Anfaal
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 1,154
- 114
Ukifika Tanzania magari mengi yanayoonekana barabarani kuanzia ya serikali hadi ya watu binafsi ni ya Kijapan. Ni vigumu saana kuelewa kwanini baadhi ya magari mengine hayapo kabisa au lipo mojamoja. Mfano zamani gari kama Peugeot zilikuwa nyingi lakini sasa hivi ni shida saana kuziona.
Gari za FIAT pia nazo zinapungua, wengi na sijui kwanini tumekuwa tukipenda kuagiza magari ya Kijapan. Huenda wengi watajibu spea zake zinapatikana kwa urahisi.
Zinapatikana kwa urahisi kwa sababu ndio magari yaliyojaa katika barabara zetu. Hapa sizungumzii ubora la hasha bali ni kuona namna tunavyokosa fursa ya kupata magari aina nyingine ambayo ni nafuu kuliko hayo ya Kijapan km Vauxhaul etc.
Lengo la maandishi haya ni kutoa angalizo kwa wale ambao wanatarajia kuanzia magari kutoka Japan miezi kadhaa ijayo. Itakumbukwa kuwa Japan ilikumbwa na yale maafa makubwa na hivyo kusababisha uzalishaji kusuasua hasa wa parts na hivyo kupunguza uzalishaji wa magari kwa kiasi kikubwa, Japani kwenyewe na nchi nyinginezo.
Kwa hiyo inamaana kuwa watu sasa hivi huenda wakanunua magari ya Kijapan kwa bei kubwa kwa sababu uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa saana. Kwamaana hiyo wale wanaouza secondhand nao wataaamua kukaa nayo na hata wakisema wauze inamaana demand yake itakuwa kubwa na bei kubwa.
Na pia pesa yako bado inanguvu saana na Tsh imeporomoka vilivyo.
Hivyo kuna haja ya kufikiria brand zinyingine za magari hasa ambazo zimeshaanza kuonekana mjini.