Maelezo ya Brig. Gen. Al-Adawi kuhusu Dowans Feb 20/02/2011

ila watu wengine sijui upeo wao wa kufikiri unaishi wapi.
Hivi Tatizo la umeme lilivyokua sensitive kipindi kile, kila kiongozi anahaha kulitafutia uvumbuzi, halafu aje mtu ambaye ni rafiki wa mkuu wa nchi hii kutusaidia kutatua tatizo hilo na Richmond yake halafu Kikwete asimjue? Labda basi hili tatizo la Umeme lilikua halimhusu Kikwete!
usisumbuke na hao watu walio mamluki, wana macho lakini wanajifanya wao ni vipofu
nakwambia hao watakuwa wanapata benefit kutoka kwenye huo uongozi si bure
waambie wasubiri tu siku zikifika waajiandae pa kwenda kuishi
 
Nadhani mtanzania wa kweli na makini hawezi kusema tatizo la Dowans ni sam6. Huyu anahitaji kupimwa akili au maombi maalumu au la huyo mtu ni miongoni mwa mafisadi. The proble is clear, that is we don't have someone to lead us.

Tatizo la Dowans? Dowans wana tatizo au wa Tanzania wana tatizo la umeme na ufinyu wa akili? Hivi dowans wamekosa nini? Mitambo wameleta kwa kuikodisha na si kuiuza, mmeikataa, walipeni pesa zao kama ilivyo kwenye mkataba waondoke? Mlilazimishwa? Si mlivunja wenyewe mkataba, walipotaka kuiuza mkazuia mahakamani isiondoshwe, ilhali hamkuwalipa chochote! Nani mwenye tatizo hapo? Adawi kisha sema, mkilipa sawa, msilipe sawa, hii ni biashara kuna kupata na kuikosa. Haya sasa, nini zaidi? Msilipe achukuwe mitamboi yake, au kaeni nae chini mkubaliane kuinunua au kuikodisha. Yote ya nini? Ni wapi Dowans au Adawi wamedhumu au kutapeli au kuhujumu?
 
Tatizo unarukia mbali wewe, kwanza jibu swali langu hapo juu.
Tatizo la Dowans? Dowans wana tatizo au wa Tanzania wana tatizo la umeme na ufinyu wa akili? Hivi dowans wamekosa nini? Mitambo wameleta kwa kuikodisha na si kuiuza, mmeikataa, walipeni pesa zao kama ilivyo kwenye mkataba waondoke? Mlilazimishwa? Si mlivunja wenyewe mkataba, walipotaka kuiuza mkazuia mahakamani isiondoshwe, ilhali hamkuwalipa chochote! Nani mwenye tatizo hapo? Adawi kisha sema, mkilipa sawa, msilipe sawa, hii ni biashara kuna kupata na kuikosa. Haya sasa, nini zaidi? Msilipe achukuwe mitamboi yake, au kaeni nae chini mkubaliane kuinunua au kuikodisha. Yote ya nini? Ni wapi Dowans au Adawi wamedhumu au kutapeli au kuhujumu?
 
Dowans Ilitoka wapi?
Dowans imesajiliwa kisheria Tanzania na wamiliki wake wapo kwenye nyaraka za BRELA na wakurugenzi wake pia wapo wamesajiliwa na walishwekwa wazi na Waziri wa Nishati na nchi walizotoka zilitajwa.

Au ulifikiri kampuni zinaota kama mimea?

Kampuni ni mjumuiko wa watu zaidi ya mmoja au kampuni zaidi ya moja zikaungana zikafunguwa ya ama biashara ya faida ya ama si ya faida.
 
Authorization of 90bn to Rafiki

Tatizo hujui maana ya power of attorney. Na hata kama ni authorization, kwani wewe unajuwa wana biashara ngapi zingine? Au unafikiri biashara zao ni hako kamtambo walikoleta Ubungo? Ambapo kwetu hapa kanawasha mji mzima wakati kwa wenzetu hakatoshi hata mtaa mmoja.
 
Kwani kuna ubaya akiwa rafiki yake?

Kwani ni dhambi Kikwete kusema hawajui wamiliki wa dowans?

Je, wewe unajuwa mali zote za rafiki zako wachache ulio nao? Wachache sana kwani huna cv inayomkaribia JK, do you expect kuwa JK ajuwe kila kampuni ya rafiki zake? Kila mali ya rafiki zake? Duhh, unashangaza sana na hoja zako!

Naona malaria sugu karudi na ID nyingine, anyway, thanx for your useless comment!
 
