Magari ya Kijapan

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Ukifika Tanzania magari mengi yanayoonekana barabarani kuanzia ya serikali hadi ya watu binafsi ni ya Kijapan. Ni vigumu saana kuelewa kwanini baadhi ya magari mengine hayapo kabisa au lipo mojamoja. Mfano zamani gari kama Peugeot zilikuwa nyingi lakini sasa hivi ni shida saana kuziona.

Gari za FIAT pia nazo zinapungua, wengi na sijui kwanini tumekuwa tukipenda kuagiza magari ya Kijapan. Huenda wengi watajibu spea zake zinapatikana kwa urahisi.

Zinapatikana kwa urahisi kwa sababu ndio magari yaliyojaa katika barabara zetu. Hapa sizungumzii ubora la hasha bali ni kuona namna tunavyokosa fursa ya kupata magari aina nyingine ambayo ni nafuu kuliko hayo ya Kijapan km Vauxhaul etc.

Lengo la maandishi haya ni kutoa angalizo kwa wale ambao wanatarajia kuanzia magari kutoka Japan miezi kadhaa ijayo. Itakumbukwa kuwa Japan ilikumbwa na yale maafa makubwa na hivyo kusababisha uzalishaji kusuasua hasa wa parts na hivyo kupunguza uzalishaji wa magari kwa kiasi kikubwa, Japani kwenyewe na nchi nyinginezo.

Kwa hiyo inamaana kuwa watu sasa hivi huenda wakanunua magari ya Kijapan kwa bei kubwa kwa sababu uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa saana. Kwamaana hiyo wale wanaouza secondhand nao wataaamua kukaa nayo na hata wakisema wauze inamaana demand yake itakuwa kubwa na bei kubwa.

Na pia pesa yako bado inanguvu saana na Tsh imeporomoka vilivyo.
Hivyo kuna haja ya kufikiria brand zinyingine za magari hasa ambazo zimeshaanza kuonekana mjini.
 
Mkuu hapa mtu si unafanya window shopping tu kwenye mtandao kisha unafahamu wapi waweza kupata gairi kwa bei rahisi? Wala haina shida kama unavyofikiria.
 
Ukifika Tanzania magari mengi yanayoonekana barabarani kuanzia ya serikali hadi ya watu binafsi ni ya Kijapan. Ni vigumu saana kuelewa kwanini baadhi ya magari mengine hayapo kabisa au lipo mojamoja. Mfano zamani gari kama Peugeot zilikuwa nyingi lakini sasa hivi ni shida saana kuziona. Gari za FIAT pia nazo zinapungua. Wengi na sijui kwanini tumekuwa tukipenda kuagiza magari ya Kijapan. Huenda wengi watajibu spea zake zinapatikana kwa urahisi. Zinapatikana kwa urahisi kwa sababu ndio magari yaliyojaa katika barabara zetu. Hapa sizungumzii ubora la hasha bali ni kuona namna tunavyokosa fursa ya kupata magari aina nyingine ambaye ni nafuu kuliko hayo ya Kijapan km Vauxhaul etc.
Lengo la maandishi haya ni kutoa angalizo kwa wale ambao wanatarajia kuanzia magari kutoka Japan miezi kadhaa ijayo. Itakumbukwa kuwa Japan ilikumbwa na yale maafa makubwa na hivyo kusababisha uzalishaji kusuasua hasa wa parts na hivyo kupunguza uzalishaji wa magari kwa kiasi kikubwa, Japani kwenyewe na nchi nyinginezo. Kwahiyo inamaana kuwa watu sasa hivi huenda wakanunua magari ya Kijapan kwa bei kubwa kwa sababu uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa saana. Kwamaana hiyo wale wanaouza secondhand nao wataaamua kukaa nayo na hata wakisema wauze inamaana demand yake itakuwa kubwa na bei kubwa. Na pia pesa yako bado inanguvu saana na Tsh imeporomoka vilivyo.
Hivyo kuna haja ya kufikiria brand zinyingine za magari hasa ambazo zimeshaanza kuonekana mjini

nahisi kuna mantiki flani katika usemayo.. nimeshuhudia hata katika miradi nyingi ya wafadhili hapa bongo... hela ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 ni kama imepungua kwa sababu ya mtikisiko wa uchumi. nchi nyingi zajaribu kurejea kati uchumi imara... ni muhimu kawaza unapohitaji kununua vitu vya gharama toka nje kwakweli...
 
