Maelfu ya Wakenya waendelea kumiminika Dar kuangalia mechi ya Simba na Yanga

The best 007

JF-Expert Member
Oct 6, 2019
38,217
83,743
WIMBI la mashabiki wa soka kutoka Mombasa nchini Kenya wameendelea kumiminika Bongo, Tanzania kushuhudia mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ambayo imekua gumzo humu hapa Afrika mashariki na kati.

Mechi hiyo ambayo itapepetwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili imewavutia mashabiki ambao wameanza kuondoka Mombasa tangu Alhamisi kwa kutumia magari madogo pamoja na mabasi.

Mmoja wa maofisa wa kampuni ya mabasi ya Tawakal yanayofanya safari zake kutoka Mombasa kwenda Dar, Mudrick Mohamed Kassim, alisema amepokea wasafiri hususan vijana ambao wameondoka kuelekea Bongo kwa ajili ya mechi hiyo kubwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“Siku ya Alhamisi tumekuwa na vijana wengi walioondoka nikiwa nawasikia wakisema wanaelekea huko (Dar) kucheki mechi ya Yanga dhidi ya Simba. Ni uhakika tangu Alhamisi na Ijumaa tumepokea abiria wengi na ya kesho Jumamosi tumekaribia kujaza,” alisema Kassim.

Cc joto la jiwe babayao255 Sama boy 255 ichoboy01 NDINDA Mkwanzania chongchung Gwakagwaka 7seven

#mwanaspoti
#mwanaspotiupdates
#tunawezeshataifa
FB_IMG_16663689952214189.jpg
 
#tunawezeshataifaView attachment 2393902
Hahahaha, hawa watu tumewakamata kila eneo, baadae utasikia wanasema Kama sio wao hii Derby isingekua maarufu
 
Back
Top Bottom