Mafisadi - Ni ruksa kuwa mafisadi na Ushahidi wanao. Hakuna wakuwagusa. Chenge anajua.

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Wenzangu wana JF najua wengine mna hasira za ghafla lakini tujadiliane hili. Wakati Mheshimiwa Chenge akiwa Mwanasheria mkuu Katiba yetu ilifanyiwa marekebisho na yeye aksaini katiba ile ya mwaka 1977 ambayo tunatumia sasa. Kuna suala moja nategemea mnisaidie Katiba yetu inaruhusu mtu kumiliki mali na kulindiwa mali yake. Haizuii mtumishi wa umma amiliki kiasi gani. Kwa mawazo yangu naona jamaa(Mafisadi) hawana wasiwasi maana ushahidi huo hapo chini. Katiba yetu ibara hiyo :--


Haki ya kumiliki
mali
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
24​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi
zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya
hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya
kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria
ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
_____________
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977


Dar es Salaam, A.J.
CHENGE
1 Novemba, 2000 Mwanasheria Mkuu


Kwa hayo masharti yanayotajwa kuwa bila kuathiri masharti ya sheria za nchi, mie nadhani hawa jamaa wangeshtakiwa kwanza, maana ccm hadi inajivua magamba imekiri kuwa ni kuondoa mafisadi. Sasa kwa nini wasishtakiwe??? Pia wakataifishwa vitu vyao kama ilivyo sehemu ya haki hii. Vinginevyo kushtakiwa hawawezi hata kama wanafedha za kufa mtu kiasi cha kukifadhili chama. Maana Chenge mwenyewe anajua kumiliki mali ni haki yake ( hata kama kaiba maadam hajakamatwa) ni haki yake kuwa na vijisenti au majisenti maana hamna limit, RA ambaye anamiliki jimbo la Igunga na watu wake(ambao hatujasikia wanaandamana wala kumkanya mbunge wao maana inawezekana akichota huku anapeleka Igunga!!!!)awanajua wao. Mapacha hao wataishtaki ccm kuwataka watoe ushahidi. Chiligati kesha sema ccm hawana ushahidi wa ufisadi woote unaotajwa na hata J.K alisema Haijui DOWANS!!!.

Ili tuelewe somo, inabidi CCM iwatimue , pili wawashitaki kwa kuwa mafisadi na kuiba mali za wananchi maana wanamiliki mali zisizo halali ndio maana wamewaachisha ulaji CC, then wafilisiwe ili mali irudi kwa umma . Ila kumbuka ile Ibara inasema " ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya
kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria
ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili" Chenge mjanja. Wezi wadogo wadogo wako jela wengine walifungwa wakaachiwa kwa msamaha wa raisi kama Aden Rage wa Tabora wako wanapeta tu, Ila wezi , mafisadi ambao hadi nyinyi wenyewe mmewasusa ( maana kwa sasa linawanuka) mnakaa kimya . Wasiposhtakiwa na kuambiwa warudishe walicho kifisadi mtakuwa mnatuyeyusha.

Kuna jamaa yangu hapa anataka kunidanganya eti " Kikwete kaona hana fedha za kuilipa Dowans = (RA) sasa kaamua kumchinjia baharini ili selikali imuingize mjini RA. Nikamwambie thubutuuuuuu. Katiba yetu inasema ruksa kumiliki mali hata kama unamiliki Reli ya Kutoka Dar hadi Bukoba maadam uliyemwibia hajashtuka na wala hana ushahidi kama ambavyo J.K haijui Dowans. Kwa hiyo jamani Hiyo idhini ya sheria inayotajwa ya kutaifishwa mali ni kwa wengine. Reasoning yangu ni kwamba kama mmewatemesha uongozi na nyiie mkadai kuwa ni mafisadi na mmejivua gamba basi muwashtaki, vinginevyo inaonekana hii matrix ya gamba la anaconda mmeicheza wote. Naishia hapa ila kumbukeni maneno ya katiba hapo juu.

Hakuna limit kumiliki mali kiasi gani, maadam we Mtanzania kama RA na Chenge .​
 
Back
Top Bottom