Elections 2010 Magazeti haya ni wakala wa CCM

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi 2010 nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana uandishi wa habari kwenye magazeti yanayochapishwa hapa nchini ili kuona ni kiasi gani yamejikita katika kuandika habari zilizo balanced na bila upendeleo kwa wagombea au chama fulani (kama inavyotakiwa kitaaluma). Lakini nimebaini kuwa magazeti yafuatayo yamejidhihirisha wazi kuwa ni wakala wa chama tawala na yamekuwa yakitumiwa kikamilifu kama vyombo vya propaganda vya CCM. :violin:: Daily News/Sunday News, Habari Leo (magazeti ya serikali), Mtanzania, Rai (magazeti ya Rostam Aziz) Sauti Huru (gazeti la Subash Patel) , Tazama (linafadhiliwa na Lowassa). Katika kundi hili pia kuna stesheni za TV za Channel 10 na TBC1 ambazo zina uhusiano wa karibu sana na mafisadi. Ukifuatlia taarifa za vyombo hivi utagundua kwamba vimekuwa vikitumika kupotosha ukweli unaozungumzwa na vyama vya upinzani (hasa Chadema). Mfano ni jinsi walivyopotosha kile alichokisema Marando pale Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chadema kuhusu wizi wa EPA na kudai ni MATUSI na CHUKI, ingawa sisi tuliokuwepo Jangwani na wale waliomsikiliza Marando watakubaliana nami kwamba tamko lile linahitaji tu uthibitisho (Marando yupo tayari kuthibitisha) na kamwe sio tusi. Taaluma ya habari inataka chombo chochote kinachodhani kinaunga mkono chama fulani cha siasa katika uchaguzi kutangaza waziwazi msimamo wake ili wasomaji au wasikilizaji wajue mapema kuwa habari zitakazoandikwa au kutangazwa na chombo hicho zitakuwa ni za kuunga mkono upande fulani. Lakini hii ni kwa vyombo vilivyo independent na sio vyombo vya umma kama Daily News/Sunday News au TBC. Hawa wanapaswa kuwa impartial na sio vinginevyo. Sijui kama watendaji wa vyombo hivi wanatambua wajibu wao huo!
 
mhaririri wa habari corporation Muhingo Rweyemamu ndi mratibu wa Habari wa kampeni za CCM unategemea katika hali hiyo na njaa za pale HC wataandika nini chema kwa vyama vingine zaidi ya kupendelea mabwana wao walioko CCM
 
vyombo vyo habari hivi naona vitaendelea kupotosha watu wasio na uelewa kama akina kibonde
Nilitaka kusema na Clouds FM unaiacha wapi? Wao wanafagilia CCM kiaina. Whatever CCM or JK says is taken as a gospel truth by people like Kibonde. How weird!
Kusema kweli mimi sijaona Marando katukana wapi. Anachosema ni kwamba walioko mahakamani ni wachache bado wengine na baadhi yao wamo vigogo na anaweza kudhibitisha. Why do CCM call the bluff and ask Marondo to substantiate his allegations? Matusi yako wapi hapa?
 
You are right! Kwanini CCM hawamtaki Marando ku-substantiate claims zake na badala yake wanasema amemtukana mgombea wao? Wanajua kwa nini hawawezi kuchukua hatua kwa sababu amewashika pabaya. Si Rostam, Mkapa wala JK anayeweza kuukana ukweli huu.
Naamini wapiganaji hawa wana mengi zaidi ya EPA. Ngoja tusubiri.
 
huu ni wakati wa kampeni bila shaka chama hicho kimelipia matangazo hayo. ningeshauri na vyama vya upinzani navyo vilipie matangazo.
 
tehe tehe he he he...!
simple minded people discuss people/objects...!
bila shaka wewe ni yule yesu msukule wa bongo. kazi ipo!

MWAKA HUU mtaangaika saaana na avatar yako itakusaidia kwenda kwa sheih Yahaya

Kazi ipo
 
You are right! Kwanini CCM hawamtaki Marando ku-substantiate claims zake na badala yake wanasema amemtukana mgombea wao? Wanajua kwa nini hawawezi kuchukua hatua kwa sababu amewashika pabaya. Si Rostam, Mkapa wala JK anayeweza kuukana ukweli huu.
Naamini wapiganaji hawa wana mengi zaidi ya EPA. Ngoja tusubiri.

