Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue, ameweka bayana kuwa hata safari ya nje ya nchi isiyogharamiwa na serikali nayo inaweza kukataliwa pia kama itaonekana haina tija kwani mtumishi awapo nje ya nchi bado serikali inamlipa mshahara wake hivyo ni lazima serikali ijiridhishe kwanza kuhusu umuhimu wa safari hiyo.
Chanzo: Channel 10.
Changamoto:Katibu Mkuu kiongozi hii kazi ya kuidhinisha safari sidhani kama ataimudu peke yake labda kazi zake zingine zisimame maana bila shaka meza yake itajaa maombi ya safari za kila siku na bado zingine zitakuwa safari za dharura.
Ushauri:Kwenye Bunge litakaloonza mwishoni mwa mwezi January mwakani,serikali ipeleke taarifa Bungeni imepokea maombi kiasi gani ya safari na ni maombi kiasi gani yamekubaliwa na yale yaliyokataliwa na pia umma upewe taarifa ni kiasi gani cha fedha serikali imeokoa.
Bado siku ya siku hii nia njema ya kuokoa pesa ni sehemu ya kutengeneza mianya ya rushwa tena kubwa kubwa itakayo husu Ofisi ya Raisi mmoja kwa Mmoja-chini ya Usimamizi wa Katibu Mkuu Kiongozi.
Nilitegemea mpaka sasa Katibu Mkuu Kiongozi angekuwa amekwisha weka wazi Vigezo vinavyotumika kufikia kutoa kibali cha kusafiri nje.
Maana itafika mahali Mfumo huu wa nyuma ya pazia ndiyo utakuwa Fimbo kwa waisopendwa kwa kuchuki binafsi au za Kisiasa,Ukabila nadani yake na mengineyo.
Everything you do in life you must do with caution!