Maeneo muhimu ambayo wataalamu wa Serikali wanapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo zidi makampuni ya mafuta na gesi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,331
8,254
Uvumbuzi wa rasilimali za mafuta na gesi huleta msisimko mkubwa sana katika taifa. Mataifa yenye utajiri wa rasilimali za mafuta na gesi hutafuta ushiriki wa makampuni ya kimataifa yenye rasilimali za fedha na utaalamu ili kusaidia kuzalisha mafuta na gesi iliyovumbuliwa.

Mara baada ya uvumbuzi serikali na makampuni ya mafuta na gesi huweka juhudi kubwa katika kuelewa masuala ya kiufundi na kibiashara kwaajili ya kuendeleza miradi ya mafuta na gesi iliyovumbuliwa. Hata hivyo, changamoto kubwa katika miradi ya mafuta na gesi kwa serikali huwa ni swala zima la majadiliano zidi ya makampuni yanayo onyesha nia ya kuwekeza.

Changamoto tajwa hapo juu huanza kuonekana, mara tu wataalamu wa upande wa serikali wanapoanza kufanya mazungumzo ya kujadili mikataba itakayotumika. Ukweli ni kwamba makampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi huwa yanakua na rasilimali nyingi za kifedha, ujuzi bora wa kutafuta maeneo yenye mafuta na gesi, na zaidi uzoefu katika mazungumzo ya mikataba.

Bahati mbaya nchi nyingi zenye rasilimali ya mafuta na gesi huwa na rasilimali chache za kifedha kuliko makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa. Kwa mfano, mapato ya kampuni Exxon Mobil ya dola bilioni 371 yalizidi pato lote la nchi ya Saudi Arabia lililokua na utajiri wa mafuta wa dolla bilioni 281. Unaweza kuona kwamba mazungumzo na kampuni yenye utajiri kama huo lazima yawe magumu sana.

Lakini mbali na hilo, makampuni ya mafuta na gesi huhamasika sana wakati wa mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi zidi ya wataalamu wa serikali. Makampuni hayo huzingatia sana gharama na uwekezaji waliofanya kwenye utafutaji wa mafuta na gesi na idadi ya visima vikavu vilivyopatikana. Hivyo macho yao yote wakati wa mazungumzo hutafuta zaidi kurejesha kwa haraka gharama walizotumia kwenye uwekezaji katika mazungumzo yoyote watakayofanya.

Lakini pia mbali na hilo makampuni hayo mara zote hukiri kwamba wao hupaswa kufanya kazi katika hali na mazingira magumu sana ya ufisadi na rushwa, ambayo huhitaji taasisi za kimataifa na serikali ambazo kampuni za mafuta na gesi zinakuazimewekeza wakati fulani ili kutoa msaada wa kisiasa.

Rais wa kampuni fulani huru ya mafuta na gesi aliwahikusema: "Tunapaswa kukabiliana na machafuko lakini kisha baadaye tunabasamu, hivyo tunapata pesa katika machafuko. Hivyo basi Makampuni ya mafuta na gesi mara zote hurekebisha mtindo wao wa mazungumzo kulingana na tafsiri zao za mazingira ya kisiasa ambayo hufanya kazi. Wakiwa wamezoea kushughulika na serikali za kimabavu au katika nchi zilizokumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, kampuni za mafuta na gesi mara nyingi huleta ulinzi binafsi, mtazamo usio na maelewano na wa kiburi kuelekea mazungumzo.

Je ni masuala gani muhimu hupaswa kuzingatiwa wakati wa mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi?

(1) Masuala ya kiufundi na biashara.
Masuala ya kiufundi na biashara ni mambo ambayo hutakiwa huzingatiwa sana. Mara nyingi hili ndilo eneo ambalo huwa na mgogoro wakati wa majadiliano. Kampuni nyingi za mafuta na gesi hutaka kulimiliki eneo hili. Na katika eneo hili mara nyingi kampuni huajili wataalamu waliohitimu katika eneo hili. Kiukweli asilimia 90-95% ya juhudi za majadiliano hutumika hapa kwenye eneo la kiufundi na biashara.

(2) Maswala ya kimazingira, kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Maswala ya kimazingira, kijamii, kiuchumi na kisiasa ni mambo ambayo hupuuzwa kwa kiasi wakati wa mazungumzo. Lakini masuala hayo ni muhimu sana pia wakati wa kujadili mikataba ya mafuta na gesi.

Imewahi kusisitizwa na mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta ya zamani ya kimataifa kwamba muda na juhudi kidogo sana hutumika katika upande wa watu wa mchakato wa kuendeleza mafuta na gesi, na matokeo yake ni kwamba hatari nyingi muhimu zaidi za mazungumzo na makubaliano yanayofuata hupuuzwa.

