Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Magufuli adaiwa kuikosesha serikali mapato
Na Reuben Kagaruki
KAMPUNI zinazojihusisha na uwekekaji mabango ya matangazo nchini, zimemshauri Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, kusitisha agizo lake la kutaka
mabango yaliyopo kandokando ya barabara kuong'olewa badala yake akutane na wadau wote ili kujadiliana mfumo unaofaa kwa nia ya kuepuka usumbufu na athari ambazo zimeanza kujitokeza.
Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZEK Group International, Bw. Edwin Sannda, alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana.
Alisema iwapo wadau wote wakishirikishwa itapitishwa sheria ndogo, ambapo mabango ambayo yataonekana yanafaa kuendelea kuwepo yatabaki na mengine yaondolewe kwa wahusika kupewa notisi.
Alifafanua kuwa utaratibu wa aina hiyo kama ungefuatwa ungeondoa usumbufu na 'ugomvi' ulioanza kujitokeza kwa sasa.
Mwishoni mwa mwaka jana Dkt. Magufuli alitoa maelekezo kuwa hataki kuona katika hifadhi ya barabara mabango ya matangazo kwa madai kuwa ni chanzo cha ajali. Agizo hilo lilifuatiwa na uwekaji alama ya X kwenye mabango na mengine kuondolewa au kuharibiwa bila wahusika kupewa notisi au kushirikishwa kama wadau.
Bw.Sannda alisema baada ya kutolewa agizo hilo, wao walienda kuonana na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROAD) Mkoa wa Dar es Salaam na kumweleza maoni yao kama wadau, lakini inaonekana juhudi zao zimegonga mwamba kwa kuwa ung'oaji mabango hayo umeendelea.
"Jitihada zote za kuomba utaratibu wa sasa ubadilishwe zimegonga ukuta, ni vema waziri akakutana na wadau vinginevyo suluhisho linaweza kuishia kwenye masuala ya kisheria," alisema Bw.Sannda na kutoa mfano kuwa mabango ambayo tayari yameong'olewa au kuharibiwa walikuwa na mikataba na wateja wao kwa miaka kati ya mmoja hadi mitatu. Alisema kutokana na mabango hayo kung'olewa, tayari wateja wameishaanza kudai kulipwa fidia kwa madai ya kuvunjwa kwa mikataba.
Alibainisha kuwa uamuzi wa waziri wa kuagiza mabango yang'olewe bila kushirikisha wadau yameathiri kampuni zaidi ya 20 zinazojihusisha na uwekaji mabango. "Uamuzi huo umepunguza chanzo kikuu cha mapato ya serikali kuu na serikali za mitaa," alisema.
Alisisitiza kwamba kwa mwaka wamekuwa wakilipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kiasi cha sh. bilioni 10 na kwa halmashauri sio chini ya sh. milioni 300 kwa mwenzi. Alisema msimamo wa waziri ukiendelea kubaki ulivyo utasababisha wafanyakazi wa kampuni hizo kupoteza ajira na mapato mengine kuendelea kupotea.
Alitoa mfano akisema kampuni yake imekuwa ikilipa sh. milioni 20 kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutokana na kutumia umeme kwenye mabango, mapato ambayo shirika litaanza kuyapoteza.
Kwa upande wa kampuni yake alisema uamuzi huo utaiathiri hasa kwa kuzingatia kuwa ilikuwa na mkopo wa sh. bilioni nne kutoka Benki ya CRDB. Alishauri kuwa maamuzi mengine yanatakiwa kufuata sheria vinginevyo yanaweza kuigharimu serikali pale yanapotolewa bila kushirikisha wadau.
1 Maoni:
Anonymous said... Poleni waathirika, lakini mujuwe mlikuwa hamfati sheria, kwani munajuwa fika umbali wa hifadhi ya barabara na pia wakurugenzi na watendaji wao wa jiji ndio wenye makosa, leo waziri anawajibika kufata sheria mnaanza kulalamika eti mpk mukae sio yeye wa kukaa nae wakuwabana ni hao jiji. mnajuwa namna ya kuyaweka hayo mabango na yakasomeka bila kuingilia mamlaka zingine.Na hizo pesa mnazitaja leo ktk hasara, lakini wao jiji hawatangazi makusanyo hayo ni aibu jiji kuwa chafu maana chanzo kimoja tu ni zaidi ya million 300 kwa mwezi je, vyanzo vingine