Madudu CCM hayaupi hadhi upinzani kushika dola

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Maendeleo huchagizwa na viongozi bora. Siasa nayo ndiyo huzalisha viongozi. Sentensi hizo mbili zinatosheleza ufafanuzi kuwa kama nchi zinahitajika siasa safi ili kupata matokeo mawili kwa mpigo; viongozi bora na maendeleo.

Inapotokea kwenye nchi kunakuwa na siasa ambazo hazikidhi hadhi ya kuitwa siasa safi, vyama na wanasiasa wanakosa misingi ya kujipambanua kwa ujenzi wa hoja, hapo matarajio huwa ya aina mbili kwa mkupuo; kukosa viongozi bora na maendeleo yenye unyoofu.

Zifahamu siasa za kigotcha (gotcha politics). Gotcha ni neno la Kimarekani ambalo limetokana na maneno mawili “got you”, yaani kunaswa au kukamatwa. Ukiambiwa gotcha maana yake ni got you, kwamba umenaswa. Gotcha politics ni siasa za kuviziana, kutafuatiana makosa ili kumkamata mpinzani wako. Siasa za ‘kipaparazi’.

Mwanasiasa anajikita kwenye kutafuta kasoro za mpinzani wake na kuzipigia mbiu ili zijulikane. Ndiyo maana siasa za kigotcha zikawa ni aina fulani ya siasa za kipaparazi. Husemi ubora wako ni nini mpaka upewe nchi, wewe unakazana kusema upungufu ya mwenzako.

Sawa, unaweza kusikika sawia kwa jinsi unavyochambua upungufu wa mwenzako, je, hiyo ndiyo sifa ya kukufanya upewe nafasi badala yake? Siasa za kutafuta kasoro ya mpinzani na kuipigia debe ijulikane inaitwa utapeli kwa sababu unautumia udhaifu wa mwenzako kama mtaji wa kisiasa.

Wananchi wanahitaji kukuona ulivyo bora ili wakuamini na wakuchague. Haitakiwi wakuchague kwa sababu wameona mwenzako amejaa kasoro. Unamfanya mwananchi akuchague akiwa hajui unakwenda kufanya nini katika uongozi wako.

Siasa za kuviziana hazijengi. Ni siasa za ulaghai. Viongozi bora hupambanuliwa na jinsi ambavyo wanajijenga kisiasa. Wanapambanua rangi zao na kuwaaminisha wananchi kisera, kifalsafa na kiitikadi.

Wanajiweka wazi kwa yale ambayo wanayapigania. Inakuwa rahisi kutabirika kuwa wakipewa mamlaka nini watafanya. Hizo ndizo hasa zinatakiwa kuitwa siasa safi. Siasa za kujipambanua kuliko kujificha kwenye mwavuli wa makosa ya wapinzani.

Tanzania inahitaji tiba

Siasa za kuviziana kuliko kujipambanua ndizo ambazo zinachukua nafasi kwa sasa chini. Chama Cha Mapinduzi (CCM) wapo tayari kuwekeza rasilimali zao kwenye kuutangaza upungufu wa wapinzani, kama ambavyo wapinzani wanavyokuwa wepesi kupigia debe kasoro za CCM.

Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii, hakuna siri tena kuwa CCM wana watu wao wa kushambulia na kutetea, kama ilivyo wapinzani. Nguvu kubwa inajikita kumtazama hasimu, kuchambua kasoro zake na ‘kuzibeba bango’ ili zifahamike kwa uwanja mpana.

Wale wa CCM, jukumu lao ni kutetea pale chama chao kinaposhambuliwa na kushupalia kasoro za wapinzani. Vivyo hivyo kwa wapinzani mitandaoni, wao ni kupiga mbiu kwenye ule udhaifu wanaouona CCM na kukosoa yote yanayofanywa. Wakikosa la kukosoa, wanaona bora wanyamaze kimya.

CCM wanayo majukumu mawili tu, kukitetea chama chao kisha kutazama kasoro za wapinzani wote na kuzisemea. Wao hawana rafiki kwenye upinzani. Kila chama cha upinzani wanapambana nacho kwa uzito sawa, inategemea na wakati husika.

Wapinzani wao wanayo majukumu mengi zaidi, kila chama kina watu wake wa kukitetea kisha kutazama kasoro za CCM na kuzishikia bango. Kazi nyingine ya vyama vya upinzani ambayo ni ngumu zaidi ni kutazama udhaifu wa wao kwa wao na kuupigia debe.