So what wakiwa marafiki? Sikujuwa kwamba kwa mila za baadhi ya wa Tanzania ni Dhambi kwa Rais kuwa na rafiki Tajiri, Mbunge, International business man!

:confused: wewe ni jamii ya walibya wanaopata kila kitu cha muhimu katika maisha yao lakini wanadanganywa na wamarekani kisa wawaibie utajiri wa wa mafuta;watanzania tuna utajiri mkibwa sana viongozi wetu wanamarafiki matajiri wanaotuibia mali yetu,mambo yakijulikana wanawakana,huku sisi tunabakia masikini wa kutupwa duniani,Gaddafi anamarafiki matajiri sana lakini wote hao hawachezei mafuta yao.Ninakuhakikishia akiondolewa Gaddafi Libya hapatakalika tena,wamarekani wataingia kubeba mafuta yote ya akiba yaliyopo Libya.
Sasa sisi hatukatai marafiki lakini watuheshimu wasiibe mali yetu kwa kushirikiana na viongozi.
 
So what wakiwa marafiki? Sikujuwa kwamba kwa mila za baadhi ya wa Tanzania ni Dhambi kwa Rais kuwa na rafiki Tajiri, Mbunge, International business man!

Tatizo sio kuwa na marafiki matajiri, hiyo sisi haituhusu, shida inakuja pale ambapo kupitia urafiki huo mali zetu zinaibiwa na kuhujumiwa. Au mzee na wewe uko kwenye huo mgao wa bil. 94? manake napata shaka unapata wapi ujasiri wa kutetea ufirauni huu!
 
Tunatumia muda mrefu sana kujiuliza maswqli ya kuwasafisha Rostam na Lowassa ambao kwa makusudi kabisa wanataka Wadanganyika wamtazame Alawi kama mchawi hali wao wakiendelea kulipwa mabillioni ya fedha toka wakati wa Richmond hadi hii Dowans kwa uzalishaji wa megawatts kiduchu..wanaiua Tanesco kama walivyoua ATC, TRA na mashirika mengineyo. Ama kweli Miafrika ndivyo tuulivyo.

Ahsante mkuu,
Ulipotea muda. Anyway ilianza Richmond ghafla Dowans, ghafla Al adawi n.k. Hakuna utetezi wowote wa maana utakaotengenisha Richmond/Dowans, Utakaomsafisha Lowasa na Rostam. Tunajua kazi inaendelea na wapo watumishi usiku kucha.
Kwa myopic RA/EL wanaweza kutufikisha pale pa Al Mahd/ Farah aideed. Watch out these monsters!
 
Kwa muda sasa kumekuwa na malalamiko juu ya hii kampuni ya kufua umeme ya DOWANS.Yamesemwa mengi ya kuilalamikia kampuni hii.DOWANS imezalisha umeme kwa mujibu wa mkataba wake na tanesco.RICHMOND haikuwahi kuzalisha hata megawat 1.Nataka kujua ubaya au tatizo la dowans,wakati wao umeme wao ni nafuu zaidi kuliko wengine.Shida yetu ni umeme hawa wanazalisha sisi hatuwataki,nini tunataka.Mgao umekuwa mkubwa kwa kuzima umeme wao.Naomba nielezwe tatizo lao

Tatizo lake ni kama wewe na wengine wa aina yako mnavyotumiwa, kwa kujua au bila kujua lakini kwa maslahi pamoja ubinafsi wenu. Hili ndio tatizo lenyewe, watu wamenunuliwa kutoka sekta mbalimbali kupigia chapua dowans, sasa kwa nini iwe hivyo kama hamna tatizo, tatizo lipo ila rushwa imewatia watu upofu na ukizwi hawaoni wala hawasikii kuhusu dowans wameamua kuwa majuha wewe ukiwa mmoja wao.
 
Kwa muda sasa kumekuwa na malalamiko juu ya hii kampuni ya kufua umeme ya DOWANS.Yamesemwa mengi ya kuilalamikia kampuni hii.DOWANS imezalisha umeme kwa mujibu wa mkataba wake na tanesco.RICHMOND haikuwahi kuzalisha hata megawat 1.Nataka kujua ubaya au tatizo la dowans,wakati wao umeme wao ni nafuu zaidi kuliko wengine.Shida yetu ni umeme hawa wanazalisha sisi hatuwataki,nini tunataka.Mgao umekuwa mkubwa kwa kuzima umeme wao.Naomba nielezwe tatizo lao