Walijua tu safari hii watabanwa kwenye issue hizi za EPA ndio maana kwa kutumia Puppet wao yaani NEC wakaamua kuwatega wapinzani kwa kuwalazimisha kusaini walichoita "maadili ya vyama", ukisoma hayo maadili yote yamelenga kufanya maisha kuwa rahisi kwa CCM!
 
khah!!! kumbe we ni mlozi!!
Tokeni hapa ukumbini nendeni ****** mkazozane. Waacheni watu wajadili hoja.
Vyombo vya habari vinaposahau maadili vina wajibu wa kukumbushwa. Hata kama wanalipia matangazo sio vipindi kama taarifa za habari na makala zinazowahusu watu wote. Nijuavyo kuna utaratibu wa kufikisha suala hili kwenye vyombo husika. hata wale wanaofuatilia uadilifu wa vyombo hivi, shime mlinukuu hili na historia imeshaandika
TBC wasilalamike eti tumefanyiwa fujo bila kusahau ushabiki wao katika siasa ndio umewafikisha hapo. Jaalia Lipumba ameshinda, wataweka wapi sura zao?
kabla hujaruka agana na nyonga
 
Mkuu Mzee Punch, heshima kwako. Observations zako ni sahihi kabisa kwani kinachofanywa na vyombo hivyo vya habari pamoja na waandishi wao ni aibu kubwa na udhalilishji wa tasnia nzima ya habari. Waandishi wamekuwa wapambe wa CCM na bila aibu wanatetea kuvalishwa vizibao, kofia na fulana za CCM pamoja nakutumia kalamu na notebook za CCM.

Hakuna cha ME, mwandishi mwandamizi wala mhariri waliomo kwenye huo msafara wa JK mwenye kufuata maadili ya uandishi wa habari, baadhi hushiriki hata kushangilia. Ni mwandishi mmoja tu, yule wa Mwananchi, aliye huru, hatumii hivyo vifaa vya CCM na muda mwingi unamuona yuko peke yake, au waandishi wa Mbeya ambao walikataa hata gari wanalotumia kuwekwa mabango ya CCM.

Hali halisi inasikitisha, ni kujikomba kwa kwenda mbele!
 
Tokeni hapa ukumbini nendeni ****** mkazozane. Waacheni watu wajadili hoja.
Vyombo vya habari vinaposahau maadili vina wajibu wa kukumbushwa. Hata kama wanalipia matangazo sio vipindi kama taarifa za habari na makala zinazowahusu watu wote. Nijuavyo kuna utaratibu wa kufikisha suala hili kwenye vyombo husika. hata wale wanaofuatilia uadilifu wa vyombo hivi, shime mlinukuu hili na historia imeshaandika
TBC wasilalamike eti tumefanyiwa fujo bila kusahau ushabiki wao katika siasa ndio umewafikisha hapo. Jaalia Lipumba ameshinda, wataweka wapi sura zao?
kabla hujaruka agana na nyonga

umenena.
 
kwenye Orodha ya mzee punch umeacha ITV,Radi One, Nipashe , Star TV, NA Radio Free Afrika.
 
Mnashangaza kama news ina msifu padre slaa.....basi gazeti hilo poa...kama ..akipondwa ...basi......mnalalama........mambooo badooooooo....jk hakuna anamweza kwa sasa hapa tz......hata mfanye nini....
  • ni mtu wa watu
  • mstaarabu
  • amelelewa
  • hapayuki hovyo
  • hana mihemko kama slaa
  • anakubalika dunia nzima
  • anakubalika tanzania nzima
  • anajali raia wake
  • amefanya raia wanajua haki zao sasa kuliko wakati wowote ule
  • amefanya police force imekua na nidhamu
  • ni mwerevu
  • ni msikivu
  • anapenda michezo
  • anapenda maendelea ya raia wake sio mchoyo
  • ameonesha mfano wa kubuni mambo mazito kama kilimo kwanza
  • malaria haikubaliki
  • tanzania inawezekana bila ya ukimwi
  • dodoma university ni kielelezo cha ubunifu na mipango thabiti
  • na ameahidi kujenga butiama university
  • ameweza kutuliza mambo zanzibar sasa hatusikii vifaru kupelekwa huko..hata nyerere yalimshinda ya huko
  • sasa ni nadra kusikia virungu na mabomu ya ffu
  • amewapa hali nzuri machinga kujitegemea na kuwapatia sehemu nzuri za biashara
  • ameweza kuwafikisha baadhi ya maafisa na mawaziri mahakamani kwa tuhuma za ubadhirifu..haijawahi kutokea
  • amesaidia kuweka chati ya tanzania juu kisiasa, kimichezo,na kiuchumi,
  • ameweza kuleta mkutano wa world economic forum hapa bongo kwa mara ya kwanza...mkutano huu ulitangazwa dunia nzima ..na faida yake ipo wazi....investments nyingi zimepatikana
  • ana aminiwa na nchi jirani....ndugu zetu wakenya walimtaka apatanishe....na akafanikiwa....
  • hapa shule zimeengezeka na wanafunzi wameengezeka
  • ni msema kweli.....alipowambia wafanya kazi wasitumiwe na wanasiasa bali serikali inaangalia kupandisha mishahara yao kwa kuangalia uwezo wa serikali walimwelewa..kwa ufupi anakubalika.......
 
mnatuchanganya, kwani mijadala ya humu ni kumponda jk na ccm yake na kumsifia slaa na chadema yao
 
JK, kwisha habari yake, nasikia hali ya afya yake imetetereka karejeshwa tena Dar bila kutegemewa.
 
Back
Top Bottom