Mafuriko Dar ni kipimo cha serikali ya JK...wameshikwa pabaya sana....

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Kelele nyingi zimepigwa na zitaendelea kupigwa juu ya mapungufu ya serikali hii ya awamu ya nne kwenye kushughulikia mafuriko na uharibifu uliotokana na mvua zinazonyesha dar.....tatizo kubwa likiwa jinsi ya kupambana na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya barabara na madaraja na pia makazi ya watu. Kama tujuavyo resources zoote zitakazotumika(pamoja na kuwa kutakuwa na misaada)zitahitaji PESA na tunajua kumeshakuwa na kilio kinachoendelea juu ya suala hili la upungufu mkubwa wa PESA serikalini katika kushughulikia uendeshaji wa shughuli zake za kila siku.Watu watasema kuwa hawa jamaa (serikali)pesa wanayo ya kushughulikia maafa lakini napata kigugumizi kuamini kama kweli hizo pesa za maafa kweli zipo!!!.......tunaweza kubaki tunapiga kelele kuwa oh serikali imechelewa kuchukua hatua.......pasipo kujua je PESA ya maafa ipo????...kwa mtazamo wangu....serikali hii sasa wameshikwa pabaya kweli kweli kwenye kuwahudumia raia zake........tutafakari...
 
Hizo hela za maafa pengine ziko kwenye miradi binafsi zinatafuta faida.
lakini pia mwisho wa maafa matumizi hayaletwagi na kama yakiletwa sisahihi.
 
Nimesoma gazeti moja linasema serikali ya kikwete kwa sasa iko hoi haina pesa hao waanga wa mafuriko watasaidiwaje/ tunaona helikopter zikiishia kuzunguka hewani bila ya msaada wowote! kweli nchi yetu iko kwenye janga kubwa.
 
Hizo hela za maafa pengine ziko kwenye miradi binafsi zinatafuta faida.
lakini pia mwisho wa maafa matumizi hayaletwagi na kama yakiletwa sisahihi.

Pia matumizi yanaweza kuwa makubwa kuliko wangechukua taadhari mapema
 
Mh mh mh! Viongozi waliochaguliwa na walioiba kura sasa ni wakati mwafaka wa kukubali ukweli wa mambo kuwa mmeshindwa kutuongoza na kutujali kama raia wenu na mwaachie wengine wenye kuweza
 
Back
Top Bottom