Mafao ya wastaafu bado ni kero

ingipower

Member
Apr 3, 2012
86
37
Mafao ya wastaafu bado ni kero licha ya Mh Rais kutangaza kuwa amebatilisha asilimia 25, lakini cha kushangaza mstaafu aliyestaafu kuanzia mwezi wa 8, 2018 bado analipwa aslimia 25, Na malipo badala ya kulipwa kwa hundi yanaingizwa moja kwa moja kwenye banki husika , na ukienda kwenye mfuko wako eg PSPF unaambiwa andika barua, kwa mwajiri, je hii imekaaje? tunaomba ufafanuzi kwa jambo hili,
 
Na enaelekea kama kawaida yetu,viongozi wetu na sisi wenyewe tumeshasahau malipo ya mafao ya waliokuwa wafanyakazi wa EAC,Wazee wanakufa mmoja baada ya mwingine,na kijiwe chao pale central kimebaki kimya,Mungu anawaona wanasiasa wetu na tuelewe haya mafao haikuwa fedha ya serikali yetu,ila walipewa dhamana ya kuwalipa wazee hawa.ipo siku historia na muda vitakuja eleza ukweli nani ameiba mafao haya.
 
Kile alichosema Jiwe ilikuwa matangazo au promo? Nchi hii drama ni njingi kuliko unavyofikiria naamini watalipwa labda mambo hayajakaa Sawa. Tuko busy na korosho kwanza
 
Mafao ya wastaafu bado ni kero licha ya Mh Rais kutangaza kuwa amebatilisha asilimia 25, lakini cha kushangaza mstaafu aliyestaafu kuanzia mwezi wa 8, 2018 bado analipwa aslimia 25, Na malipo badala ya kulipwa kwa hundi yanaingizwa moja kwa moja kwenye banki husika , na ukienda kwenye mfuko wako eg PSPF unaambiwa andika barua, kwa mwajiri, je hii imekaaje? tunaomba ufafanuzi kwa jambo hili,
Hivi wewe ulimini zile kiki za kisiasa za raisi? Naona huwajui wanasiasa

Na huenda unaamini kuwa tuna hela ya ndani ya kutosha kujenga SGR, Stiegler Gorge, elimu bure, daraja jipya Sarenda nk?
 
Back
Top Bottom