Magufuli akiteua wakuu wa wilaya 171, sitoelewa azma yake ya kubana matumizi

Mkuu wa wilaya, MKURUGENZI, Katibu tawala, AFISA tawala wa wilaya, mbunge, mwenyekiti wa HALMASHAURI ya wilaya(Mayor), only in Tanzania
 
mmmh ama kweli hivi ni nani mwenye job descriprion ya mkuu wa wilaya atupie hapa !!
Utaitafuta sana hutoipata, cheo cha kisiasa! Ila nadhani ukipata job description ya mwenyekiti wa ccm wilaya itakuwa inafanana na ya mkuu wa wilaya
 
Utaitafuta sana hutoipata, cheo cha kisiasa! Ila nadhani ukipata job description ya mwenyekiti wa ccm wilaya itakuwa inafanana na ya mkuu wa wilaya
Hii umetoa kali, watanzania bwana!
 
Rafiki yangu ambaye ni mkuu wa wilaya aliwahi kuniambia wakuu wa wilaya wanapositaafu au kutoteuliwa tena au wakiambiwa msemo maarufu wa mzee wataepangiwa kazi nyingine hulipwa kiinua mgongo cha Tsh milioni 80. Hii hajalishi unapandishwa kuwa mkuu wa mkoa au unahamishiwa wilaya nyingine. Ili mradi miaka mitano imeisha inahesabika umesitaafu.

Leo nchi yetu ina wilaya 171, kwa utaratibu huo wakuu wa wilaya 171 wanatakiwa dkulipwa au wameshalipwa kiinua mgongo cha mil 80 kila mmoja! Hapo hujaesabu magari ya kifahari 171 ambayo hakuna linalopungua sh mil 300! na mshahara wa mil 3.8 kwa kila mkuu wa wilaya. Huu ni ubadhilifu!

Ningemuelewa rais wetu kama angewaacha hawa waliopo waendelee wakati anatafakari kukubaliana na rasmu ya Warioba ya kuundoa mfumo huu. Ikiwa rais atafanya uteuzi wa wakuu wa wilaya kitu ambacho najua atafanya, basi aache kutwambia ana adhima ya kubana matumizi.
Acha kumtisha Rais
 
Tusubiri akabiziwe chama, nahisi anasubiri akabiziwe chama ili afanye kitu tunachosubiri wengi kwenye katiba mpya. Naziona dalili za kukubaliana na maoni ya Waliyoba kutoka kwa Magufuli.

Tumuombee..
 
Tusubiri akabiziwe chama, nahisi anasubiri akabiziwe chama ili afanye kitu tunachosubiri wengi kwenye katiba mpya. Naziona dalili za kukubaliana na maoni ya Waliyoba kutoka kwa Magufuli.

Tumuombee..
Kumbuka Kikwete alibadirikia njiani baada ya wazee wa chama kumwambia katiba mpya itaiangusha Ccm
 
Watu wengine bhana. Mtoa mada anajaribu kuangalia namna ya kupunguza ufujaji wa pesa yetu ili tufanye mambo ya kimaendeleo wengine mnamshambulia.
Kuna haja gani mtu kulipwa kiinua kifua mil.80 halafu baada ya miaka 5 hata kama ataendelea au atateuliwa kuwa mkuu wa mkoa?
Tusijipofushe ufahamu wetu. Magu lazima aendelee kuonyesha tofauti na aliyemtangulia hata ktk hili.
Angekuwa alishafanya angesifiwa sana tu lkn kwa sababu anakumbushwa, mkumbushaji anashambuliwa.
Poor Tanzania.
Nadhani kama mna nia njema, tungeanza kupiga kelele au kumshauri Rais kufuta zile posho za wabunge kablay ya wakuu wa wilaya, mana hata ukiangalia posho ya mbunge bado ni ndefu sana.
 
