Maelezo ya Brig. Gen. Al-Adawi kuhusu Dowans Feb 20/02/2011

Dowans yataka mazungumzo na serikali



*Anayetajwa kuimiliki ajitokeza Dar
*Akiri kumpa Rostam nguvu ya kisheria


Na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA wa Oman anayetajwa kuwa ndiye mmiliki wa Kampuni ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited, Brigedia Jenerali (Mstaafu), Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi amejitokeza na kukiri kumiliki kampuni hiyo huku akiweka wazi kuwa iko tayari kwa na mazungumzo na serikali.

Al Adawi aliyezungumza na baadhi ya wahariri wa magazeti jijini Dar es Salaam kwa sharti la kutopigwa picha wala kurekodiwa na kamera za televisheni, alisema ameamua kujitokeza kutokana kuondoa kiwingu kilichokuwa kinaizunguka kampuni hiyo hasa kuhusu umiliki wake na akakiri kwamba alimpa Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz nguvu ya kisheria kuisimamia nchini.

"Mimi ndio mwenye hisa nyingi katika kampuni ya Dowans Holdings SA na kampuni yake tanzu ya Dowans Tanzania Limited...Nimekuja nchini kuweka sawa habari za upotoshaji kuhusu Dowans na kufahamu kama uwezekano wa kupata suluhisho la hali iliyopo," alisema.

Mfanyabiashara huyo aliambatana Bw. John Miles, aliyetambulishwa kama mwanasheria maarufu wa kimataifa ambaye amekuwa akiiwakilisha kampuni hiyo tangu ilipoingia katika mgogoro na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Bw. Stanly Munai aliyetajwa kama Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans Tanzania Limited, ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo waliotajwa na Waziri William Ngeleja Januari mwaka huu.

Mbali na Brigedia Jenerali Al Adawi, wengine waliotajwa ni Andrew James Tice kutoka Canada, Gopalakrishnam Balachandran wa India, Hon Sung Woo wa Malaysia, Guy Arthur Picard kutoka nchini Canada pamoja na Stanley Munai wa nchini Kenya.

Brigedia Jenerali Al Adawi alisema tangu kampuni hiyo ilipoanzishwa mwaka 2005 alikuwa amenuia kuwekeza katika mkongo wa mawasiliano katika nchi za Afrika Mashariki, lakini kwa kuwa yeye anaishi Muscat, Oman, alihitaji mtu wa kumwakilisha kufanikisha mpango wake, ndipo alipomchagua rafiki wake wa siku nyingi Bw. Rostam Aziz.

"Ili Bw. Aziz awe na mamlaka ya kutosha kusimamia kampuni yangu, mwaka huo wa 2005 nilimpa nguvu ya kisheria," alisema na kufafanua kuwa mpango huo ulibadilika baada ya kutokea mpango mpya wa mitambo ya kuzalisha umeme mwaka uliofuata.

Alisema Baada ya kampuni ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme, Septemba 2006, Bw. Aziz aliwasiliana naye akimwelezea tatizo la umeme akimshawishi awekeze kwenye umeme, akiamini kuwa mwekezaji anayetakiwa ni mwenye uwezo na anayeweza kufanya shughuli hiyo haraka.

"Mtakumbuka kuwa TANESCO iliomba kupitia kwenye vyombo vya habari mwekezaji mwenye uwezo wa kuzalisha kuanzia megawati 1 kuwasiliana nayo kuzalisha umeme wa dharura. Gridi ya taifa ilikuwa inaishiwa umeme kabisa.

"Hatimaye, Dowans ilifikia makubaliano na Richmond, kuwa kama TANESCO ingekubali kampuni yake ingechukua nafasi ya Richmond kuchukua mkataba wa kuzalisha umeme. Tuliamini kuwa Dowans ingepokewa vizuri na TANESCO, serikali na umma kama shujaa, kinachotushangaza haikuwa hivyo.

Alisema Dowans ililipa dola za Marekani milioni 109 (kwa ajili ya mitambo, vifaa vyake na wahandisi na baadaye kuongeza mtaji wa dola milioni 20.

Al Adawi alisema kuwa watu wasiokuwa taarifa sahihi wamekuwa wakiishutumu kampuni yake wakiita ya mfukoni, lakini yeye anawapa changamoto waoneshe kampuni nyingine ya mfukoni yenye mitambo ya dola za Marekani milioni 109.

