubwa kinatumika ktk sfari za nje. Vile vile ameelekeza mabalozi walioko nje waiwakilishe serikali lakini kama kuna ulazima itabidi kibali kitolewe na Katibu Mkuu Kiongozi au yeye mwenyewe.

Amewaagiza Makatibu Wakuu kwa sasa waelekeze nguvu zao kutembelkea miradi na kutatua kero za wananchi vijijini.

Kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, amewataka kutoza kodi kwa wafanya biashara wakubwa wakubwa na wale watakaokwepa basi maafisa wa TRA wajiandae kuwajibika.

Ameitaka Mamlaka ya Bandari kuhakikisha inasimamia vilivyo upitishwaji wa mizigo na kulipa kodi inayotakiwa.

zile ziara za NHC kuwapeleka wabunge hongkong na Dubai kushangaa barabara hazitakiwi, kila mtu ajifunze kula mshahara wake.
 
makatibu wakuu wasiende nje ila mawaziri ambao ni product ya ccm ni ruksa kwenda nje kama karamagi alivyoenda london kusaini mkataba wa buzwagi..
 
Exactly, kuna mabalozi karibu nchi nyingi duniani. Kazi yao ni kuiwakilisha nchi kwa mambo ya kidiplomasia na sio kusafirisha watu kila siku fedha za walipa kodi zinaliwa pasi na huruma. It's a good beginning mister president.
 
Back
Top Bottom