Nadhani kama mna nia njema, tungeanza kupiga kelele au kumshauri Rais kufuta zile posho za wabunge kablay ya wakuu wa wilaya, mana hata ukiangalia posho ya mbunge bado ni ndefu sana.
Hiyo haizuii jambo hili kuongelewa.
Hata ungeletwa uzi unaotaka kupunguzwa/kufutwa posho hizo, kuna watu wangetaka mjadala uanzie kwingine.
 
Acheni kumshambulia mleta mada anayo pointi kwenye hoja yake. Kama kweli kuna gharama kubwa namna hiyo sioni mantiki yoyote ya kuwa na hawa watu. Kama kweli kuna kubana matumizi hiv vyeo vya ajabu ajabu viondolewe abakizwe mkurugenzi anatosha kabisa kusimamia wilaya.

Hv kuna sababu ipi ya msingi kuwa na wateule wawili wa Rais katika wilaya?

Mkurugenzi na wawakilishi wa wananchi waliopo kwenye wilaya wanatosha kabisa.

Sielewi nini kilichowafanya CCM kukataa rasmu ya Warioba. Sielewi kama CCM kama kweli wana nia ya dhati kufanya Taifa hili kusonga mbele.

Mbona haya ni mambo yaliyo wazi tu hata kama mtu hana uwezo wa kupambanua jambo hili atakuwa na uwezo wa kuona hivi vyeo havina maana yoyote?

Tunamwamini Magufuli tusubiri. Tuna imani atatekeleza mapendekezo ya wananchi.. tuna imani hatatuangusha Watanzania. Tuna imani ataacha legacy ambayo wengine walishindwa. Tuna imani katika hili atakuwa mtu wa kukumbukwa katika uongozi. Tuna imani anawaangalia Watanzania na siyo waliotegesha meno kumaliza nchi hii. Tuna imani na wewe Magu hutatuangusha. We pray for you.
Mawazo yako ni ya kimaendeleo na yenye uono mkubwa wa uelewa ndani yake tofauti na wale wenye kuandika kwa ushabiki tu wa chama chao raisi wao asielekezwe au kushauriwa kwa lolote.Hao ndio ninao piga kelele kila siku hawatakiwi kuingia jukwaa hili la great thinkers kwani wana majukwaa yao ya viwango vyao.Ndio ccm ndio iliyomtoa raisi Magufuli.Ccm sio chama chenye kupenda mabadiliko.Uongozi alioongoza nao mwalimu Nyerere,Karume,Sokoine na Kawawa ki-utendaji na ki-uwajibikaji wao.kwa wananchi sio ulioendelea baada tu ya wao kufariki.Hakuna kitakachofanikiwa kwa maendeleo na ustawi wa wananchi wa taifa hili kama(kwa maoni yangu)na wengi kama rasimu ya judge Warioba ambayo ndiyo ina mapendekezo ya wananchi haitapitishwa na bunge la katiba.Ikishafanyika hivyo azimio letu la Arusha lirudishwe na kuachana na la Zanzibar walilokimbilia huko wakubwa na kuzika lile la Arusha na kujiondolea miiko yote ya viongozi ili waweze kumiliki majumba,bishara kubwa kubwa,viwanda na migodi na kubinafsisha mali za taifa ilihali bado ni watumishi wa umma/serikali.Kwa kweli matatizo haya makubwa makubwa na ukwapuaji wa hela na rasilimali za taifa ulianzia hapo.Kama ulivyojiuliza nini mantiki ya kuwa na wateule wawili wa raisi kwenye wilaya hata mimi siioni.Mkurugenzi na timu yake ni wataalam.Labda mkuu wa wilaya yupo pale kisiasa tu basi angelipwa na chama chake.Wakuu wa wilaya 171,mashangingi,nyumba zao,madereva,masecretary na wahudumu wa ofisi ni gharama kubwa kwa serikali.Gharama za service ya magari haya na mafuta yake ni kubwa sana wakati hata toyota hardtops zingetosha.Kazi za wakuu wa mikoa nazo zingeweza kufanywa na makatibu tawala wa mikoa kwani ni wataalam.Sasa uje uwalipe mil.80 wakistaafu na bado posho walishachota za kutosha taifa hili haliwezi kupiga hatua wakati kodi ya mapato inayolipwa na viwanda vya bia ni zaidi sana ya malipo tulipwayo na migodi yote ya madini.Tukija kwa raisi wetu Magufuli nasema tunamwamini na tunamwombea mwenyezi Mungu amuepushe na mabaya/wabaya katika kutekeleza adhma ya kuwaletea wananchi maendeleo.Nae ni ccm kindaki ndaki na mwezi June mwaka huu kama haikutokea figisu atakabadhiwa kofia ya chama taifa na mh.Kikwete.Hapo hapo raisi anza kusafisha chama chako kuanzia usafi wa wanachama,misingi yake,muundo,taratibu za utendaji na huko huko tangaza kulirusha azimio la Arusha.Rudi bunge la katiba waambie rasimu itakayojadiliwa na kupitishwa sio maoni ya wabunge kwa niaba ya wananchi wanaowawakilisha bali ni maoni ya wananchi ambayo tayari walishayatoa kwa tume ya Warioba. Nakuhakikishia utaongoza vizuri kwani hata mafisadi unaotumbua sasa watakuwa wameshatumbuliwa na miiko ya azimio na nakuhakikishia kipindi chako cha pili wala huna haja ya kufanya kampeni.HAPA KAZI TU.
 