Mfanyabiashara huyo alionekana kama anajibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikimtaja Bw. Aziz kuwa mtu mwenye mamlaka na Dowans, alisema wakati anaweka sawa kampuni yake nchini, alimwomba mbunge huyo ambaye ni rafiki yake amsaidie, pia aliwatumia wafanyakazi wa kampuni ya mbunge huyo, Caspian limited, ambao baadaye walikabidhi majukumu kwa wengine walioajiriwa na Dowans limited.

Akijibu maswali ya wahariri, mfanyabiashara huyo alisema kwa sasa ameitwa nchini na serikali kuzungumzia uwezekano wa kutumia mitambo yake kuzalisha umeme kuinusuru nchi na mgawo unaoendelea sasa.

Alipobanwa zaidi ni nani hasa serikali aliyemuita kuzungumza naye, alisema kwa sasa atazungumza na uongozi wa TANESCO kwa kuwa ndiyo inayohitaji umeme, huku akisisitiza kuwa kampuni yake imekuwa ikiuza umeme kwa gharama nafuu ya senti 4.99 kwa uniti moja, jambo ambalo anaweza kufanya hata sasa ikiwa wataelewana.

Kuhusu uwezekano wa kupunguza fidia iliyotolewa kwenye hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), alisema ikiwa serikali itazungumza hilo atakuwa tayari kusaidia kwa nia njema.

Alipoulizwa kwa nini ameamua kujitokeza yeye mwenyewe badala ya Bw. Aziz ambaye alishapewa nguvu ya kisheria, Brigedia Jenereli Al Adawi alisema ni kwa sababu kumekuwa na maneno juu ya mmiliki wa kampuni hiyo, hivyo amejitokeza ili kuonekana.

Alipoulizwa kama anataka kuonekana kwa nini hakutaka kupigwa picha za magazeti wala televisheni, alisema yeye ni mfanyabiashara asiyetaka kufahamika kwa kuwa si vizuri kufanya hivyo kwa mtu kama yeye anayemiliki mali nyingi, akitolea mfano India anakomiliki mitambo ya mabilioni lakini picha yake haijawahi kutokea kwenye magazeti.

Akizungumzia tuzo ya ICC, Al Adawi alisema baada ya hukumu hiyo, Dowans iliwaandikia TANESCO na serikali ili kufanya mazungumzo kutafuta maelewano kwa njia mbalimbali lakini haijajibiwa.
 
Huu ndio ubabe wa ccm. kweli wametuweza. Ikija kampeni wanamweka kinana. ikija kutuibia wanamweka rostam na lowassa. wakitaka kudanganya wanamleta mkwere na katibu wake....hahahaha
mimi nipo tayari kuchoma gamba. ivi hili ni kosa la jinai?
 
Waungwana tuliambiwa hii Dowans ina wamiliki sita Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenyan). Mbona huyu Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) anajitambulisha kama vile yeye ni mmiliki pekee wa Dowans? Huyo Stanley Munai (Kenyan) ametambulishwa kama Director of Finance. Kulikoni hadi ajitambulishe kama yeye ni mmiliki pekee wa Dowans? Hao wamiliki wengine nao wana mpango wa kuja nchini ili kushiriki katika kudai malipo yao? au wameingia mitini baada ya kuona kasheshe inazidi kuwa ngumu?
 
Waungwana tuliambiwa hii Dowans ina wamiliki sita Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenyan). Mbona huyu Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) anajitambulisha kama vile yeye ni mmiliki pekee wa Dowans? Huyo Stanley Munai (Kenyan) ametambulishwa kama Director of Finance. Kulikoni hadi ajitambulishe kama yeye ni mmiliki pekee wa Dowans? Hao wamiliki wengine nao wana mpango wa kuja nchini ili kushiriki katika kudai malipo yao? au wameingia mitini baada ya kuona kasheshe inazidi kuwa ngumu?

Wizi mtupu!
 
Habari wana jamvi.
Baada ya Waziri wa Nishati na Madini kutaja orodha ya "Wamiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans" mapema mwezi jana, nilibaki kutatizwa na maswali kadhaa kichwani mwangu:

1. Kwa nini Mh. Waziri amewataja watu hao mara baada ya hukumu ya ICC kutoka, na kipindi ambacho serikali pamoja na ccm wameonesha shauku ya hali ya juu ya kutaka kuilipa sh. 94 bilioni kampuni hii, licha ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, wasomi na wanaharakati juu ya uhalali wa "fidia" hiyo.

