Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
- Thread starter
- #121
Hapo ni sawa na kusema Mimi nimeongopa.
Sawa!
But I gave you figures, you can deny them by bringing your figures from your sources.
Nguruvi3 , amesema in 11months government imekopa 10T. Si aonyeshe sources au aweke hizo data hapa? Ukisema bila kuanika chanzo, unamaanisha kuwa you just know it.
Okay, taarab pembeni.
December, 2015 mpaka July, 2016 Deni LA Taifa zimeongezeka kwa 3.6T na Kati ya hizo, Private sector loans ni 1.2 na Central government and Public Corporations Deni liliongezeka by 2.4T. Hapa tunazungumzia ongezeko LA principal na interest. Central Government part of this loan is about 1.9T.
Kwa hiyo, kutoka na data za Nguruvi3 . Kuna Kama 8T zilikopwa August na September. Kwanini asiuonyeshe sources zake?
Sources zangu zipo kwenye BOT (MER/QEB)
Total interest paid by Central Government ni approximately 0.97T.
Ninachowaambia Mimi ni kuwa, mwezi July ambazo ni mwezi wa kwanza wa (2016/17), serikali imelipa 0.625T to domestic banks and non-bank institutions. Na imekopa net bil17 foreign na bil.76 local.
Sasa hapo ni sawa kusema serikali imelipa kuliko ilivyokopa kwa 2016/17 financial year? Maana estimates za bajeti zulikadiria -178bn balance and it ended up to be 461bn surplus.
.
Huko juu ulisema kwamba Serikali ya awamu ya Tano haikopi tena, lakini sasa mwelekeo wako ni wa kuserereka - serikali bado inakopa. Inaonekana unapenda kuwasilisha takwimu za mwezi badala ya kuwa na a holistic presentation of facts. Sio wakati wote takwimu za mwezi zinasema ukweli wote, na unachofanya ni kujaribu kuchukua kasampo cha mwezi kurubuni watanzania wa "Twaweza" lakini sisi wa "Tunaweza" tupo imara na tutawasaidia waelewe nini kinaendelea.
Deni la taifa limegawanyika katika sehemu mbili kuu namely deni la ndani na deni la nje. Tuanze kujadili deni la ndani kisha tutaenda kwenye deni la nje. Tukae kwenye hoja moja kabla ya kurukia nyingine kwani unachofanya hapa ni kuja na ujanja janja wa kusukumiza takwimu and flawed analysis kuwapendezesha waliokutuma kazi huko CCM kwa imani kwamba wale watanzania 1/4 wenye matatizo ya akili wataridhika na kinachoendelea.
Deni la ndani linaratibiwa moja kwa moja na Benki Kuu (BOT), tofauti na Deni la nje ambalo linaratibiwa na Wizata fa Fedha, pale ambapo Magufuli amemteua binamu yake mwenye uzoefu wa miaka michache ya uhasibu ofisi ya wakala wa majengo wa mkoa wa Dar-es-salaam, kuwa Katibu Mkuu.
Deni la ndani linahusisha amana za serikali (government securities) zinazouzwa kwenye soko la ndani la deni la taifa (Domestic Debt Market) kupitia minada maalum inayoratibiwa na Benki Kuu (BOT). Chini ya Serikali hii ambayo tunaambiwa ni transparent, hakuna maelezo yoyote Serikali inakopa ndani kwa lengo la kufanyia nini hizo fedha. Hii ni tofauti na nchi nyingine, hata hapo majirani Kenya ambapo any domestic debt raised inaendana na taarifa kwenye magezeti zinaenda kutumika kwenye nini - item by item.
Kwa Takwimu zilizopo (nenda kwenye Website ya BOT fuata link ya regular publications'), deni la ndani lipo katika hali ifuatayo:
Kufikia July 2015, deni la ndani lilikuwa ni takriban TZS 7.5 Trillioni. Mwaka mmoja baadae - yani kufikia July 2016, deni la ndani lilifikia TZS 10.1 Trilioni. Kwa maana hii, kati ya Mwezi July 2015 na Mwezi July 2016, deni la ndani limekuwa kwa kiasi cha takriban TZS 2.6 trilioni.
Tufananishe utawala wa JPM na JK:
Mnamo July 2014, deni la ndani lilifikia TZS Trilioni 6.8. Mwaka mmoja baadae - yani kufikia July 2015, deni hilo liliongezeka na kufikia TZS Trilioni 7.5. Kwa maana, katika kipindi hiki, deni la ndani lilikuwa kwa kwa kiasi cha takriban TZS Bilioni 740.
Kufikia hapa tunaona nini?
Linapokuja suala zima la deni la ndani, Serikali ya Magufuli inakopa zaidi ndani kuliko ilivyokuwa chini ya Serikali ya Kikwete. Je kufikia hapa, unaweza kutusaidia kuondoa kauli kwamba:
-Serikali ya Magufuli imeacha kukopa?
-Tukichukua sample ya 2014/15 & 2015/15, Serikali ya Magufuli inakopa kwa kasi zaidi kutoka vyanzo vya ndani kuliko ya Kikwete?
-Serikali ya Magufuli haipo transparent inakopa fedha kutoka vyanzo vya ndani kufanyia nini chenye manufaa kwa walipa madeni (wananchi walio wengi)?
Tafadhali bakia kwenye mjadala wa deni la ndani tuumalize halafu tutaingia kwenye mjadala wa deni la nje. Usituchanganye kisa ujira wa CCM.