Watu wengine bhana. Mtoa mada anajaribu kuangalia namna ya kupunguza ufujaji wa pesa yetu ili tufanye mambo ya kimaendeleo wengine mnamshambulia.
Kuna haja gani mtu kulipwa kiinua kifua mil.80 halafu baada ya miaka 5 hata kama ataendelea au atateuliwa kuwa mkuu wa mkoa?
Tusijipofushe ufahamu wetu. Magu lazima aendelee kuonyesha tofauti na aliyemtangulia hata ktk hili.
Angekuwa alishafanya angesifiwa sana tu lkn kwa sababu anakumbushwa, mkumbushaji anashambuliwa.
Poor Tanzania.

Mkuu hao wanaopingana na mleta hoja ni wakuu wa wilaya wanaopigania matumbo yao! Ila kiukweli wakuu wa wilaya ni majipu, ndo maana kuna mdau ameomba job description ya wakuu wa wilaya.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Wanataka kusikia sifa tu za kumpamba Magu.
He is not God.
Tena ningetamani azipunguze wilaya na mikoa iliyowekwa kisiasa na kiujanja ujanja ili kulipana fadhila kipindi cha JK.
Tunaumia sana kuiendesha serikali kuu wakati baadhi ya majukumu yangefanywa na watu wachache tu.
 
N
~~>Tuletee Uthibitisho wa Hayo Malipo ya 80M.....

~~>Ikiwa hayo malipo yapo Kisheria nani wa kuyabadilisha¿¿¿
a hizo sheria kandamizi hazibadilishwi? Kila kitu kwa mujibu wa sheria.!!
 
Rafiki yangu ambaye ni mkuu wa wilaya aliwahi kuniambia wakuu wa wilaya wanapositaafu au kutoteuliwa tena au wakiambiwa msemo maarufu wa mzee watapangiwa kazi nyingine hulipwa kiinua mgongo cha Tsh milioni 80. Hii hajalishi unapandishwa kuwa mkuu wa mkoa au unahamishiwa wilaya nyingine. Ili mradi miaka mitano imeisha inahesabika umesitaafu.