2kizungumzia mambo ya spear hakika kuna baadhi ya magari hapa Kwe2 ni mpk u2me ama Japan yenyewe ama kwa hawa jrn ze2 wa Kenya na haya yote yanasababishwa na ndg ze2 kuwa Mapapa kwenye vyanzo vya Mapato kwani unaweza2ma spear toka huko lkn ukifikisha zinakwamia bandari na kuwa uchafu kisa wanataka pesa mara dufu ya uliyonunua. Ukizingatia hata wao wenyewe wana magari ya si ajabu wakanunua baadae hizo spear lakini wanamind fedha balaa. Mi nilitaka kufanya hiyo biashara lakini baada ya kupata mahesabu hayo nikagairi kbs. Yani we acha2
 
Mkuu hapa mtu si unafanya window shopping tu kwenye mtandao kisha unafahamu wapi waweza kupata gairi kwa bei rahisi? Wala haina shida kama unavyofikiria.
Nadhani unahitaji kusoma tena nilichoandika. Vinginevyo utakuwa unafanya tu window shopping. Nimeandika kwa wale ambao wako cost sensitive na kuwashauri kufikiria wigo mwingine maana huko mbeleni huenda hawataweza hata kununua magari tena.
 
Hapana mkuu, amejitahidi kuchangia hoja yako-usimuonee. Ukweli ni kwamba wengi wa wanaonunua magari wako sensitive kabla hawajanunua na ukweli utabaki kwamba hayo magari ya kijapani yanaendeshwa sana siyo Tz pekee-ni all-over Africa, Amerika kaskazini na kwingineko kwa kuwa yako durable, affordable na stable kwa mazingira yetu.

Pia pamoja na tetemeko lililotokea kumbuka kwamba nchi zilizoendelea hususan Japan zina-intervene mno sekta zinazoimarisha uchumi wao ikiwa pamoja na sekta ya magari kwa japan.

So serikali ya Japan imeshachukua hatua madhubuti kuakikisha kuwa sekta hiyo inaendelea kuwa world leading window shopping and buying.

Magari ya Ulaya mengi yao yametengenezwa kufit environment ya ulaya na ghali mno kutokana na production cost ya kuzalisha gari ulaya kuliko Japan, China na India.

Plz come again with concrete and constructive idea ya thread yako kwani pia ina nia njema kwa watanzania but-plz re-arrange as appropriate.
 
Labda tutaje magari ya Kijapan ambayo ni common Tanzania. Kuna Honda, Toyota na NIssan. Haya ndio maarufu. Ya nchi nyingine kuna;, kuna BMW, benz, kuna audi, Lexus, Peugeot, Vauxhal, Landrover etc. Nikikurudisha nyuma. Utakumbuka miaka ya nyuma namna gari aina ya pijo na landrover zilivyokuwa zimejaa. Unataka kuniambia gari zile zilikuwa hazihimili mikikimikiki ya Tz? Pia fanya zoezi rahisi, hebu angalia bodi ya magari mengi ya Kijapan yanayotoka Ulaya na yale ya Japan moja kwa moja. Hoja ya kwamba serikali inaprotect sekta zake ni sahihi, lakini Japan sasa hivi kuna matatizo. Mfano Toyota wamesema uzalishaji wao utapungua kwa karibu 50% mwaka huu kwa kukosekana kwa parts na makampuni mengine pia ya huko yamesema hivyo. Financial report yao ya March imeonyesha sales imeshuka kwa 30%.
Pia nadhani wewe ndio unahitaji kufanya research ya hii kitu. Ingia online angalia bei za magari wanayoyatumia Watanzania wengi kisha useme ya wapi ni ghali.
 
Mjihadhari na hayo magari ya Kijapan sasa, yasije kuwa na mihonzi hatari ya nyuklia mkasababisha maafa kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia zenu.
 
Back
Top Bottom