Mafuriko Dar: Vi wapi vikosi vya jeshi wanamaji vilivyoonyeshwa kwenye Miaka 50 ya uhuru?

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Katika kilele cha maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru tarehe 9 December mwaka huu tuliona vikosi vya jeshi la majini vikipita kwa bashasha na mbwembwe nyingi mbele ya Rais kitu kilichotupa moyo kuwa maisha yetu yapo salama. Sasa yametokea mafuriko Jijini Dar es salaam mbona hatuvioni vikosi vile kwenda kuokoa watanzania wanaoangamia kwenye hili janga?
 
....Wanasubiri Watanganyika waandamane ili waje kutoa mkong'oto ili kuendelea kulinda madaraka ya Jemedari wao wa Serikali taahira.
 
inawezekana haupo tanzania.jeshi kwa kushirikiana na red cross wameSaidia sana na wameokoa maisha na mali za watu wengi sana.mi nadhani ungeuliza ile helkopta ya mbowe na ya magamba zilokuwa igunga leo ziko wapi?
 
....Wanasubiri Watanganyika waandamane ili waje kutoa mkong'oto ili kuendelea kulinda madaraka ya Jemedari wao wa Serikali taahira.
haya maneno ni sawa kile kiungo kinachotumika mtu akibanwa na haja kubwa.
 
Hata spice irelander ilipozama wanamaji wa jeshi hawakuonekana kuokoa zaidi ya wavuvi, jeshi nalo kama polisi wapo kulinda maslahi ya wakubwa na mafisadi wananchi wa kawaida hawana mpango nao zaidi ya kujisaua
 
inawezekana haupo tanzania.jeshi kwa kushirikiana na red cross wameSaidia sana na wameokoa maisha na mali za watu wengi sana.mi nadhani ungeuliza ile helkopta ya mbowe na ya magamba zilokuwa igunga leo ziko wapi?
Hata ukiwa na helkopta 10 kama huna vifaa na watu wenye ujuzi na uokozi ni kazi bure, sana sana utaua watu, nawasifu CHADEMA walipeleka helkopta kwa Babu Samunge japo walitapeliwa, kulikuwa na nia njema
 
haya maneno ni sawa kile kiungo kinachotumika mtu akibanwa na haja kubwa.

Hahahahahah lol! Una uwezo mdogo sana wa kuchanganua mambo....Kama leo hii kungekuwa na maandamano ya kuipinga Serikali, FFU na polisi wangemwaga kwa fujo ili kutoa mkong'oto na kuwapa majeraha Watanganyika na si ajabu hata kuwaua. Yameshatokea haya kule Arusha, Mbeya, Tarime, Mwanza n.k. lakini kwenye haya maafa hatujaona juhudi za Serikali kuwamwaga FFU na polisi ili wawasaidie waathirika wote na labda kupunguza maafa. Fungua macho uache kuwa na uwezo finyu wa kuchanganua mambo kama wa Kikwete.
 
inawezekana haupo tanzania.jeshi kwa kushirikiana na red cross wameSaidia sana na wameokoa maisha na mali za watu wengi sana.mi nadhani ungeuliza ile helkopta ya mbowe na ya magamba zilokuwa igunga leo ziko wapi?

....tumeona picha chungu nzima zilizopigwa kuhusiana na mafuriko katika sehemu mbali mbali za jiji. Mbona hatujaona hata picha moja inayowaonyesha wanajeshi wakiwasaidia waathirika? au walikuwa wanasubiri mvua isimame ndio wakatoe msaada?
 
Bado uwezo wa hii nchi kwenye majanga ni mdogo mno.Kwa sabab hakuna bajet kwa ajil ya dharura au ni kidogo sana.Ingekuwa sherehe ungeiona Serikal yote na mbwembwe au kama ni kutafuta ulaj wangevaa kijan na njano kila mahal ila leo huwaon!Nawapongeza Watz kwa ujasir wao hata saa ya kufa!
 
Umefika wakati tutumie majeshi kwa dharura kama hizi. Sio kuongoza magari, kuongoza misafara, matamasha, Uchaguzi nk Nadhani Waziri mhusika inabidi ajiuzuru kwani ameshindwa kutimiza wajibu wake.
 
Kwa hali ya Dar, yaani mkuu wa mkoa ameshindwa kuomba msaada wa majeshi yetu kuja kuasaidia? huyu jamaa kwa nini wananchi wasimkatae? na serikali kuu kimia? hivi kwa nini haya mafuriko hayakuja Dec 9?
 
Wanadai kwamba...Wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele....Cha ajabu hawajatoa ufafanuzi wa lipi walilothubutu, lipi waliloliweza na wanasonga mbele kwenye mambo yepi!? Ni usanii wa hali ya juu kila kukicha!!!!
 
ohhh, vijana wetu hawa hapa wakifanya mambo
 
Attachments

  • Askari wa kikosi cha Uokoaji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakitoa msaada kwa watu w.jpg
    Askari wa kikosi cha Uokoaji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakitoa msaada kwa watu w.jpg
    55.5 KB · Views: 52
  • jwtz.JPG
    jwtz.JPG
    39.2 KB · Views: 39
...ni vigumu kupiga gwaride juu ya maji. Haikua rahisi na hawakufunzwa kuokoa zaidi ya kupiga ikibidi kuuwa.
 
Back
Top Bottom