2. Utata wa wamiliki wa kampuni hii ulikuwepo tangu mwaka 2007 mara baada ya uchunguzi wa tume ya Mh. Mwakyembe juu ya sakata la Richmond, na katika kipindi hicho Mh. Ngeleja ndiye aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini. Mh. Ngeleja hakuwahi kuthubutu kuwaweka hadharani wamilki wa kampuni hiyo licha ya kutakiwa kufanya hivyo mara kadhaa. Badala yake kulionekana jitihada za makusudi za kulazimisha kufunga mijadala juu ya Richmond/Dowans na kuficha wamiliki wake.


3. Katika uchunguzi wa Tume ya Mh. Mwakyembe, kuna watu kadhaa walitajwa kuwa na uwezekano wa kuwa wamiliki wa Dowans. Miongoni mwao yumo Rostam Aziz. Cha ajabu ni kuwa hakuna hata mmoja katika orodha hii ya Mh. Ngeleja ambaye alitajwa kwenye ripoti ya tume ya Mh. Mwakyembe ambayo ilifanya uchunguzi wa kina wa kashfa hii. Orodha ya Mh. Ngeleja ni mpya kabisa.


4. Hakuna ushahidi unaoonesha kuwa hao waliotajwa na Mh. Ngeleja kuwa wamiliki wa Dowans ndio waliosajiliwa na Brela kama wamiliki halali wa kampuni hiyo. Hata picha zao hazipo huko.


5. Kwa nyakati tofauti tofauti walipotakiwa kuwataja wamiliki wa Dowans, wahusika kutoka mamlaka mbalimbali za serikali (Waziri Ngeleja akiwa mmojawapo) walitoa majibu yaliyolenga kuaminisha umma kuwa wamiliki wa Dowans hawajulikani.


6. Hata wakati anataja majina hayo ya "wamiliki wa Dowans", Mh. Ngeleja alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana kitu kilichotoa taswira kuwa ama Mh. Ngeleja hakuwa na uhakika na anachokizungumza au taarifa alizokuwa anazitoa hazikuwa sahihi.


7. Zaidi ya yote, jana amejitokeza mtu mwingine bw. Seleman Al-Adawi akijinadi kuwa yeye ni mmiliki wa Dowans tena kwa masharti ya kutopigwa picha, ajabu kubwa hii! mmiliki halali wa kampuni iliyokuja kututatulia tatizo halafu hataki umma umfahamu. Huenda kumiliki kampuni ya kufua umeme ni dhambi! Cha kushangaza ni kuwa jina la huyu bwana halimo kwenye orodha ya Mh. Ngeleja.

Kwa kuzingatia maswali hayo hapo juu niliamini kulikuwa na mazingira ya dhahiri shahiri kuwa wale waliotajwa na Mh. Ngeleja hawakuwa "Wamiliki wa Dowans".


Baada ya kutafakari kwa kina niliamua kufanya utafiti ili kuona kama kuna ukweli wa watu wale kuwa wamiliki wa Dowans. Nilibahatika kupata taarifa za watu wawili kati ya wale waliotajwa na Mh. Ngeleja kuwa ni "wamiliki wa Dowans".

Guy Picard (pronounced gii):
Huyu ni raia wa Canada. Alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza ama mwishoni miaka ya 90 au mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiiwakilisha kampuni ya AES Energy ya Marekani, kampuni ambayo ndiyo iliyoshinda zabuni ya uendelezaji wa mradi wa gesi ya Songosongo.



AES Energy ilikuja kuuzwa kwa kampuni ya CDC Globeleq na baadaye CDC ilikuja kuuza hisa zake zote kwa kampuni ya Globeleq Limited ya London Uingereza.



Kazi ya kampuni hii ilikuwa ni kujenga mtambo wa kuchimba na kusafisha gesi, kujenga bomba la kusafirishia gesi kutoka kisiwani Songosongo wilayani Kilwa hadi Dar es Salaam; vilevile kuendesha mtambo huo wa kuchimba na kusafishia gesi, bomba la kusafirishia gesi pamoja na kituo cha kuzalisha umeme wa gesi cha Songas. Kampuni hii ndiyo iliyokuwa ikimiliki hisa nyingi zaidi katika kampuni ya Songas. Wanahisa wengine katika kampuni ya Songas ni Tanesco, Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC) na FMO ya Uholanzi.


Baada ya kazi ya ujenzi wa mradi wa gesi ya songosongo kumalizika mwaka 2004, Guy Picard aliendelea kuwa mtumishi wa kampuni ya Songas na alikuwa katika cheo cha General Manager.