Leo nchi yetu ina wilaya 171, kwa utaratibu huo wakuu wa wilaya 171 wanatakiwa kulipwa au wameshalipwa kiinua mgongo cha mil 80 kila mmoja! Hapo hujaesabu magari ya kifahari 171 ambayo hakuna linalopungua sh mil 300! na mshahara wa mil 3.8 kwa kila mkuu wa wilaya. Huu ni ubadhilifu!

Ningemuelewa rais wetu kama angewaacha hawa waliopo waendelee wakati anatafakari kukubaliana na rasmu ya Warioba ya kuundoa mfumo huu. Ikiwa rais atafanya uteuzi wa wakuu wa wilaya kitu ambacho najua atafanya, basi aache kutwambia ana adhima ya kubana matumizi.
Hata kama mtu ni mzigo aachwe aendelee kuwepo kwa kuogopa gharama, unadhani kuna kitu kizuri cha bure? Hujui pia kua bure ni aghali?
 
Watu wengine bhana. Mtoa mada anajaribu kuangalia namna ya kupunguza ufujaji wa pesa yetu ili tufanye mambo ya kimaendeleo wengine mnamshambulia.
Kuna haja gani mtu kulipwa kiinua kifua mil.80 halafu baada ya miaka 5 hata kama ataendelea au atateuliwa kuwa mkuu wa mkoa?
Tusijipofushe ufahamu wetu. Magu lazima aendelee kuonyesha tofauti na aliyemtangulia hata ktk hili.
Angekuwa alishafanya angesifiwa sana tu lkn kwa sababu anakumbushwa, mkumbushaji anashambuliwa.
Poor Tanzania.
Hiyo ndiyo sheria kwa sasa na haikuanza leo na ili hilo jambo liwe kama mtoa mada alivyoshauri na wewe kumuunga mkono basi ni lazima sheria hiyo ifanyiwe marekebisho mahsusi. Rais hawezi akaamka asbhi tu na kuitengua hiyo Sheria, kuna taratibu zake.
 
Hata kama mtu ni mzigo aachwe aendelee kuwepo kwa kuogopa gharama, unadhani kuna kitu kizuri cha bure? Hujui pia kua bure ni aghali?
Ukisoma vizuri uzi wangu utajua kwamba siungi mkono uwepo wa wakuu wa wilaya. Hivo kama ni mizigo waondolewe na tusiwe na mfumo huu wa kikoloni
 
Acheni kumshambulia mleta mada anayo pointi kwenye hoja yake. Kama kweli kuna gharama kubwa namna hiyo sioni mantiki yoyote ya kuwa na hawa watu. Kama kweli kuna kubana matumizi hiv vyeo vya ajabu ajabu viondolewe abakizwe mkurugenzi anatosha kabisa kusimamia wilaya.

Hv kuna sababu ipi ya msingi kuwa na wateule wawili wa Rais katika wilaya?

Mkurugenzi na wawakilishi wa wananchi waliopo kwenye wilaya wanatosha kabisa.

Sielewi nini kilichowafanya CCM kukataa rasmu ya Warioba. Sielewi kama CCM kama kweli wana nia ya dhati kufanya Taifa hili kusonga mbele.

Mbona haya ni mambo yaliyo wazi tu hata kama mtu hana uwezo wa kupambanua jambo hili atakuwa na uwezo wa kuona hivi vyeo havina maana yoyote?

Tunamwamini Magufuli tusubiri. Tuna imani atatekeleza mapendekezo ya wananchi.. tuna imani hatatuangusha Watanzania. Tuna imani ataacha legacy ambayo wengine walishindwa. Tuna imani katika hili atakuwa mtu wa kukumbukwa katika uongozi. Tuna imani anawaangalia Watanzania na siyo waliotegesha meno kumaliza nchi hii. Tuna imani na wewe Magu hutatuangusha. We pray for you.
Wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwepo tangu Uhuru nadhani kuna mantiki yao kuwepo cha kufanya hapa ni kurekebishiwa majukumu ili watumike kwa tija zaidi.
 
Back
Top Bottom