Madudu ya Uchaguzi Mkuu wa CUF haya hapa

Sijawahi kuona watu wajinga kama hawa wanajadili mambo ya CUF badala ya mambo ya msingi kama vile gym ya bunge kuitengeneza kwa gharama ya bilion 8, au wiraza ya kilimo kutengewa bilion 51 wakati rais anatengewa bilion 50 kwa ajili ya safari zake, jamani hii kweli ni akili? Halafu mnasema ccm #1 for what? Stupidity? Kuweni na uzalendo ndugu zangu.pigeni vita ufisadi na uwajibikaji sio kila siku CHADEMA au CUF,
 
Sijui twende wapi tukajifunze maana ya demokrasia. Kwani ukikosa au ukiacha uongozi ni dhambi? Kama tunataka mabadiliko ya kweli viongozi wa vyama na serikali lazima wakubali kungatuka kuachia damu changa.. vijana.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kama ilivyoamuliwa na baraza Kuu la chama, uchaguzi wa viongozi wa juu wa Chama cha Wananchi ( CUF ), ulitarajiwa kufanyika tarehe 22 Juni 2014. Katika uchaguzi huo, Katibu Mkuu Seif Sharif Hamad alihakikisha kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti ni Prof Ibrahim Haruna Lipumba na mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Mkuu ni mwenyewe Maalim Seif Sharif Hamad.

Katika hali nyingine isiyokuwa imetarajiwa na inayoleta utata ni kwamba, Maalim Seif Sharif Hamad alipendekeza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti igombewe na Juma Duni Haji badala ya Makamu Mwenyekiti wa sasa Machano Othman ambaye kwa upande mwingine ndiye anayeungwa mkono na Ibrahim Lipumba. Maalim anafanya hivyo akiamini kwamba yeye akishirikiana na Duni wataongeza nguvu ya kumdhibiti Lipumba. Wawili hao Maalim Seif na Duni Haji hawataki Lipumba agombee tena Urais na wameshamshauri agombee Ubunge Jimbo la Temeke kwenye uchaguzi Mkuu wa 2015. Juma Duni Haji ndiye aliyepangwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi wa 2015.

Halikadhalika, Maalim Seif Sharif Hamad anataka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu igombewe na Joram Bashange, Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Bukoba badala ya Julius Mtatiro ambaye hamtaki kwa sababu anambana Maalim Seif Sharif Hamad katika masuala kadhaa ya kiutendaji ya chama hicho. Sababu ngingine ya Maalim kumuogopa Mtatiro ni hisia kwamba yeye ni pandikizi la CHADEMA.

Aidha, katika kupingana na maamuzi ya Baraza Kuu, Maalim Seif Sharif Hamad ameagiza uchaguzi huo ufanyike tarehe 27 Juni 2014. Sababu ya kusogeza mbele ni jitihada za maalim Seif kupanga safu yake ya uongozi na kuwaweka wagombea dhaifu ambao watakaopambana nao. Katika kufanikisha hilo, nafasi ya Mwenyekiti itagombewa na Prof Lipumba ambaye atapambana na Chifu Rutanyosha ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Shinyanga. Kwa upande wa nafasi ya Katibu Mkuu, Maalif Seif amejipangia kupambana na mwanachama wa kawaida Adam Bakari kutoka Temeke. Kiini macho hiki kimeandaliwa ili kuwahadaa Wanachama na Watanzania kwa ujumla kwamba uchaguzi wa ndani ya chama hicho umefanyika kidemokrasia.

Makamu Mwenyekiti wa sasa Machano Othman ameshinikizwa ajitoe kwenye kinyang'anyiro hicho na nafasi yake itachukuliwa Juma Duni Haji ambaye atashindanishwa na Said Abdallah kutoka Micheweni. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu itachukuliwa na Joram Bashange kama nilivyoeleza hapo juu. Hii maana yake ni kuwa Julius Mtatiro amekalia kuti kavu ndani ya CUF na soon atatangaza maamuzi magumu ya kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA.

Wadau, mnajionea wenyewe jinsi vyama hivi vinavyojiita vya upinzani ambavyo vina ndoto ya kuing'oa CCM vilivyo na siasa za kinafiki na kilaghai. Yaani mtu mmoja tu ndiye huamua nani agombee na nani asigombee. CUF mungu mtu wao ni Maalim Seif, CHADEMA yupo mzee Edwin Mtei na NCCR yupo James Mbatia. Hakika kwa mwendo huu kuitoa CCM madarakani ni ndoto za mchana.


Nawasilisha

SOURCE: Mimi Mwenyewe kutokana na ukaribu wangu na vyanzo muhimu ndani ya CUF.

Jitihada zako za kutaka kuvuruga ushirikiano wa UKAWA zitagonga Mwamba tu
 
Sijui twende wapi tukajifunze maana ya demokrasia. Kwani ukikosa au ukiacha uongozi ni dhambi? Kama tunataka mabadiliko ya kweli viongozi wa vyama na serikali lazima wakubali kungatuka kuachia damu changa.. vijana.
Hakika Mkuu. Lipumba amechuja sana. Alipaswa kuwaachia vijana waongoze chama
 
Back
Top Bottom