Aliachishwa kazi Disemba 2006 baada ya kubainika kuwa alifanya ubadhirifu mkubwa wa fedha ya kampuni. Taarifa zinadai kuwa kuachishwa kazi kwa Guy kulikuwa ni kwa aibu kubwa kwani inasemekana taarifa zilitumwa kutoka Globeleq London (Kampuni iliyokuwa inaendesha Songas) kuwa Guy haruhusiwi hata kuingia ndani ya jengo la kampuni na inasemekana asubuhi yake alizuiliwa na walinzi wa geti pale Songas.


Guy alitoweka na gari ya kampuni aina ya Jeep Grand Cherokee namba T917 ABM. Baadaye Songas ilimshitaki Guy mahakamani kudai gari ambalo lilikuwa ni mali ya kampuni, lakini baada ya mvutano wa kisheria ambapo kampuni iliwakilishwa na FK law chambers, inasemekana Guy alishinda kesi na Songas ilitakiwa kumlipa mkanada huyo takribani $40,000 alizokuwa akiidai kampuni. Alilipwa fedha taslimu $10,000 kwani kwa wakati huo gari alilotoroka nalo Guy lilithamanishwa $30,000 na iliamriwa aachiwe.


Mwaka 2007, Guy Picard aliajiriwa na kampuni ya kufua umeme wa dharula ya Richmond baadae Dowans, akiwa na cheo cha Plant Manager. Hata wakati tume ya Mh. Mwakyembe ilipotembelea kwenye mitambo ya Richmond/Dowans, Guy alikuwa tayari ni mwajiriwa wa kampuni hiyo na alikuwa ni mmoja wa watu waliohojiwa na tume hiyo.



Katika mahojiano na tume hiyo Guy aliwahi kunukuliwa akisema kuwa hakuona sababu iliyowezesha Richmond kupewa tenda ya kuzalisha umeme wa dharula, akimaanisha kuwa Richmond haikuwa na vigezo. Je mmiliki anaweza akaiponda kampuni yake?


Guy amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya utumbo kwa zaidi ya miaka mitano sasa na afya yake imekuwa ikizorota siku hadi siku. Mara kadhaa amekuwa akienda ng'ambo kwa ajili ya matibabu.



Tangu mwaka jana Guy amerudi nchini kwake Canada ili kwenda kutibu maradhi hayo ambayo yamekuwa yakimsumbua kiasi cha yeye kushindwa kufanya kazi zake ipasavyo, na inasemekana ameshaacha kazi na huenda asirudi tena hapa nchini. Je kama yeye ni mmiliki wa Dowans, kampuni yake amemwachia nani? Au ndio ameikimbia? Je sababu ya maradhi na kutokuwepo kwake ndiko kulikomfanya Mh. Ngeleja kudai kuwa huyu ni mmoja wa wamiliki?



Taarifa kutoka ndani ya Dowans zinasema kuwa huyu mzee hana hisa hata moja katika kampuni hiyo zaidi ya yeye kuwa mwajiriwa.

Stanley Mun'gai:
Huyu ni raia wa Kenya ambaye naye pia ni mwajiriwa katika kampuni ya Dowans. Yeye yupo katika nafasi ya Finance Manager. Alijiunga na Richmond mwaka 2006 na baadae aliendelea na Dowans baada ya mkataba kurithiwa.



Taarifa zinasema kuwa hakuna namna ambayo huyu jamaa anaweza kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo zaidi ya kuwa ni mwajiriwa.
Sikufanikiwa kupata taarifa za kutosha za huyu jamaa lakini natarajia kuzipata ndani ya siku mbili, na nitaziunganisha katika thread hii.


Swali langu Kwa Mh. Ngeleja ni kuwa: Ni wapi ametoa taarifa za hawa jamaa kuwa "wamiliki wa Dowans"?


Kwa mujibu wa watu wanaowafahamu kiundani watu hawa ni wazi kuwa Guy Picard na Stanley Mung'ai si wamiliki wa Dowans, na hii inatoa taswira kuwa hata hao wengine waliotajwa na Mh. Ngeleja si wamiliki wa Dowans.Hivyo tunamtaka Mh. Ngeleja atuletee orodha ya wamiliki halali wa kampuni ya Dowans.
 
Kuna mambo mengi yanayotia shaka katika ujio wa hyu anaejiita mmiliki wa Dowans.


