Magufuli apiga STOP Safari za nje ya Nchi; Elimu Bure kuanza Januari 2016...

Mlonganzila

Member
Feb 28, 2013
99
26
Leo Jumamosi, Rais Dr. Magufuli akutana na makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu na watendaji wakuu wa serikali leo Ikulu.

Huu ni Mkutano Maalum.

=============================

Updates;

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka mara baada ya kuapishwa.

"Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU' na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja" Rais Magufuli amesema.

Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.

Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:

Kuanzia mwezi Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji

Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi
Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi huko nje.

Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.

Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.

Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais ama Makamu wake.

Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.

"Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja". Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.

………………………MWISHO……………………

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

7 Novemba, 2015

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKUTANA NA MAKATIBU WAKUU, MANAIBU MAKATIBU WAKUU NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI LEO IKULU

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Rished Bade na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Katibu Mkuu Utumishi Mhe HAB Mkwizu na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Picha na Ikulu

Kama mikutano ndo kasi na viwango waliomtangulia mbona wangetisha?? Mikutano si tija, aelekeze anachokitaka kifanyike tu. Walikaa mahoteli makuubwa ya Ngurdoto lakini mwisho wa siku tuliona kilichotokea. Akumbuke maneno yake mujarab; HAPA KAZI TU sio vikao na kutembeleana ofisini. Hiyo ni kazi ya tarishi tuuuu
 
Msumari baraza la mawaziri kwa sasa halipo litaundwa upya baadA ya kuteuliwa waziri mkuu mpya
 
Kama mikutano ndo kasi na viwango waliomtangulia mbona wangetisha?? Mikutano si tija, aelekeze anachokitaka kifanyike tu. Walikaa mahoteli makuubwa ya Ngurdoto lakini mwisho wa siku tuliona kilichotokea. Akumbuke maneno yake mujarab; HAPA KAZI TU sio vikao na kutembeleana ofisini. Hiyo ni kazi ya tarishi tuuuu
Hiyo HAPA KAZI TU inatekelezwaje kama haukutani na watendaji kazi wako wakuu? Acheni chuki!
 
Kama mikutano ndo kasi na viwango waliomtangulia mbona wangetisha?? Mikutano si tija, aelekeze anachokitaka kifanyike tu. Walikaa mahoteli makuubwa ya Ngurdoto lakini mwisho wa siku tuliona kilichotokea. Akumbuke maneno yake mujarab; HAPA KAZI TU sio vikao na kutembeleana ofisini. Hiyo ni kazi ya tarishi tuuuu

tengeneza chai ya tangawizi tembea nayo utakufa kwa kihoro mwishowe
 
UKAWA maswali yenu ya ajabu jibu ni hili rais mpya alipoapishwa baraza la mawaziri la Kikwete nalo lilimaliza muda wake.

wanaposema kuvunjwa kwa baraza la mawaziri usifikiri wanavunja kwa kutumia nyundo.

So Hawa makatibu wakuu wanakuwa wapo tu kama wale wazee wa baraza ktk mahakama za mwanzo au walishawekwa wengine siku Pombe ilihalalishwa kuwa Rais?
 
Back
Top Bottom