Hivyo mara nyingi kujadili mgawanyo sawa wa mali za mafuta na gesi na makampuni haya ya kimataifa huwa ni changamoto kubwa na huhitaji uwekezaji mkubwa wa muda na fedha katika kukusanya timu ya wataalamu wa kufanya mazungumzo. Hivyo wataalamu wa upande wa serikali wanatakiwa kujua masuala muhimu ya kujadiliana na makampuni haya kabla ya kuanza mazungumzo.

I.
Kiukweli macho mengi katika taifa lolote huwa kwenye mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi, sio tu yale ya pande mbili kuu yaani serikali na kampuni za mafuta na gesi zinazowekeza. Bali hata wamiliki wa ardhi pia mara nyingi jamii za wakazi ambao ardhi yao huathiriwa, wao pia hudai fidia kwa matumizi na usumbufu wa mali zao katika ardhi yao ambayo mradi utapita. Hili pia hutakiwa lizingatiwe sana, hata kama vikundi vya watu hao sio sehemu ya mchakato rasmi wa mazungumzo.

Wenyeji wa mahali mafuta na gesi ilipogunduliwa ambao hawawekwi kwenye orodha ya mambo ya kuzingatia kwenye mkataba wa mafuta na gesi, mara nyingi wao hudai sehemu yao kwa njia ya ajira na malipo ya fidia kwasababu ya mradi kuanzishwa kwenye eneo lao. Madai haya yatalazimika kushughulikiwa, na kutatuliwa kwa njia bora, kupitia mchakato wa kisiasa wa ndani ya nchi, na, ikiwezekana, kama sehemu ya mazungumzo ya jumla ya mkataba wa mafuta na gesi.

Na wakati wa mazungumzo makampuni ya mafuta na gesi mara nyingi hutoa ahadi maalum za kutoa mafunzo na kuajiri wazawa wa mahali hapo, na pia kusaidia jamii kwenye miradi ya maendeleo na mshikamano. Na hili swala ndilo la mwisho katika kile kinachoitwa maswala laini (au ya kijamii).

Kwa mapana zaidi, mijadala ya kisiasa kuhusu jinsi ya kutumia mali ya mafuta na gesi ambayo kiukweli bado huwa haijapatikana huendelea kutawala haraka masikioni na midomoni mwa watu ndani ya taifa, na hata kusababisha kuenea habari zisizo za kweli.

Si hivyo tu mashinikizo ya kisiasa hupelekea kudhoofika kwa mazungumzo yanayotarajiwa zidi ya makampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi kwa kubadili ratiba ambayo ni ya haraka ili kuharakisha mazungumzo. Hata hivyo kama historia ndio mwongozo mazungumzo ya mkataba wa mafuta na gesi mara nyingi huwa makali na huchukua muda mrefu.

Maeneo muhimu ambayo serikali zetu zinapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo yao zidi ya makampuni ya mafuta na gesi.

Yafuatayo ni maeneo muhimu ambayo serikali zetu zinapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo zidi makampuni ya mafuta na gesi.

(1) Ni nani anayepaswa kujadiliana, juu ya masuala gani, na mazingira gani ya taarifa, na kwa wakati gani.

(2) Vipengele kama vile muundo wa mkataba wa mafuta na gesi pia vinapaswa kuzingatiwa sana na serikali;

(3) Pia maswala ya viwango vya uhasibu;

(4) Jukumu la kusaidia miradi ya kijamii;

(5) Masuala ya afya na mazingira;

(6) Vifungu muhimu vya sheria vilisivyoweza kuingiliwa na mabadiriko ya kisiasa au mabadiriko ya sheria au sera na;

(7) Masharti ya kusitisha mkataba wa mafuta na gesi.


Nitaendelea................ Nikipata muda: (0747744895)


Zingatia sana hili:
Pamoja na kuongezeka kwa ushindani wa kimataifa wa kuchukua na kumiliki rasilimali za mafuta na gesi hasa kutoka kwa makampuni ya mafuta na gesi ya serikali, ambayo hutoa msaada wa serikali kwa urahisi kwa makampuni yanayotaka kuwekeza kwenye sekta ya mafuta na gesi na pia kutokana na wasiwasi mkubwa wa usalama wa nishati, haswa katika bara la Ulaya na Amerika, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwa mataifa yanayo miliki rasilimali za mafuta na gesi kuwa na ujuzi wa kitaalamu wa kujadili mikataba na makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa ambayo yatakubaliwa na kuheshimiwa baadaye na serikali zijazo za mataifa yetu.

Lakini mazingira haya mapya ya ushindani pia yatahitaji zaidi, uwazi kutoka kwa makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa katika mchakato mzima wa mazungumzo. Bila hivyo, mataifa yanayozalisha mafuta na gesi hayatakuwa na njia ya kujua ikiwa yanatendewa haki au la.
 