WALA HATUKULAUMU! Umeingia humu JF wiki mbili zilizopita kama sehemu ya vile vifaa vinavyohitajika maliwatoni kwa ajili ya mradi wa kuwasafisha wanaonuka. Ni kama Nguruvi3 alivyosema, nyie mmeingia humu kuvuruga mijadala na kuleta hoja tasa ambazo kwa bahati mbaya hazitavuruga mwelekeo chanya tuliouchukua kuwalinda wale wanaonyonywa jasho na damu zao na hao unaojaribu kuwasafisha. Wewe unaishi nchi hii halafu unauliza ETI TATIZO LA DOWANS NI NINI? Kwa taarifa yako hakuna maji, sabuni, brashi wala manukato yatakayowatakasa hao wanyonyaji unaowatetea. Huo mradi wao wa urais 2015 labda waende igunga au monduli ndiyo wataufanikisha, siyo Tanzania yetu hii.
 
Mimi pia najiuliza swali hivi mbona Dowans tu I think something fishy here..... ina maana IPTL na Songas mikataba yake safi sana? ukiangalia viwango vya capacity charges Dowans wanachaji kiwango cha chini kulinganisha na Songas na IPTL na IPTL ina mkataba wa 20 years! kwanini tusiwazungumzie wote? Nashindwa kuelewa

Capacity carges
IPTL 300 mil
Songas 265 mil
Dowans 152 mil

Hizi takwimu umezipata wapi mkuu?
 
Wengi hufata mkumbo wa kurukia mambo wasioyajuwa. Huhamasishwa tu kwenye ujinga na kwa ujinga wao hukurupuka na kufata lisemwalo hata kama halipo.
Dowans hawana kosa hata moja, na wasuluhishi wa ICC wamepitia mkataba wao na Tanesco na wameamuwa walipwe. Hivi hawa ICC wanawapenda sana Dowans hata waamuwe walipwe? La, hasha, wameuona mkataba, wakaupitia kwa kina, wakaamuwa haki.

Hivi, kuna hata mmoja humu JF aliekuja na jibu kuwa Dowans walichokosa ni hiki hapa. Mimi sijaona, ukiwauliza Dowans wamekosa nini? Jibu huwa mzunguko usio na jibu la wazi.
 
Tatizo ni media circus na siasa za maji taka. Tatizo wabongo wakisikia jamaa wanavuta kama mil150 kwa siku wanaona jamaa wanafaidi lkn wanasahau yale majenereta yanatumia mafuta na siyo maji.
Na pia TNSCO wakituuzia huo umeme walikuwa wanapata faida kama mil 600 kwa mwezi.

Sahihisho...mitambo inatumia gesi(yetu) sio mafuta....TANESCO wanapata 20m kwa siku na hao jamaa wanchukua 150m? Plus capacity charge
 
Wengi hufata mkumbo wa kurukia mambo wasioyajuwa. Huhamasishwa tu kwenye ujinga na kwa ujinga wao hukurupuka na kufata lisemwalo hata kama halipo.
Dowans hawana kosa hata moja, na wasuluhishi wa ICC wamepitia mkataba wao na Tanesco na wameamuwa walipwe. Hivi hawa ICC wanawapenda sana Dowans hata waamuwe walipwe? La, hasha, wameuona mkataba, waupitia, wakaamuwa haki.

Hivi, kuna hata mmoja humu JF aliekuja na jibi kuwa Dowans walichokosa ni hiki hapa. Mimi sijaona, ukiwauliza Dowans wamekosa nini? Jibu huwa mzunguko usio na jibu la wazi.

kwa hiyo hata raisi wako aliyekutuma kuja huku jamvini kuchafua hali ya hewa unapingana naye ... JK ameshakiri kiini cha scandal ya DOWANS ni Richmond kampuni ambayo ameiita phantom company ..... inakuaje richmond ndiyo inachagua kampuni ya kurithi mkataba.. bado unaenedelea kubwabwaja kama vile wewe binafsi umenyimwa haki .... wewe nahisi si mtanzania ...kama ni mtanzania basi wewe ni mnafiki mkubwa na kuliko watu wote Tanzania ...tena unachuki ya hali ya juu .... unatetea DOWANS ambayo imenyonya na inataka kuchota pesa za wananchi ili waendelee kupata taabu ..... humu JF kuna characters za ajabu sana .... this is more than suicide bombers .... naweza kukufananisha na Mohamed Atta suicide hijacker American airline flight 11 ....twin tower attack sept 11

Mohamed_Atta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom