MSAKA-UHURU
Member
- Sep 5, 2012
- 12
- 0
Sisiem na sera ya nguv mpya har mpya na kas mpy! ina maana watafkia maamuz ya kufunga viwanja vyote vya wazi coz of cdm?
Sakata la uwanja wa NMC kugeuzwa na kuwa hifadhi ya wamachinga imechukua sura mpya baada ya madiwani wa CCM kumgeuka meya gaudence lyimo na mkurugenzi kuwa ajenda ya kubadilisha matumizi ya uwanja huu haikufikiwa hitimisho.
Diwani mmoja wa kati ya maeneo ya mjini mjini amesema kuwa awali madiwani walikuwa wameridhia kuwa uwanja uliopo karibu na soko la kilombero utumike mahaliilipokuwa stendi ya semunge. Baadae kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa iliingiwa na hofu baada ya chadema kuubatiza uwanja huo kuwa ni uwanja wa ukombozi - chadema square na hivyo uamuzi wa kuuchukua uwanja huo ukafanyika kiholela holela kwa hamaki bila vikao vya maamuzi kukaa.
Diwani huyo amesema kuwa kiutaratibu uwanja wa wazi unapobadilishwa matumizi unatakiwa utangazwe kwa siku 21 na inapokuwa hauna pingamizi ndipo mkurugenzi anapotangaza mabadiliko ya uwanja wa wazi na matumizi mapya. Katika mazingira haya madiwani wa CCM wameonyesha kulalamika kwa vile vitu vidogo vidogo hivi vimekuwa vingi na vya kizembe na ndivyo vimekuwa vikiwapa chadema nguvu na hoja za kuonyesha ubabaishaji na udhaifu katika uendeshaji wa halmashauri ya arusha mjini kwa ujumla.
Nanyaro Ephata sio wala suala la kufanyia vikao tuu ni suala la kupanga mji unaendaje
Unawezaje kukaa na jiji halina uwanja wa wazio hata mmoja hata bustani ya jiji hakuna zaidi ya tu- round about na visehem kama pale ofisi ya mkuu wa mkoa au soweto pale kati kati ya makazi ya watu
Huyo mtu anayueeamua kuwa pale wawekwe machinga alifikiria nini na je haoni kuwa pale mbele ya uwanja kuna shule ya secondary
Huo usumbufu wanafunzi watauzoeaje au ndio mpango wa kuua kabisa ile shule isisikike tena
Naonewa tuu mkuu Ngoja utaona wiki simaliziHabari za kifungoni mkuu?
Nionavyo huu ni mpango kamili wa kuwagombanisha CHADEMA na wamachinga. Kama CHADEMA watapinga mpango huo wapinzani wao wataweza kujenga hoja hasi kuwa CDM hawawajali wamachinga.Hapa lazima kuwa makini sana.
Nionavyo huu ni mpango kamili wa kuwagombanisha CHADEMA na wamachinga. Kama CHADEMA watapinga mpango huo wapinzani wao wataweza kujenga hoja hasi kuwa CDM hawawajali wamachinga.Hapa lazima kuwa makini sana.
Maamuzi haya ni ya KIWENDAWAZIMU,maana kwenye vikao hilo lilipingwa na wadau wengi kwa hoja kuwa kama ikitokea maafa yoyote Arusha hakuna uwanja mwingine wa wazi zaidi ya NMC.Pressure kubwa imetoka kwa Rc na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa lengo la kuidhofisha CHADEMA Arusha,pamoja na ule mpango wake wa kuwatumia vijana kupita mtaani wakitukana viongozi wa CHADEMA
RC amekuwa ndio Meya,ndio Mkurugenzi ndie mipango miji
kama vipi wabanwe waeleze nan alikuwa nyuma ya maamuzi yao, maana lazima kuna mkono wa mtu
waache wapambane na sijui mara haukufikiwa maamuzi
maana ya arusha ni mengi yanafanywa kiholela hata uuzwaji wa uwanja wa wazi ulio Kilombero pale ulifanywa bila maamuzi
Kila mtu Arusha hii anafanya kile ambacho anakiona cha maana au akishakuwa madarakani ana maamuzi yale ya kivyake na maamuzi ya pamoja ila mengi ni maamuzi ya mtu mmoja mmoja
| ||
|