TAHADHARI yako mleta mada umechelewa Sana. Mikataba yote ya gesi ilishasainiwa tangu 2017
 
TAHADHARI yako mleta mada umechelewa Sana. Mikataba yote ya gesi ilishasainiwa tangu 2017
Hapana boss, gesi bado inaendelea kutafutwa kila mahali hapa nchini. Na mikataba bado inaendelea kujadiliwa mkataba mmojawapo ni huo wa LNG, kuna EACOP na n.k. Hili andiko haliwezi kuwa na expire date.
 
Ukiona majadiriano yanachetewa ujue inatafutwa account km ya escrow kwanza na angle ya kuvutia kamba.
 
Ukiona majadiriano yanachetewa ujue inatafutwa account km ya escrow kwanza na angle ya kuvutia kamba.
Boss majadiliano ya mikataba ya mafuta na gesi mara nyingi huchukua muda mrefu kwasababu ya ugumu wa vipengele vya mkataba. Mara nyingi vipengele vya mkataba vikiwa na masharti magumu lazima wachukue muda kuafikiana juu ya masharti hayo.

Lakini pia muda wa majadiliano ukiwa mrefu sana huwa unadhoofisha umakini wa wawashiriki wa pande zote mbili. Muda mwingine upande mmoja ukishachoka unaweza kuyakubali masharti ambayo mwazo ulikua haukubaliani nayo kwasababu ya muda kupotea. Na hilo sasa linaweza kuwa ni faida inayoweza kusubiriwa na upande mwingine yaani kusubiri uchoke ili ukubali mkataba kiurahisi.

Lakini pamoja na hilo thamani ya muda inapaswa kuzingatiwa sana wakati wa kujadili mkataba wa mafuta na gesi. Kwasababu kadiri majadiliano yanavyoendelea kuchukua muda mrefu, ndivyo gharama za kujadili zitakavyokuwa kubwa. Lakini bila kusahau kama nilivyo kudokeza hapo juu hamasa ya washiriki wa majadiliano ya kuleta ushirikiano itadhoofika kadri muda unavyosonga. Hivyo hadi makubaliano yaje yafikiwe, gharama za mazungumzo zinaweza kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Na mwishowe gharama zitakazotumika zitagawanywa kwa pande zote mbili, na mapato halisi yatakayo patikana kutoka na mafuta na gesi pia yatapunguzwa.

Hivyo, mara nyingi pande zote mbili hutarajia kufikia makubaliano haraka iwezekanavyo ili kuokoa muda na gharama.
 
Uvumbuzi wa rasilimali za mafuta na gesi huleta msisimko mkubwa sana katika taifa. Mataifa yenye utajiri wa rasilimali za mafuta na gesi hutafuta ushiriki wa makampuni ya kimataifa yenye rasilimali za fedha na utaalamu ili kusaidia kuzalisha mafuta na gesi iliyovumbuliwa.
ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwa mataifa yanayo miliki rasilimali za mafuta na gesi kuwa na ujuzi wa kitaalamu wa kujadili mikataba na makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa ambayo yatakubaliwa na kuheshimiwa baadaye na serikali zijazo za mataifa yetu.

Lakini mazingira haya mapya ya ushindani pia yatahitaji zaidi, uwazi kutoka kwa makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa katika mchakato mzima wa mazungumzo. Bila hivyo, mataifa yanayozalisha mafuta na gesi hayatakuwa na njia ya kujua ikiwa yanatendewa haki au la.
Mkuu Meneja Wa Makampuni , asante kwa hii, wewe ni baraka ubarikiwe sana!. Nlibahatika kuiona PSA moja ya gesi, kiukweli kabisa kwanza ilivyo kubwa tuu, inaonyesha TPDC wameletewa drafted document!, law firm inayoweza ku draft kitu kama hiyo ni Mkono, tena kwa sababu ina partners na wazungu!. Hili nililisema hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!
By then Tanzania tulikuwa hatuna Oil and Gas Law in Tanzania, sasa tunayo pale UDSM.
P
 
Mkuu Meneja Wa Makampuni , asante kwa hii, wewe ni baraka ubarikiwe sana!. Nlibahatika kuiona PSA moja ya gesi, kiukweli kabisa kwanza ilivyo kubwa tuu, inaonyesha TPDC wameletewa drafted document!, law firm inayoweza ku draft kitu kama hiyo ni Mkono, tena kwa sababu ina partners na wazungu!. Hili nililisema hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!
By then Tanzania tulikuwa hatuna Oil and Gas Law in Tanzania, sasa tunayo pale UDSM.
P
Ahsante sana boss Mayalla kwa mchango wako chanya.
 
Back
Top Bottom