Mathalan, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinajielekeza kwenye upungufu wa ACT-Wazalendo, kama ambavyo ACT-Wazalendo kinavyoziona kasoro za Chadema kama mtaji wa kisiasa. Vita ya wapinzani kwa wapinzani.

Kabla ya kuwepo kwa muungano wa vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Chadema kilikishambulia Chama cha Wananchi (Cuf), kama ambavyo Cuf nacho kilivyokuwa kinayatolea macho na kuyasemea yaliyokuwa yanajiri ndani ya Chadema. Ilikuwa hivyo pia hata kwa NCCR-Mageuzi na Chadema.

Hili la wapinzani kushambuliana wao kwa wao limekuwa mtaji mzuri kwa CCM, maana ni kawaida hasimu wako anapokuwa na mahasimu mbali na wewe, kipindi ambacho anakong’otana na wengine, wewe unabaki unapumua, ukitazama mchezo unaishaje.

Ikiwezekana yule hasimu ambaye haguswi, hutazama mgogoro husika na kufanya uchochezi ili mapambano yaendelee. Vievile anaweza kuusaidia upande usio na madhara kwake au wenye hatari ndogo dhidi ya hasimu wake mwenye nguvu.

Ndege mpya na mgogoro Cuf

Sakata la ununuzi wa ndege mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATC) liliibua hoja za ushambulizi na utetezi. Kulikuwa na upondaji mkubwa kutoka kwa wapinzani, vilevile utetezi wa kiwango cha juu ulifanywa na vijana wa mtandaoni wenye kujipambanua kuwa wafuasi wa CCM.

Wapondaji hawakuwa na na kazi nyingine zaidi ya kuponda aina ya ndege zilizonunuliwa Bombardier Q400, kwamba hazina hadhi. Hawakuishia hapo walijenga hoja kwa historia ya ndege kubwa zilizowahi kununuliwa nchini lakini hivi sasa hazipo kutokana na sababu tofauti.

Hoja za wapondaji ziliingia mpaka kwenye kufananisha kuwa Tanzania kama taifa kubwa na lililo na utulivu wa katosha kwa miaka yake 55 ya Uhuru, inashindwa na Rwanda na Somalia zenye historia ya machafuko, vileveile ni nchi ndogo.

Kwamba mashirika yao ya ndege yenye kubeba bendera za taifa, RwandAir na Somali Air, yanamiliki ndege kubwa aina ya Boeing na Airbus zenye kubeba abiria mpaka 300, wakati ATC imenunua Bombardier Q400 yenye wastani wa kubeba watu 70.

Watetezi kwa kasi kubwa nao wakawa na hoja ya kwa nini imekuwa mwafaka kununua Bombardier Q400 badala ya ndege kubwa. Sababu nyingi walitoa kuhalalisha na kupongeza uamuzi huo ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliutekeleza wa kununua ndege hizo mpya.

Baadaye zilipoibuka taarifa kuwa mwakani kuanzia Machi, Serikali ina malengo ya kuinunulia ATC ndege kubwa aina ya Airbus, upande wa utetezi ambao ulisema mengi kuhalalisha uamuzi wa ununuzi wa Bombardier Q400, ukaibuka tena na sifa kemkemu kuhusu ujio wa Airbus.

Suala la ndege linavyoamsha hisia za mgawanyo wa pande mbili, zinakuja pia na namna ambavyo CCM wanavyofurahia mtifuano wa sasa ndani ya Cuf. Siyo uongo kuwa kuyumba kwa uongozi Cuf, kunatoa nafuu kubwa kwa CCM na Serikali yake, hususan Zanzibar.

CCM ni wanufaika wakuu wa mgogoro wa Cuf, maana endapo katika vuta nikuvute ya sasa, itakibakisha chama kwenye mikono ya Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba, maana yake majaliwa ya Ukawa yatakuwa shakani. Kuvunjika kwa Ukawa ni afya kwa CCM.

ACT-Wazalendo wanamtetea Lipumba. Kama ambavyo Chadema wanavyojiweka wazi kuhakikisha Lipumba habaki na chama. Utaona kuwa vuta nikuvute ya wapinzani wao kwa wao, inaipa ahueni CCM.

Cuf kikipasuka vipande viwili kama ambavyo dalili zinaonekana kwenda kutokea, ACT-Wazalendo wanaweza kunufaika kwa kupata wanachama ambao wataamua kujiunga nacho, Chadema na Ukawa, kuna mawili, kubaki na Cuf au watu.

Chadema na Ukawa wataweza kubaki na Cuf kama kitabaki chini ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na timu yake ya uongozi chini ya Julius Mtatiro. Hata hivyo, Chadema na Ukawa watavuna watu, kwa maana ya Maalim Seif, Mtatiro na timu yao, kama Profesa Lipumba atashinda vita ya uongozi kwenye chama hicho.

Matokeo yote yanayoendelea Cuf, mwisho kabisa ni sumu kali kwa upinzani. Hata kama baada ya dhoruba hakuna atakayejiunga na CCM, bado nguvu ya upinzani itakuwa imepungua.

Ubaya wa mwenzio si uzuri wako

Kuchunguzana na kuviziana ni siasa za umbea. Kuyasema mabaya ya mwenzako haikufanyi wewe uwe mzuri. Hili linatakiwa lifanyiwe kazi kubwa na wapinzani kuliko CCM. Maana CCM wana dola, wapinzani wanaifukuzia dola.

Si vibaya kuusema ubaya wa mpinzani wako lakini haipaswi kuwa agenda ya chama. Ubora wa chama hauwi katika kuibua dosari za chama pinzani, badala yake inatakiwa iwe kwa namna ambavyo kinajijenga kwa hoja endelevu. Kinavyojipambanaua kwa misingi yake ya kiitikadi na kifalsafa. Si hoja za kudandia.

Hii tabia ya wapinzani kujishughulisha zaidi na kasoro za CCM haina tija, maana hizo ni siasa za kipaparazi, kufuatiliana na kuumbuana, kwamba bila udhaifu wa mpinzani huwezi kujijenga. Hizo ndiyo siasa za kigotcha kama wasemavyo Wamarekani.

Wapinzani wakae na ukweli huu kuwa kuzijua na kuzisema sana kasoro za CCM, haziwapi hadhi na uhalali kwamba wanatosha kuongoza nchi, badala yake wajikite kwenye kuupambanua ubora wao kisha wafanye kazi ya kuwekeza itikadi na falsafa zao kwenye mioyo ya Watanzania. Kasoro za CCM zinapita, ndiyo maana leo litasemwa hili, kesho lile, lakini itikadi na falsafa vinadumu.

Maandishi Genius
 
You can't be great just by showing how small someone else is.

Upinzani unatakiwa uwathibitishie watanzania kuwa wao ni mbadala wa CCM kwa kuanzia na namna wanavyoendesha vyama vyao.

Watu wanajua weaknesses za CCM tayari,waonesheni strength zenu siyo kuendelea kuwaimbia chorus hizo hizo wanazozijua.

Udhaifu wa mwenye nguvu hauwezi kuwa nguvu ya wadhaifu.

CCM inaweza kuwa mbovu na upinzani ukawa mbovu zaidi.

Disclaimer:Sijasoma makala yote.
 
suala je wanaviziana kwa hoja au kwa kung'ong'ana kuhusu sura nyuso zao mbaya? poor minded people discuses people while smart people discusses issues!
 
....
....hizo nguvu ulizotumia kuandika wekeza kwenye kilimo cha mananasi
Umesoma makala? Kama umesoma naamini utakuwa umejifunza jambo.

Mananasi yanalimwa katika kila aina ya ardhi?
 
Sisiem hawataki usemwe udhaifu wao wanataka wapinzani wawafundishe jinsi ya kuwa viongozi bora eeh kituko hiki

Naona sisiem sasa wamefika mwisho wa kufikiti ndo maana zinatengenezwa skendo kwenye upinzani ili uparaganyike badala ya wao kujikita kuleta maendeleo ya nchi

Amini nawambia mkitaka kuona upinzani wanafanya nini tofauti, ni kutoa fursa za uongozi kwao bila shaka watanzania wakiona kumbe hakuna tofauti watawaacha baada ya miaka mitano tuu, lakini najua hata sisiem inajua kila mtanzania anajua kuwa siku upinzani ukiongoza serikali kuu ndio mwisho wa sisiem na mafidadi yao yote. Na kwa hivyo hawataki kuachia madaraka ili wajifunze bali wanapora uongozi na king'ang'ania madaraka wasije kufa kwa kihoro.
Tunajua viongozi na wenye sisiem yao ni waoga wa mabadiliko kuliko kufa hawataki kubadilika wala sheria na katiba zinaonyesha mabadiliko zinapingwa kwa nguvu zote, kumbukeni tuu chenye mwanzo kina mwisho na mwisho wa ccm upo karibu sana na mabadiliko ya kweli yatakuja.
 
You can't be great just by showing how small someone else is.

Upinzani unatakiwa uwathibitishie watanzania kuwa wao ni mbadala wa CCM kwa kuanzia na namna wanavyoendesha vyama vyao.