  1. Imemchukua muda mrefu (takriban miaka mitano) kugundua kuwa yeye ndie mmiliki wa Dowans, baada ya kuikana alipohojiwa miaka iliyopita
  2. Kujikanganya kwenye maelezo yake kuhusu wamiliki wa kampuni. Anasema yeye ndie mmiliki pekee, wakati hati za usajili zinaonyesha sie pekee, na pidai kuwa major shareholder bila kutaja minor shareholders
  3. Aliwezaje kuwekeza pesa zote hizo na kukaa kimya mpaka mahakama iamuru alipwe?
  4. Nini kinachomfanya asitake kupigwa picha na wakati huo huo akijivunia preformance nzuri ya Dowans kwenye mradi huo wa uzalishaji umeme?
  5. Anategemea serikali (isiyomjua/isiyomfahamu) ifanyeje mazungumzo nae?
  6. Nini kinachompa nguvu ya kushughulikia na kufuatilia suala ambalo alishamkabidhi RA kulishughulikia kwa ukamilifu, wakati RA huyo huyo akidai haijui kampuni ya Dowans? Ni uwakilishi gani wa siri uliopo kati yao?
Ukiangalia kwa makini utaona kuna nia kuu ya kusafishana zaidi hata ya kudai kulipwa fidia husika. Ndio maana anadai yuko tayari kuipa TANESCO pungufu zuri la award.

Huo ni mtazamo wangu binafsi.
 
Haswaa... Sisi kweli vilaza...tena vilaza...wa wakutupa

Kuna mambo mengi yanayotia shaka katika ujio wa hyu anaejiita mmiliki wa Dowans.



  1. Imemchukua muda mrefu (takriban miaka mitano) kugundua kuwa yeye ndie mmiliki wa Dowans, baada ya kuikana alipohojiwa miaka iliyopita
  2. Kujikanganya kwenye maelezo yake kuhusu wamiliki wa kampuni. Anasema yeye ndie mmiliki pekee, wakati hati za usajili zinaonyesha sie pekee, na pidai kuwa major shareholder bila kutaja minor shareholders
  3. Aliwezaje kuwekeza pesa zote hizo na kukaa kimya mpaka mahakama iamuru alipwe?
  4. Nini kinachomfanya asitake kupigwa picha na wakati huo huo akijivunia preformance nzuri ya Dowans kwenye mradi huo wa uzalishaji umeme?
  5. Anategemea serikali (isiyomjua/isiyomfahamu) ifanyeje mazungumzo nae?
  6. Nini kinachompa nguvu ya kushughulikia na kufuatilia suala ambalo alishamkabidhi RA kulishughulikia kwa ukamilifu, wakati RA huyo huyo akidai haijui kampuni ya Dowans? Ni uwakilishi gani wa siri uliopo kati yao?

Ukiangalia kwa makini utaona kuna nia kuu ya kusafishana zaidi hata ya kudai kulipwa fidia husika. Ndio maana anadai yuko tayari kuipa TANESCO pungufu zuri la award.

Huo ni mtazamo wangu binafsi.
 
Leo kaja huyu brig. ambeye aliwahi kuikana kampuni hii zaidi ya mara mbili huko nyuma alipohojiwa na mwanakijiji. Hata RA na EL watajitokeza nao wakiwa na discount zao. Tusubiri tuone
 
hahahhahaa tz oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, yale yale alipokufa Balali kila kitu kwake....
 
Mmiliki wa Dowans raia wa Oman Sulaiman Mohammad Yahya Al Adawi amejitokeza rasmi na kuweka bayanaa kuwa Dowans ni kampuni yake na kwamba alikuwa ana nia ya kuwekeza zaidi na zaidi ila watanzania(wanasiasa dhaifu na wanasheria-siasa) wamemkatisha tamaa.

Ni matumaini yangu kuwa baada ya kujitokeza, hoja ya DOWANS itakufa na sijui wanasiasa wetu watakuja na hoja gani nyingine kutudanganya wadanganyika. Je, waliokuwa wakisema Dowans ni ya Rostam Aziz watakiri hadharani kuwa walikosea na walikuwaa wanasema wasichokijua? Je, wanaweza kumuomba msamaha R.A?
 
mbona kupata majina brela rahisi tu. muda wote hao ndio wamiliki wa dowans. mgeja alisoma tu taarifa ambayo iko pale miaka yote. rostam angepata wapi dola milioni 100 za kukunua mitambo. rostam ni dalali tu.
 
Lakini si nimewahi kusikia ati Dowans ni ya hawa

images
images
images
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom