Madiwani wa CHADEMA Arusha wamfukuza mkurugenzi wa TAMISEMI

Am not Mandela.....we do not think the same....am Michelle he is Mandela.....we differ in opinions.....:coffee:
Fine madam; but we're here for exactly those reasons - we're great thinkers and great thinkers do not necessarily think the same. There will always be arguments and counter-arguments before we reach a consensus or even a disagreement!.
 
Madiwani wa CHADEMA na Mbunge wenu wafanyabiashara wadogo wa Arusha wanasubiri kwa hamu MACHINGA COMPLEX, sasa kama mtaendelea kusuguana na serikali sijui ni Serikali ipi itakayotenga bajeti kwa ajili ya kutekeleza ahadi hiyo ya CDM. Kwa kuwa CDM haijaunda Serikali, kubakia kuwa WATCH DOG kwa Halmashauri ya Arusha ni afadhali kuliko kuongoza.

Kama hiyo complex ilitegemea pia mchango wa halmashauri ni wazi kuwa ccm wakiwa ndio meya hawatatenga fungu hilo kwani kufanya hivyo itakuwa kumpa ulaji huyo mbunge/diwani wa cdm. Ndiyo maana unaambiwa kwanza kiongozi (meya) awe aliyechaguliwa kwa ridhaa ya watu then awatumikie; huyu wa kuchakachua hawezi!
 
Katika semina elekezi,madiwani wa chadema waibana serikali,kuanzia mkurugenzi tamisemi,RC,DC wakishinikiza ufafanuzi juu ya uchaguzi wa meya.Katika hali ya msisitizo wamemfukuza mkurugenzi wa tamisemi,na msimamo wao ni kutomtambua meya.
Hadi kieleweke
Nguvu ya Umma!!!
 
Tunapongeza hatua hiyo, lakini ni muhimu kujua ya kuwa wananchi wanahitaji maendeleo. Chadema wanahitaji kufanya yale ambayo wamewaahidi wananchi. Kama kesi waifungue mahakamani na waendelee kuwafanyia kazi wananchi. Hata mahakama za Arusha zinajua haki iko wapi. Ni muhimu sana sasa madiwani na mbunge wao wa Arusha wakaanza kazi ya kutimiza ahadi zote za CDM kwa wana wa Arusha. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Arusha.

unategemea wafanyeje chini ya meya asiekuwa wa wananchi na ambae yupo kwenye system mbovu? au hujui kazi za meya?
 
Nafikiri wanachofanya chadema ni utoto na usaliti kwa wananchi waliochagua madiwani toka chadema. Wananchi wanategemea madiwani wawe chachu ya maendeleo na si vinginevyo. kususia meya, mkurugenzi, Rc na Dc bila kwenda mahakamani ni kuwanyima wananchi haki yako ya kuwazungumzia na kuwapelekea maendeleo ambayo wanayasubiri kwani bila kwenda mahakamani miiaka mitano itaisha bila kufanya lolote.

Siasa wakati mwingine inahitaji simple reasoning badala ya kutumia msuli hali kuna njia nzuri tu, pia kuangalia je kususia na kutaka maelezo kutasaidia nini bila kwenda mahakamani kama sheria inavyotaka endepo kuna hoja ya msingi. Hivi collegemate wangu Tundu Lissu ndiyo anavyowashauri kisheria, kama ni yeye basi atakuwa kalewa siasa na kasahau sheria.
 
Waanze kazi ya kuwatumikia wananchi,manake hawshindwi fika 2015 wakigomea Meya na kusema ndo sababu ya kutotimiza ahadi zao kwa wananchi.....:coffee:
For God's sake ondoa kiherehere chako hapa kabla hujapatakibano unasikia wewe m....a....l....?
 
Ina maana Madiwani wa CCM ndio wanaowatumikia wananchi, my foot.
 
For God's sake ondoa kiherehere chako hapa kabla hujapatakibano unasikia wewe m....a....l....?

Mkuu Usimtishe wa kumtukana MICHELE

Kila mtu anahaki ya kutoa mawazo yake, pia kumbuka si kila Mwaan JF ni chadema, kuna wengine hawana vyama, wengine CCM, CUF, NCCR n.k, wengine ni Activists wa mambo mbalimbali. Lakini bado wana haki ya kutoa mawazo yao bila kutishiwa. Sasa kama mnatisha watu hivi mkipewa uongozi si ndiyo mtaua na kunyima watu kali ya kuongea.
JF ni jukwaaa la kila mtu, " a forum where a member could dare to talk openly" without threat
 
Ina maana Madiwani wa CCM ndio wanaowatumikia wananchi, my foot.

Hata madiwani wengine kutoka vyama vya siasa, ila madiwani wa chadema wanapogomea kazi za halmashauri ni kusaliti waliowapa kura ili wawatumikie kwa kuwapelekea maendeleo. na maendeleo kufika kwa waliokuchagua kuwa meya yatategemea jinsi ambavyo diwani unajenga hoja za kutetea wananchi wako na kushawisi maendeleo yaqfanyike kwenye eneo lako ambapo hauhitaji mpaka uwe na meya anaetoka kwenye chama chako
 
Wao CCM waendelee na kazi zao kwani mwaka jana walizifanyaje bila madiwani wa Chadema, CDM ina utaratibu wake.
 
Habari za ndani ya mji wa Arusha, la kwanini meye wa mji wa Arusha ang'ang'anie nafasi ambayo hajachaguliwa ki uhalali ni kwamba yuko pale kulinda maslahi ya wa kubwa kwa garama yoyote, pale Arusha kuna mashamba yanaitwa mashamba ya Burka. yako karibu na makao makuu ya TANAPA na kwa Askofu wa jimbo kuu katholiki arusha, yaani kwa ujumla ni sehemu yenye mandhari nzuri sana hali ya hewa nzuri, ndo lango la jiji la Arusha, sasa hayo mashamba yalikuwa yanamilikiwa na mwekezaji kwa ajili ya kilimo cha kahawa, serikali ikaamua imlipe huyo mwekezaji pesa zake maeneo hayo wagawiwe wananchi kwa ajili ya kujenga majumba ya biashara,kilicho tokea maeneo hayo inasemekana yameshagawanywa kisiri, na hakuna mwananchi wa Arusha aliye pata kitu wamechukua watoto wa vigogo kutoka Dar na sehemu zingine lakini mwananchi wanaendelea kusubiri ngawo, sasa chadema walilijua hilo na wakasema wanaichi lazima wapewe maeneo, sas huyo bwana yuko pale kwa ajili ya kulinda hayo maeneo.
 
Waanze kazi ya kuwatumikia wananchi,manake hawshindwi fika 2015 wakigomea Meya na kusema ndo sababu ya kutotimiza ahadi zao kwa wananchi.....:coffee:

Mambo ya Sheikh Yahya mwachie mwenyewe. Embu tuambie kazi za kutumikia wananchi kweye semina elekezi ni zipi?
 
Madiwani wa CHADEMA na Mbunge wenu wafanyabiashara wadogo wa Arusha wanasubiri kwa hamu MACHINGA COMPLEX, sasa kama mtaendelea kusuguana na serikali sijui ni Serikali ipi itakayotenga bajeti kwa ajili ya kutekeleza ahadi hiyo ya CDM. Kwa kuwa CDM haijaunda Serikali, kubakia kuwa WATCH DOG kwa Halmashauri ya Arusha ni afadhali kuliko kuongoza.

I beg to differ hapa.. mi naona kila mtu apewe haki yake, kama CCM walishindwa na wao si ndo wana serikali kwa nin wanang'ang'ania Halmashauri ya Arusha? mi nadhani CDM wamechoka kuwa watchdogs wakat nchi inazidi kutafunwa.. as you know kelele za chura!!... umewadia wasaa wa CCM kukaa pembeni na kuwa watchdogs wakiangalia kama wenzao watafanya makosa kama waliyokuwa wanafanya,

Nadhani ahadi za CDM zinategemea kwa ukaribu zaidi nguvu yao ya kukusanya na kusimamia mapato na matumizi katika halmashauri ya Arusha. Sasa wakiwa watchdogs watawezaje kutekeleza ahadi wakati mamlaka wanazo wengine. mi nadhani CCM wanalijua hili na ndio maana wanajaribu kila dakika kuwa kikwazo kwa CDM in Arusha. but bettre yet.. Aluta Continua, Ts a gud start for CDM hakuna kucheka na kima this time around kwani tumechoka kuvuna mabua nchi hii!!!
 
Nafikiri wanachofanya chadema ni utoto na usaliti kwa wananchi waliochagua madiwani toka chadema. Wananchi wanategemea madiwani wawe chachu ya maendeleo na si vinginevyo. kususia meya, mkurugenzi, Rc na Dc bila kwenda mahakamani ni kuwanyima wananchi haki yako ya kuwazungumzia na kuwapelekea maendeleo ambayo wanayasubiri kwani bila kwenda mahakamani miiaka mitano itaisha bila kufanya lolote.

Siasa wakati mwingine inahitaji simple reasoning badala ya kutumia msuli hali kuna njia nzuri tu, pia kuangalia je kususia na kutaka maelezo kutasaidia nini bila kwenda mahakamani kama sheria inavyotaka endepo kuna hoja ya msingi. Hivi collegemate wangu Tundu Lissu ndiyo anavyowashauri kisheria, kama ni yeye basi atakuwa kalewa siasa na kasahau sheria.

Tunafurahi kupata mitazamo ya wanasheria.. lakini Boma naomba utambue mabadiliko katika jamii si suala la kisheria peke yake nadhani unatambua kwamba CDM are talkin about "social change" na haya ni mara chache sana yanapatikana mahakamani.. rudi kwenye historia utaona mkuu' Mi nadhani kama mmoja wa wananchi waliyoichagua Chadema sijaona usaliti wao na nadhani tunazungumza lugha moja na nadhani ule wakati wa wa kuhoji kila mtu unakaribia. Kuna mwanasheria mmoja aliwah kuniambia kuna wakat watu wanavunja sheria ili we uende mahakamani kwa sababu mahakamani sio kila wakat mwenye haki ndio atakayeshinda, na hata akishinda inaweza kuwa kwa ule msemo "Justice delayed is Justice denied".

Kama mwanajamii naamini mabadiliko katika jamii mara nyingi na kama sio zote yanapatkana kwa kutunisha misuli kwa sababu the legal system mara nyingi lakin sio zote imewekwa na wenye "power" kuwalinda wao "wenye power" kwenye jamii. Na hii inaonekana.. iba kuku, jela miez 6 ila iba epa rudisha pesa uende zako, Poteza Bilioni 200+ miaka miwili!! Tafakari'
 
Tunapongeza hatua hiyo, lakini ni muhimu kujua ya kuwa wananchi wanahitaji maendeleo. Chadema wanahitaji kufanya yale ambayo wamewaahidi wananchi. Kama kesi waifungue mahakamani na waendelee kuwafanyia kazi wananchi. Hata mahakama za Arusha zinajua haki iko wapi. Ni muhimu sana sasa madiwani na mbunge wao wa Arusha wakaanza kazi ya kutimiza ahadi zote za CDM kwa wana wa Arusha. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Arusha.

Kupinga kuburuzwa ni sehemu ya kazi.

Watanzania siku zote tunashindwa kujua nini kifanyike kwanza. Mtu anapigwa kibano mpaka kieleweke.
Wananchi kamwe hawawezi kuona tofauti kwani CCM miaka yote hakuna lolote la maana walilowafanyia wananchi zaidi ya kutafuna fedha ya Halmashauri.
Madiwani wa CDM endeleni kbano na vikumbo mpaka kieleweke.
2015 Jimbo lote lenu wala msiwe na Homa wala nini.
 
Mabadiliko siku zote hayataanzia Dar wala Dodoma ni humu humu mikoani kwanza then get rid of all trashes in Dodoma.
 
SAFI SANA MPAKA KIELWEKE.sWALA SIYO KUWATUMIKIA WANANCHI SWALA NI ccm ITOKE MADARAKANI
 
Back
Top Bottom