Watu wanajua weaknesses za CCM tayari,waonesheni strength zenu siyo kuendelea kuwaimbia chorus hizo hizo wanazozijua.

Udhaifu wa mwenye nguvu hauwezi kuwa nguvu ya wadhaifu.

CCM inaweza kuwa mbovu na upinzani ukawa mbovu zaidi.

Disclaimer:Sijasoma makala yote.
Huna haja ya kusoma utumbo wote,, soma sub-headings zake tu utapata picha nzima,, kwa ufupi huu ndio mwanzo wa mwisho wa upinzani Tanzania,,Angalia na soma kila siku upinzani hujikita ktk vitu visivyofaa kama vile Bunge Live, je nchi kama TZ kweli inauwezo huo kitekinolojia??? haya kuminywa demokrasia ni kudai kila mpuuzi apate jukwa la kuongelea utumbo wake,, ndio demokrasia hiyo??? haya Dikteta uchwara hiyo kweli ni lugha ya mtu aliyesoma sheria kweli au ni mtu aliyesoma KUFAULU??? Dikiteta hachaguliwi jamani na mbona hawaombi uchaguzi urudiwe??? Waje na hilo tuone kama CCM hataipata 89% Ohh uchumi unaporomoka au unadorora huku unaona wawekezaji wa kimataifa toka hadi CUBA wanakuja kuomba kuwekeza,, wapinzani wamejikita ktk kupotosha raia na ndio wanajizika wenyewe
Kwa ufupi CUF has already gone and next is Chadema you just wait and see!!!!
 
Mpango wa Mungu yupi? Ni Mungu gani anakuwa upande wa wakwepa kodi na Mafisadi?
 
Umesahau kueleza jinsi Kiongozi wenu mkuu wa ACT, Mh. Zitto anavyomchachafya Magufuli kwamba amenunua ndege za mtumba toka Kazakhstan then akazipaka rangi ili zionekane mpya. Siasa za kuviziana hizo.
 
Swala la kusemwa kwenye siasa halipingiki. na hata kama hausemwi kwenye siasa haimanidhi kwamba ww ndio mwanasiasa bora.
Ila unaweza ukawa haujishughulishi na chochote.
Yani unaishi kama tikitiki maji ambalo mtu akilisukuma linabunguruka.
 
wananchi wenyewe wanafuata mikumbo ya watu wachache katika kuchaguo viongoz kupitia madhaifu yasemwayo majukwaani na si ahadi za nn watafanya.
pia siasa zetu ndivo zilivo kuzingatia ss niwatu ambao kypitia hizo tunaona ni zakweli na pia hatuna uchungu na mali zetu kias kwamba uongoz ama kura mtu anaweza kui dump. mf mtu anakuuliza ndege zitamsaidia nn bibi yangu wa kijijin.? mh swali gani hili. au mwenye jazba kuvunja kiti.
 
Upinzani wana kosa moja linalowatafuna katk kipindi hiki nalo ni kwamba wamekosa agenda maaalumu,na hiyo inawafanya wawe wanaharakati sio wanasiasa,Pia kuna tabia Kama ya kugombana na mtu mmoja kwa kivuli cha serikali,Upinzani utafute mambo ya msingi ya kuwashawishi wananchi kuona uovu wa Chama kinachotawala vinginevyo MATAMKO YA UKOSOAJI USIO NA AGENDA,MALALAMIKO YA KUIBIWA KURA YATABAKI KUWA WIMBO,Mwisho vyama vya upinzani viwe na mikakati ya kujenga vyama ngazi za chini hasa vijijini,mahala pengine ukiiiona ofisi ya chama unakata tamaaa,waache kujikita mjini pekeee,Siri ni kwamba CCM hupata kura nyingi vijijini ambako watu siku ya kupiga lazima washiriki sasa wenzangu Wa mjini wanakuwa bize na kusaka hela.
 
Umesahau kueleza jinsi Kiongozi wenu mkuu wa ACT, Mh. Zitto anavyomchachafya Magufuli kwamba amenunua ndege za mtumba toka Kazakhstan then akazipaka rangi ili zionekane mpya. Siasa za kuviziana hizo.
Kweli siasa za kuviziana Hazina nafasi CHA MHIMU KUWA NA AGENGA ZA KUDUMU,sio Leo mnapinga hili,kesho mnapinga lile na kusubiri keshokutwa watafanyaje mpinge,HIYO HAPANA huuuuu ni uanaharakati kitu ambacho ata mkongwe E LOWASA anakikataaa.
 
Back
Top Bottom